Naomba ufafanuzi: Upendo Peneza kwenye ziara ya Waziri Mkuu Ruangwa

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,311
Nimeona Upendo Peneza viti maalum CHADEMA kwenye ziara ya Waziri Mkuu wilayani Ruangwa wakigawa pikipiki kwa vijana wa CCM. Naomba ufafanuzi hiyo ziara inahusiana na nini.?

=============================
Updates

Mbunge viti maalum CHADEMA kutoka Mkoa wa wa Geita, Upendo Peneza ameungana na wabunge wa CUF wa Mkoa wa Lindi katika ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mkoa huo.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa, Peneza amewaomba wananchi waliombee taifa ili liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

"Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa."

Mbali na Upendo, pia mkutano huo ulihudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Hassan Masala (Nachingwea), Zubery Kuchauka (Liwale), Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

Kwa pamoja wabunge hao wamesema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi maendeleo

Chanzo Azam news.

My take....
Je hii inaashiria nini kwa chama cha CHADEMA, Je CHADEMA imegawanyika rasmi kuhusu serikali ya Magufuli.?
Au nae amenunuliwa kama madiwani wa Arumeru.
 
images%285%29.jpg
images%284%29.jpg
images%283%29.jpg
images%282%29.jpg
images%281%29.jpg
images.jpg
 
Huyu mtoto hata mimi ningemteua twende naye kwenye mizunguko yangu. Hupati uchovu wa safari. Siyo unachagua kuongozana na mijitu imechoooka...safari inakuwa ngumu maradufu.
Vipi ukipewa katika ziara yako Juliana Shonza kama alivyokuwa Mwigulu hamuachi itakuwa vipi?
 
Mbona upendo kaongea poa tu, au wewe kwasababu umesikia mangi kicheche hata ukimuona wife anaenda kununuapo bidhaa basi mangi anakula zigo

Sent from my GT-I9105P using JamiiForums mobile app
 
Aina hii ya siasa ndio kazianzisha baba mwenye nyumba.Siasa za visasi na kutokupongezana,kwa vile baba mwenye nyumba alionyesha kuwatembelea au kuwapa pongezi watoto wa nyumba ya jirani ni kama "uhaini",sasa hata wale wa nyumba ya jirani wanasadikishwa kuwa kumpongeza au kuandamana na baba mwenye nyumba ni "uhaini".

Si ajabu Jumuiya ndogondogo ya Mtakatifu Thomas More kule bungeni imevunjika,si ajabu waliotaka kumuona Lema bungeni walitengwa,tupo njiani kuanza kuacha kuzikana.Maana alishatoa angalizo,shughulika nao huko mjengoni,mimi nitapambana nao nje.

Mkwere na mapungufu yake,siasa za "kistarabu" aliziweza sana,ndio maana ziara zake nje ya nchi aliongozana hata na Wabunge wa upinzani.

What a mother goat does,a child goat should follow!!Wana-mbuzi wanapandikizana chuki zinazotokana na tabia ya Mama-Mbuzi....Political Torelance and Political Pluralism is what we lack in the 5th regime
 
Back
Top Bottom