Naomba ufafanuzi: Upendo Peneza kwenye ziara ya Waziri Mkuu Ruangwa

hii makinikia hata mimi ningeiteua
Ğh
Kwani tatizo liko wapi?
Yeye hajajiuzulu

Kwani huyo ni Waziri Mkuu wa CCM au wa JMT? Mbona unajitoa ufahamu mchana kweupe hivi?

mimi sitaki kabisa kumzungumzia huyu binti klatika siasa kwa kweli, huyu binti ni mashine aise sintojiuliza maswali nikimuona kokote na mtu yeyote.

Sent from my SM-G355H using JamiiForums mobile app
 
idawa Ni kawaida kwa Rais, Makamu wa Rais ama Waziri Mkuu kuteua baadhi ya wabunge bila ya kujali itikadi za vyama vyao kuandamana nao kwenye ziara kama hizo. Kinachofanywa kwenye ziara hizo huwa si mipango ya wanaoteuliwa kuandamana nao bali ni mwenye ziara yake.
 
Mwingine kuleeeee
Mwingine kuleeee
Sisi ambao hawatoki kwenye majimbo yetu maendeleo tusahau
Kipaumbele kwao tu

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Utamu wa pipi Ni mate yako. Hebu jaribu kutafuna jani la alovera( Igaka), halafu kula pipi kama utasikia utamu.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
idawa Ni kawaida kwa Rais, Makamu wa Rais ama Waziri Mkuu kuteua baadhi ya wabunge bila ya kujali itikadi za vyama vyao kuandamana nao kwenye ziara kama hizo. Kinachofanywa kwenye ziara hizo huwa si mipango ya wanaoteuliwa kuandamana nao bali ni mwenye ziara yake.
Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi, umenifungua Macho....japo umeacha maswali mengi kwenye uchambuzi wa wengi.......?
 
Waziri mkuu wa JMT yuko na wabunge wa JMT, hata hivyo nadhani Majaliwa ni kiongozi mwenye siasa safi siyo za chuki, ni waziri mkuu ambaye yupo poa sana habagui kama Sizonje. Wakati mwingine JPM anapingwa kwa sababu ya anavyojiweka kichukichuki na kiubaguzibaguzi

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Siasa za umaarufu zitaimaliza Chadema.... huyo mtoto mzuri lakini wapo wengi sana huku kwetu temeke wailes....

Muda utasema
 
Nashukuru mkuu kwa ufafanuzi, umenifungua Macho....japo umeacha maswali mengi kwenye uchambuzi wa wengi.......?
Mfumo wa nchi yetu ni mchanganyiko wa falsafa nyingi sana na wakati mwingine inazua mgongano wa fikra. Bunge lina pande mbili ( Parliament not National Assembly) upande mmoja ni Rais na upande mwingine ni wabunge. Kwa maana nyingine wabunge zaidi ya mia tatu nguvu yao ni sawa na mtu mmoja ambaye ni Rais.

Na ndiyo maana Bunge linaweza kwa kutumia wingi wao wakamuondoa (Impeachment) Rais madarakani. Lakini naye rais anao uwezo wa kulivunja Bunge. Kwa mantiki hiyo Rais na wabunge nguvu zao ni sawa. Sasa hawa kuanzia Rais Mpaka waziri Mkuu huwa wanachagua wabunge wa kuongozana nao kwenye ziara wanazofanya, wenyewe wanadai wabunge wakaone serikali inafanya nini.

Serikali hutoa taarifa bungeni kueleza wabunge watakaoongozana na viongozi hao ili kama wana majukumu mengine wasihesabiwe kuwa ni watoro. Tatizo ni mitizamo ya siasa zetu kuwa za kiaudui na kuviziana. Kiongozi anaweza kutumia fursa hiyo kumshawishi Mbunge ama mbunge anaweza kutumia fursa hiyo kuharibu ziara ya kiongozi.
 
Nimeona Upendo Peneza viti maalum Chadema kwenye ziara ya Waziri Mkuu wilayani Ruangwa wakigawa pikipiki kwa vijana wa ccm.....Naomba ufafanuzi hiyo ziara inahusiana na nini.?

=============================
Updates

Mbunge viti maalum CHADEMA kutoka Mkoa wa wa Geita, Upendo Peneza ameungana na wabunge wa CUF wa Mkoa wa Lindi katika ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mkoa huo.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa, Peneza amewaomba wananchi waliombee taifa ili liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

"Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa."

Mbali na Upendo, pia mkutano huo ulihudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Hassan Masala (Nachingwea), Zubery Kuchauka (Liwale), Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

Kwa pamoja wabunge hao wamesema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi maendeleo

Chanzo Azam news.

My take....
Je hii inaashiria nini kwa chama cha Chadema, je Chedema kimegawanyika rasmi kuhusu serikali ya Magufuli.?
Au nae amenunuliwa kama madiwani wa Arumeru.

kama unaona kinyongo basi ondoka chdema yetu.kiazi mkubwa wewew
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Mfumo wa nchi yetu ni mchanganyiko wa falsafa nyingi sana na wakati mwingine inazua mgongano wa fikra. Bunge lina pande mbili ( Parliament not National Assembly) upande mmoja ni Rais na upande mwingine ni wabunge. Kwa maana nyingine wabunge zaidi ya mia tatu nguvu yao ni sawa na mtu mmoja ambaye ni Rais.

Na ndiyo maana Bunge linaweza kwa kutumia wingi wao wakamuondoa (Impeachment) Rais madarakani. Lakini naye rais anao uwezo wa kulivunja Bunge. Kwa mantiki hiyo Rais na wabunge nguvu zao ni sawa. Sasa hawa kuanzia Rais Mpaka waziri Mkuu huwa wanachagua wabunge wa kuongozana nao kwenye ziara wanazofanya, wenyewe wanadai wabunge wakaone serikali inafanya nini.

Serikali hutoa taarifa bungeni kueleza wabunge watakaoongozana na viongozi hao ili kama wana majukumu mengine wasihesabiwe kuwa ni watoro. Tatizo ni mitizamo ya siasa zetu kuwa za kiaudui na kuviziana. Kiongozi anaweza kutumia fursa hiyo kumshawishi Mbunge ama mbunge anaweza kutumia fursa hiyo kuharibu ziara ya kiongozi.
Mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi wako, japo watu kama wewe wanazidi kupungua siku hadi siku jf .

Vipi kuhusi huo uteuzi kwenye ziara za Waziri Mkuu kambi ya upinzani huwa inahusishwa hasa kwa wabunge wa upinzani.?
 
Vipi kuhusi huo uteuzi kwenye ziara za Waziri Mkuu kambi ya upinzani huwa inahusishwa hasa kwa wabunge wa upinzani.?
Kambi ya Upinzani uhusishwa sema kutokana na huo woga wa kurubuniwa na hizo siasa za kuviziana huwa kuna kuwa na mashaka kwa nini Mbunge fulani kateuliwa. uteuzi huo kwa mfano kama unahusishwa na mbunge anayeonekana ana mahusiano mazuri na wana CCM huzua taharuki.
 
Back
Top Bottom