Naomba ufafanuzi wa kisheria endapo ukifanya tukio mtandaoni lakini ukiwa nje ya nchi

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,871
Naomba kuelimishwa kwa Sheria zetu za mtandao zinahusu Mtanzania yeyote aliepo popote au lazima awe anaishi Tanzania?

Ukitukana mtu Instagram sheria inasemaje Kama uko Tanzania? Kama uko nje?..

Ukianzisha kampuni ya porn mfano uko nje ya Tanzania but wewe ni Mtanzania sheria inakubana? Kivipi? Mfano upo Kenya..
 
Hiyo ni kesi ya wakenyaaa kijanaa! Kama wao wanaruhusu nendaa kachezee pono huko
 
Naomba kuelimishwa kwa Sheri zetu za mtandao ..zinahusu Mtanzania yeyote aliepo popote au lazima awe anaishi Tanzania?....
Ukiwa raia wa Tanzania unaweza kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai ambalo umelitenda popote pale duniani ilimradi tu hilo kosa litambuliwe Tanzania kwamba ni kosa.
 
Naomba kuelimishwa kwa Sheria zetu za mtandao zinahusu Mtanzania yeyote aliepo popote au lazima awe anaishi Tanzania?

Ukitukana mtu Instagram sheria inasemaje Kama uko Tanzania? Kama uko nje?..

Ukianzisha kampuni ya porn mfano uko nje ya Tanzania but wewe ni Mtanzania sheria inakubana? Kivipi? Mfano upo Kenya..
Kama huko ulipo nalo ni kosa mahakama za ndani ya Tanzania zinauwezo wa kudeal na hiyo case na kutolewa maamuzi. Kwa maana nyengine unaweza hukumiwa na mahakama za Tanzania bila shida ila sharti tu uwe ni mtanzania ambaye upo nje ya nchi na ufanye kitendo ambacho kwa Tanzania na Huko ulipo pia ni kosa.

Pia hata kama upo nje ya Tanzania kama tu hilo kosa la kimtandao umelifanya nje ya nchi lakini umedirect kwenye mfumo wa kikompyuta ambao upo Tanzania, mahakama za Tanzania zinauwezo wa kudeal na case yako vizuri tuu.
 
Back
Top Bottom