Naomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala la mirathi

nanix

Senior Member
Oct 26, 2015
132
225
Wakuu habarini za muda huu.

Naomba kuuliza hivi katika ishu za mirathi endapo marehemu ameacha wosia na katika wosia ule umehusisha baadhi tu ya Mali zake, pia wosia ule ukiwa umetaja msimamizi wa wosia ule.

Je, kwa zile Mali ambazo hazikuorodheshwa kwenye wosia utaratibu unakuaje? Je Kuna uwezekano wa kuwa na msimamizi wa wosia na msimamizi wa mirathi?
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,418
2,000
Mtihani, lkn kuna jawabu rahisi. Kama hakuziorodhesha , basi si zake.... unless zina uthibitisho kuwa ni zake may be alipitiwa, mfano kadi ya gari ina jina lake , that is ownership, hivyo warithi watadai iongezwe,najaribu kutumia common sense ..... will dictate this supposition
 

chapangombe

Senior Member
Sep 28, 2014
149
225
Wakuu habarini za muda huu.

Naomba kuuliza hivi katika ishu za mirathi endapo marehemu ameacha wosia na katika wosia ule umehusisha baadhi tu ya Mali zake, pia wosia ule ukiwa umetaja msimamizi wa wosia ule.

Je, kwa zile Mali ambazo hazikuorodheshwa kwenye wosia utaratibu unakuaje? Je Kuna uwezekano wa kuwa na msimamizi wa wosia na msimamizi wa mirathi?
Ndio uwezekano upo kikae kikao baadaye kitambue zile Mali wapelwke mahakamani atachaguliwa msimamizi wa hizo Mali nyingine pia
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,058
2,000
Hiyo inaitwa partial testament. Hizo alizoorodhesha atathibitishwa msimamizi (executor) aliyeteuliwa na marehemu, hizo mali ambazo hakuorodheshwa msimamizi wake (administrator) atateuliwa na mahakama
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,578
2,000
Kuorodheshwa kwenye wosia hakufanyi mali hizo kuwa za marehemu automatically. Vivyo hivyo, kutoorodheshwa kwenye wosia, hakufanyi mali na madeni ya marehemu kutokuwa yake. Inategemea na ushahidi uliopo. Kwa mfano, ukiandika wosia leo, halafu kesho ukanunua gari na keshokutwa ukafa....hilo gari kuna uwezekano mkubwa lisiwepo kwenye wosia wako (kama umeataja mali na madeni). Na pia wosia unaweza kuwa kwa baadhi ya mambo tu (e.g. sehemu unayotaka kuzikwa n.k lakini mali ukaachia igawanywe kwa kufuata sheria).

Kwa ufahamu wangu, msimamizi wa mirathi ni lazima awepo either kuna wosia au hakuna.

Kazi ya msimamizi kubwa na kukusanya (taarifa za) mali na madeni halali ya marehemu na pia kuwatambua warithi halali (kisheria na kwa mijibu wa wosia). Kutumia mali ya marehemu kwanza kulipa madeni ya marehemu na sehemu inayobakia (kama ipo), kuigawa kwa wanaostahili kwa kufuata wosia na sheria.

NB: Mimi sio mwanasheria.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom