Naomba ufafanuzi wa jambo hili kuhusu laini za simu zetu

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,856
2,953
HABARI ZENU

Nimeona niandike hapa Jamiiforum kwa kuamini hapa ni jungu na pia wahusika wakuu wapo humu na wanapitia hapa japo kimya kimya

Licha ya watu kusajili laini zao kwa alama za vidole ila matapeli wameendelea kutusumbua. Je, kwanini TCRA haiwakamati? Na kama wametumia vitambulisho vya wengine kusajili laini hizo kwanini wamiliki wa vitambulisho hivyo na mawakala waliosajili laini hizo na kuziuza kwa matapeli hawakamatwi?

Swali langu la mwisho, na je kama mtu alisajili kwa kutumia kitambulisho cha kupigia kula ila baada ya mfumo wa alama za vidole laini yake ikafungiwa na akaamua kusajiri laini nyingine kwa jina lile lile kwa kutumia kitambulisho cha taifa uwezekano wa kupatikana mtu huyo upo kwa kuangalia majina yake katika system ya TCRA?

Asanteni sana naombeni majibu kwa maswali hayo machache.
 
Hili swali kujibiwa ndo muziki mwingine.
Ajabu zile namba ukipiga unaambiwa hazipo,na ukiwauliza wenye mtandao wa simu wanakwambia hawazijui.
 
Nahisi hii JF hakuna wataalamu wa maswala haya bali maswala ya mapenzi na chitchat.
Hili swali kujibiwa ndo muziki mwingine.
Ajabu zile namba ukipiga unaambiwa hazipo,na ukiwauliza wenye mtandao wa simu wanakwambia hawazijui.
 
Ila hawa jamaa wanafurahisha sana aisee.
Ukiwsshtukia unapokea matusi mazito mazito.
 
Mimi sijawahi maliza wiki bila kunipigia au kunitumia sms mara za uganga mara kakosea kutuma pesa.
Ila hawa jamaa wanafurahisha sana aisee.
Ukiwsshtukia unapokea matusi mazito mazito.
 
Niliwahi sikia tetesi eti jamaa wana mtambo toka israel,,hivyo wanaspoof number
 
Laini zinazotumika zimesajiliwa bila ridhaa ya wahausika. Je Wanazipataje? Pale mtu anaposajili kwa alama za vidole, wakala (hawa wanaotemebea mtaani) anatumia muda huo huo kusajili nambari zingine kwa kutumia ID yako bila mwenyewe kutambua , kuwa makini na wakala anaekwambua rudia rudia kuweka alama za kidole wakati wa usajili. Baadae hizi namba huwa wanauzia hao matapele kwa bei nzuri tu.
 
Back
Top Bottom