Naomba ufafanuzi kwa mwenye taarifa kamili suala la GPA 3.8 kwenye ajira

Muda wa kusoma mkawa mnakimbizana kwenye maandamano na kupiga deki barabara sasa hivi mnaanza kusumbua.

Wenye uwezo ndo watakaoajiriwa.
Hahaha aise binafsi nilitaka kujua tu GPA yangu ipo vizuri tu msomi akipata jambo hulidadisi na hii ndio njia moja wapo ya udadisi .
 
Naomba kuuliza nimesikia kua ajira za mwaka 2016-2017 lazimq uwe na gpa ya 3.8 sawa kama ni kweli naomba ufafanuzi kwa mwenye taarifa kamili na kwa wale wenzangu na mimi ulipewa mkopo na hukufikisha gpa iyo so hautapata ajira? Na huu utaratibu umeanza saiz kwa walio maliza hapo nyuma si utawaathiri wengi au anyway naomba ufafanuz ili nami nielewe. Naomba kuwasilisha

Kama ni kweli hayo maamuzi ndiyo yameafikiwa na Mamlaka au Uongozi husika basi itoshe tu kusema kuwa Watanzania tuna matatizo makubwa katika baadhi ya nyaya zetu zilizopo katika bongo zetu.

Nimeshafanya tafiti moja miaka mitatu tu iliyopita ambapo niligundua kuwa 99.999% ya Wafanyakazi wenye GPA za kuanzia hiyo alama yako tajwa hapo ndiyo wanaongoza kwa kuboronga na utendaji mbovu huku Maofisini / Makazini.

Pia sikuishia tu hapo nikachukua hatua kadhaa ya kuwauliza Watanzania wenzangu waishio Ulaya na Wazungu wawili watatu ambao ni Marafiki zangu juu ya suala zima la GPA na ajira kwa huko Ulaya. Majibu ambayo niliyapata kutoka kwa yote yalikuwa yanafana kuwa huko Ulaya kinachoangaliwa zaidi ni performance ya Mfanyakazi na siyo GPA yake.

Na tatizo hili ndilo limeharibu mno Sekta ya Ualimu / Ukufunzi / Uhadhiri humu Vyuoni kwani kuna Wanafunzi wengi tu wana Vipaji na Uwezo wa Kufundisha ila wanaachwa na kuchukuliwa wenye GPA hizo kubwa na matokeo yake hakuna kinachofanyika zaidi tu ya kupotezeana muda. Pitia Vyuo Vikuu kadhaa utashangaa Wahadhiri waliokuwa na GPA kubwa ndiyo wanaongoza kwa kutojua kukufunzi ila kuna Vichwa ambavyo vilikuwa Chuoni na vina GPA ndogo tu lakini katika deliverance darasani wako vizuri na wanakubalika sana. Na hapa nitoe tu pongezi kwa Chuo Kikuu kimoja hapa hapa Tanzania kwa kuliona hilo ambapo karibia 75% ya Wahadhiri wao wa sasa ni Vijana wenye Vipaji na Wito japo GPA zao ni ndogo ila hiko Chuo Kikuu sasa kinasifika kwa kuzalisha Wachapakazi wa ukweli.

Tujifunze kutofautisha kati ya GPA kubwa na actual competency ya Mtu. Siafiki kwa 100% Serikali kutumia mfumo huu wa Kipumbavu kabisa katika kuajiri Wafanyakazi / Watumishi wake na nitalipinga kwa nguvu zote hasa kutokana na kwamba ni mwana jamii na najua kinachoendelea on the ground pengine kuliko hata hao wachache walioamua na sana sana naona tu kuwa kuna tabaka fulani linataka kutengenezwa hapa au mpango wa kuwakomoa Watu au Kundi fulani. Siku nyingine kabla ya kuja na haya maamuzi yenu ambayo sioni aibu wala woga kuyaita ni ya Kipumbavu muwa mnafanya tafiti kwa wenzetu waliotuzidi ili tuweze kujifunza na tusije kuonekana ni Kituko.
 
Chanzo ni wenye kauli pale elimu inapoingiliwa na siasa uchwara
 
Muda wa kusoma mkawa mnakimbizana kwenye maandamano na kupiga deki barabara sasa hivi mnaanza kusumbua.

Wenye uwezo ndo watakaoajiriwa.
Wewe kwani GPA ni matako kila mtu anayo? usiongee kwa kuwa ww unayo hiyo gpa angalia wingi wa mtoto wa kitanzania, aliyekuwa akisoma huku akiwaza kusomesha, wadgo zake na kulea familia yake usibwatuka tu hapa
 
Mi ningekuwa muajiri ningezingatia form 4 na form 6 papoje maana siamini kwenye Gpa maana kuna GPA za chupi na kujuana ila hakuna GPA za chupi wala kujuana kwa sisi tuliosomea mtaala wa DIVISION
Mkuu huko sahihi. Lakini form six kufaulu sana inategemea unasoma comb gani , eg hgl, pcm etc
 
km ungetumia akili yako kidogo tu kufkiri hbr hii uloskia,, naamini ungepta mjb na usingeileta hp..hii mitandao ya kijamii inaondoa uwezo wa kufkr.jambo dogo m2 anataka asaidiwe.
 
Back
Top Bottom