Naomba ufafanuzi toka wafuasi wa CCM na viongozi wao - Mabeberu ni kina nani, ni nchi wahisani au wafadhiri?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,743
Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?
 
Mabeberu wanapotoa misaada wanakuwa wahisani..... wahisani hawa hawa wanapogeuka na kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali basi muda huo huo wanageuka kuwa MABEBERU.

Uzuri uliopo majina haya yote mawili yaani UBEBERU na UHISANI wameshayatambua.
 
Mabeberu wanapotoa misaada wanakuwa wahisani..... wahisani hao hao wanapogeuka na kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali basi muda huo huo wanageuka kuwa MABEBERU.

Uzuri uliopo haya majina yao yote wameshayatambua.
Kama ni hivyo huo ni unafiki ambao ni first class kabisa
 
Babeberu ni jina la kumkaripia/kumuonya mdau wa maendeleo akikosa ungwana. Mhisani ni jina la kiungwa la beberu wakati akiwa muungwa.
 
Inashangaza sana kutowaona makada wa CCM wakikwepa kueleza jambo hili huku kila siku wakitumia maneno “ametumwa na mabeberu”, “vita dhidi ya mabeberu” nk. Hata Lissu anashutumiwa kwa “kuwatetea mabeberu”!!

Tokeni sasa kueleza jambo hili au hata mseme ni propaganda tu ya kupumbaza wapumbavu na kuwafikirisha warevu!!
 
Inashangaza sana kutowaona makada wa CCM wakikwepa kueleza jambo hili huku kila siku wakitumia maneno “ametumwa na mabeberu”, “vita dhidi ya mabeberu” nk. Hata Lissu anashutumiwa kwa “kuwatetea mabeberu”!!

Tokeni sasa kueleza jambo hili au hata mseme ni propaganda tu ya kupumbaza wapumbavu na kuwafikirisha warevu!!
Hawawezi kujibu chochote hadi Babu yao Pole pole atakapoperuzi Kamusi ya CCM Mpya na tafsiri ya neno hilo lazima liidhinishwe na Stone.
 
Babeberu ni jina la kumkaripia/kumuonya mdau wa maendeleo akikosa ungwana. Mhisani ni jina la kiungwa la beberu wakati akiwa muungwa.
Kwa hiyo beberu na mhisani anakuwa mtu huyo huyo mmoja. Nikiwa mhisani wako ukawa unaniita beberu nyakati fulani kwa kweli sahau mambo ya uhisani!

Ila hata hivyo kuna matumizi mabaya ya neno beberu. Kwa mfano, chama cha upinzani kinapoambiwa mkawaambie rafiki zenu mabeberu, huko ni kumuita mtu beberu pasipo kuwa amefanya kitendo unachosema si cha kiungwana. Unafiki unaingia hapo
 
Ni mtu mmoja, inategemea tu kafanya nini siku husika.. mfano, akitoa msaada anakuwa mfadhiri na akihoji matumizi ya msaada alioutoa anakuwa BEBERU
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kama ccm huwa wanatumia neno mabeberu kumaanisha wale wanaoinyonya nchi yetu basi itoshe kusema
Ccm inaongoza kwa kuwa na mabeberu wengi wanaoinyonya nchi yetu tena kwa mabavu na kwa sheria za kinyonyaji.
 
Back
Top Bottom