Naomba ufafanuzi taasisi ya elimu (Chuo) kutoa gawio kwa Serikali

Ultimate

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
713
1,736
Hello Bosses,

Nimeshtushwa na hili. Je, ni halali kwa taasisi ya elimu kuwa chanzo cha mapato kwa Serikali?

Nimeshtuka kuona IFM kutoa gawio karibia billion 2, juzi hapa nimemlipia dogo ada 1,800,000+, ada tu bila hostel hela ya kula na kujikimu.

Tumefika mbali sana hadi elimu ni chanzo cha mapato, kwa wanaojua naomba ufafanuzi juu ya hili.
 
Kama ni taasisi ya serikali, ama ikiwa serikali inamiliki % ya hisa kwenye taasisi hiyo, na ikiwa kama taasisi hiyo inafanya biashara.

Basi kwa vigezo hivyo, ni sahihi serikali kupokea gawio la faida kutoka kwenye taasisi husika.

Asante
 
Sasa ulikuwa hujui? Kama elimu ni gharama jaribu ujinga
Hello Bosses,

Nimeshtushwa na hili. Je, ni halali kwa taasisi ya elimu kuwa chanzo cha mapato kwa serikali?

Nimeshtuka kuona IFM kutoa gawio karibia billion 2, juzi hapa nimemlipia dogo ada 1,800,000+, ada tu bila hostel hela ya kula na kujikimu.

Tumefika mbali sana hadi elimu ni chanzo cha mapato, kwa wanaojua naomba ufafanuzi juu ya hili.
 
Shangaa NIDA wanaopokea kila senti na hawafanyi biashara eti leo nao wanatoa gawio

Sema wewe ndo hujui ili uelimishwe....Moja ya mapato ya NIDA ni pale unapotaka kupata namba yako ya kitambulisho kwa kutumia mtandao wa simu...kuna makato ya shilingi 100/= ambayo yanapokelekwa kwa mfumo wa Malipo ya serikali
 
Ukipoteza Kitambulisho Unalipa Tshs 20000/=
Uweze Kupatiwa Kingine, Wanastahiri Kulipa Gawio Serikali
 
Kwa hiyo wataka nambia kati ya vitambulishi walivyotoa. Vimepotea zaidi ya vitambulisho 100000 laki 1?
Ukipoteza Kitambulisho Unalipa Tshs 20000/=
Uweze Kupatiwa Kingine, Wanastahiri Kulipa Gawio Serikali
 
Saa zingine tumia akili usijifanye mjuaji.
Wametoa Bilioni 2 na point je maana yake walioulizia vitambulisho ni watu milioni 20?
Sema wewe ndo hujui ili uelimishwe....Moja ya mapato ya NIDA ni pale unapotaka kupata namba yako ya kitambulisho kwa kutumia mtandao wa simu...kuna makato ya shilingi 100/= ambayo yanapokelekwa kwa mfumo wa Malipo ya serikali
 
Sema wewe ndo hujui ili uelimishwe....Moja ya mapato ya NIDA ni pale unapotaka kupata namba yako ya kitambulisho kwa kutumia mtandao wa simu...kuna makato ya shilingi 100/= ambayo yanapokelekwa kwa mfumo wa Malipo ya serikali
Unapotoa gawio maana yake unajiendesha bila ruzuku ya serikali. Sasa ni kweli kuwa hiyo 100/= inatosha kujiendesha na kupata faida!
 
Nimeona Chuo cha fedha IFM ikiwemo katika mashirika ya umma yaliyotoa gawio/ mchango kwa serikali. Wangetoa billion 2.

Vyuo vyote vya umna vina matatizo sugu ya upungufu wa vitendea kazi. Vimekuwa na wanafunzi wengi kupita uwezo wake.

Hizo ni taasisi za umma zenye kutoa huduma na kimsingi hawafanyi biashara. Ndiyo maana wanapata ruzuku toka serikalini.

Sasa nashangaa uwezo huo wa kutoa gawio/mchango wameupata wapi. Hata kama wanaingiza fedha kwa kufanya consultancy, kwa nini wasitumie fedha hizo kutatua baadhi ya changamoto walizonazo?

Tena kwa maneno ya Rais, wamevichongea vyuo vingine. Sitashangaa kuona UDSM, UDOM, ARU nao wanatoa gawio ingawa wanashindwa kuendeleza vyuo hivyo kwa ukosefu wa fedha. Lengo limekuwa kumfurahisha Jiwe.

TTCL kinara wa kutoa gawio sijawasikia mwaka huu. Mwaka jana walitoa Billion 2 lakini wakaomba Trillion moja!
 
Siasa zitatupeleka pabaya. Hata taasisi zisizofanya biashara pia zinatoa gawio.

Nchi masikini hua haziendelei kwa sababu nyingi sana. Wenzetu hizi drama hua hazipo.
Sasa unataka wafanyaje wakati necha ya awamu hii ni comedy?

Au unajitoa ufaham kuwa hujui, ndio utaratibu wa sasa, wewe kama ni mkuu wa tasisi yoyote ya serikali unapaswa kutafuta kiki, usaniii na comedy uweke hadharani mbele ya mkuu, la sivyo basi uwe unaalika vyombo vya habari kama Sendeka unasifia hadi kero, halafu unatoa hela unampa mwandishi unamwelekeza kuwa hiyo habari hakikisha mkuu ameiona.
 
Sasa unataka wafanyaje Wakati necha Ya awamu hii ni comedy? Au unajitoa ufaham kuwa hujui, ndio utaratibu wa sasa, wewe Kama ni mkuu wa tasisi yoyote Ya serikali unapaswa kutafuta kiki, usaniii na comedy uweke hadharani mbele Ya mkuu la sivyo basi uwe unaaalika vyombo vya habari Kama sendeka unasifiaaaa hadi kero Halafu unatoa hela unampa mwandishi unamwelekeza kuwa hiyo habari hakikisha mkuu ameiona
Wapi tena nimejitoa ufahamu?
 
Back
Top Bottom