Naomba ufafanuzi treni ya SGR haitakuwa inabeba mizigo?

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,630
3,578
Ukitazama picha hata mwanzo wa reli yake imeanzia station ya zamani hamna reli iliyoelekea bandarini
Pia hapo station reli yenyewe ipo juu sana naomba ufafanuzi nijue kuwa itakuwa ya kubeba watu tu ama na mizigo?
DFC7C3D4-15CC-47D5-8A66-A00251E9ACE2.jpeg
 
Itakuwa inabeba mizigo toka bandari ya Dar hadi bandari kavu huko Kwala. Kuna route nyingine itakuwa inatoka bandarini
 
Inajengwa lini na wapi itakutana na ile imejengwa juu kwa juu
Sijui 😂, ila najua kuna bandari kavu imejengwa ili mallory yasije dar, yapokee mizigo huko huko ili kupunguza foleni, so for sure najua itabeba mizigo, nikiona michoro ya design naweza nikajibu hayo maswali yako.
 
Sijui 😂, ila najua kuna bandari kavu imejengwa ili mallory yasije dar, yapokee mizigo huko huko ili kupunguza foleni, so for sure najua itabeba mizigo, nikiona michoro ya design naweza nikajibu hayo maswali yako.
Bas labda mizigo iwe inaenda kupakiziwa huko bandari ya nchi kavu lakini pia inakuwa ni kama
Usumbufu na gharama
 
Kama Taifa tuna safari ndefu sana. Pamoja na vipindi vyote vya TRC kwenye redio, televisheni, ziara za viongozi mara kwa mara, maelezo kadha wa kadha kutoka Serikalini, nk Bado hujajua SGR kazi yake kubwa Ni Nini? yaani isafirishe watu kwenda Burundi, Rwanda, DRC?

Dah
 
Aulizae bila shaka anataka kujua!. Treni ya abiria inakuwa na sehemu au "Shelf"za kuweka mizigo ya kawaida ya kilo 20+ kwenye maungio. Ndani ya mabehewa kuna "Carrier" za mizigo zilizo zoeleka kwa juu. Sidhani kama mtu ataruhusiwa kuingia na mzigo unaizidi kilo 20+ ndani ya behewa, labda kama kutakuwa na behewa mahususi kwa mizigo mikubwa. Ikumbukwe kuwa hii itakuwa seti moja ya treni ya abiria inayojulikana kwa kingeri kama "Rolling Stock".

Treni ya mizigo itaanzia Kwala bila shaka itahudumia mizigo inayotoka bandalini, reli yake ipo tena sambamba na reli yetu ya mita gauge ambayo inagawanyikia meneo jirani na Machiga Complex huenda ikajengwa kwa kiwango cha SGR. Nadhani mizigo mikubwa itabebwa zaidi na reli ya mita gauge maana ile huwa na mabehewa maalumu ya mizigo. Nimejaribu tu kushiriki kwenye mjadala huu kama mdau wa usafiri wa reli, nadhani wenye TRC yao watatujuza kwa mapana zaidi;).
 
Bas labda mizigo iwe inaenda kupakiziwa huko bandari ya nchi kavu lakini pia inakuwa ni kama
Usumbufu na gharama
Hapo chini ya hiyo " Viduct ya SGR" itajengwa tena ile reli yetu pendwa ya mita gauge, hiyo ndio itakuwa punda wa mizigo nadhani 🤔
 
Reli ya SGR itajengwa kufika bandarini hicho kipande kilihitaji usanifu na gharama za fidia kwaajili ya kupata njia kwa maelezo ya TRC ni kwamba tayari wako hatua za mwisho kukamilisha ili wamkabidhi mkandarasi ni kipande kama 5km double track hadi bandarini ila kwa sasa Treni ya mizigo SGR itaanzia kwala dry port kwenda central route
 
Back
Top Bottom