Naomba Ufafanuzi Wa Jumuiya ya WAZAZI ya CCM

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Wana JF mi dukuduku langu ni juu ya Hii jumuiya ya WAZAZI ya CCM nina maswali ambayo najiuliza kila siku lakini sipati majibu, maswali yangu ni haya yafuatayo

  1. Katika hii Jumuiya ili uwe mwanajumuia unatakiwa uwe na sifa zipi?
  2. Nini hasa lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya Hii?
  3. Na neno WAZAZI linatumika kwa maana ipi?

Nauliza haya ni kwa sababu kama tunavyojua Jumuiya za Vijana wahusika ni Vijana, Jumuiya za wanawake wahusika ni wanawake na hata kama kungekuwa na jumuiya za wanaume wangeusika wanaume na pia kungekuwa na jumuiya za wazee wangehusika wazee, sasa hii jumuiya wahusika ni akina nani?

Nawasilisha, naomba msaada wa ufafanuzi.
 
Mi nafikiri kama jina linavyojinyumbua lenyewe, sifa mojawapo na nafikiri ndio sifa kuu ni lazima uwe Mzazi bila kujali una umri wa miaka mingapi (hata kama umezaa ukiwa na miaka 9) hapa ndo panakufaa. wewe kama ni mzee lakini sio mzazi hapa sio mahala pako, tafuta jumuiya nyengine
 
Mbona Le Mutuz umri umeenda na hana mtoto ila ni kiongozi mle..ama kweli mle ni chaka la magarasa ya namna ya kuendelea kukwepa kodi.
 
BREAKING NEWZZZZ.........
Abdallah Bulembo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM (T) abwagwa(avuliwa udiwani) na aliyekuwa mgombea wa udiwani kupitia CDM
 
Wana JF mi dukuduku langu ni juu ya Hii jumuiya ya WAZAZI ya CCM nina maswali ambayo najiuliza kila siku lakini sipati majibu, maswali yangu ni haya yafuatayo

  1. Katika hii Jumuiya ili uwe mwanajumuia unatakiwa uwe na sifa zipi?
  2. Nini hasa lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya Hii?
  3. Na neno WAZAZI linatumika kwa maana ipi?

Nauliza haya ni kwa sababu kama tunavyojua Jumuiya za Vijana wahusika ni Vijana, Jumuiya za wanawake wahusika ni wanawake na hata kama kungekuwa na jumuiya za wanaume wangeusika wanaume na pia kungekuwa na jumuiya za wazee wangehusika wazee, sasa hii jumuiya wahusika ni akina nani?

Nawasilisha, naomba msaada wa ufafanuzi.
Hii jumuiia ni moja ya zao la mambo ya hayawani ambacho hakina lolote bali kuwapa wazee wa kiume ulaji tuu na kutoa wabunge wasio na lolote la maana ki uchumi. kuna jumuia za kiajabu ajabu kama mbili hivi ambazo hata ukizipima ki uzani, hazina maana yeyote ya kujenga uchumi ila kuongeza wingi tuu kutapanya hella katika vikao na uchaguzi.

wewe jiulize jumuia ya wazazi na vijana zina lengo gani ki uchumi? mwaka juzi kuna mhindi alitoa 400 million za kuendesha uchaguzi wa jumuia ya vijana, je hawa vijana wanafaida gani kimtazamo wa kiuchumi? marekani demokratic na republican hawana jumuia zozote za wanawake, wazee wala viajana na wapo juu sana kiuchumi. sasa sisi tupo masikini sana kiuchumi, lakini kila kukicha kuna majuia yanapewa ulaji ulaji tuu na kugharimu mamilion ya hella kuendesha uchaguzi wao. je turafika jamani?

swali lako nimelipenda na nilikuwa naliandikia hoja gazetini ila umeniwahi sana kuuliza. mimi napinga sana majuiya haya ya wanwake, wazee na vijana, maana sioni faida yake kiuchumi wala kijamii. ila kuwapatia ulkaji tuu watu bila maana yyte!
 
Endelea kuandika hii hoja huko gazetini kwani ni muhimu kuielimisha jamii kupitia media mbalimbali si wote wanaopita humu JF. Lakini kinachonishangaza hadi sasa sijajibiwa maswali yangu hii inamaanisha hakuna anayejua lolote kuhusu hii Jumuiya wakiwemo pia walioianzisha?
 
le mutuz anatafuta majibu muda si mrefu atakuja na pumba zake

Ndugu Majibu hawana maana hawajui wapo katika hiyo Jumuiya kama akina nani na wapo hapo kwa ajili ya nini na inawezekana wote waliopo sasa ni wapya na waasisi hawapo na hawakuacha chochote kinachohusiana na Jumuiya hii kwa hiyo sasa wanafuata Mkumbo tu kujiita wanajumuiya ya WAZAZI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom