Naomba ufafanuzi kuhusu tatizo hili la moyo

zink

JF-Expert Member
Sep 18, 2021
924
1,477
Habari wakuu natumaini wote wazima wa afya.

Kuna siku ilitokea kwa ndugu yangu mmoja hivi umri 29 years mapigo yake ya moyo yalikua yanadunda haraka sana, hali hiyo ilipelekea kwenda hospitali ya taifa ya muhimbili kwa ajiri ya vipimo na alivyofika muhimbili kitengo cha cardiac Jakaya walimpima matatizo yafuatayo;
1.kisukari
2.pressure
3.ugonjwa wa figo
4.ugonjwa wa moyo

Yaani kwa kifupi walimpima magonjwa yote na majibu yakawa mazuri yani alionekana mzima kila kitu ila walimpatia dawa kama mapigo ya moyo yakienda kasi atumie ila badae hali ikapote hivyo akaacha kutumia dawa.

Lakini pia walimfungia kifaa ambacho kitakua kinampima pressure na mapigo ya moyo kila dakika 60 na kifaa icho alikaa nacho kama week 3 hivi, badae ilibidi kwenda kuondolewa kifaa icho na majibu yakatoka na ikaonekana yupo vizuri yani haumwi wala hana tatizo lolote.

Kwa sasa hali uwa inatokea uwa kama moyo unashtuka hivi anaeweza akawa amelala, amekaa hali hiyo ya moyo kushtuka inatokea je tatizo ni nini hapo wakuu.
 
Inasababishwa na anxiety disorder. Stress na wasiwasi kwa muda mrefu husababisha hizo shida. Moyo kulipuka hovyo, kuongeza kasi sometimes mapigo kuwa 95 and above per minute, heart pounding and skipping beats...

A relax, afanye meditation, sometimes Dawa aina ya propranolol na amytriptiline zinasaidia
 
Sawa mkuu tutafanyia kazi ushauri
 
Kuna virutubisho lishe(diaterysupplements) ambazo zitamsaidia kwenye elasticity ya blood vessels ilikupitisha damu vizuri na kufunya moyo kutokupump damu kwa nguvu
Je majibu ya kipimo cha Lipid profile yalikujaje?
Kwa mawasiliano zaidi piga +255715059944 na pia utapata huduma za kitabibu bure(free consultation)
Yalikua mazuri tu ila walishauri apunguze mawazo basi
 
Ok kama hali yake bado hairidhishi unaweza kunitafuta tupo mlimani city au ukapiga hiyo namba kwa mawasiliano zaidi, hizo diaterysupplements zitamsaidia hilo tatizo lake
Sawa mkuu sahivi yupo vizuri ntakutafuta tuone na hizo dietary maana sio mpaka uumwe ndo utumiee
 
Hiyo ni hali ya kawaida ya watu wenye anxiety disorders yaani dalili zote kama za mtu anaeumwa moyo au kisukari ila akipima majibu yanakuja negative.
Apuke vitu kama soda hasa pepsi,hii huchangia sana kufanya dalili kuwa worse,
Atumie Karan game zinaitwa almonds ni nzuri sana
 
Mkuu hiyo karan game ndo kitu gan nieleweshe
 
Mkuu hiyo karan game ndo kitu gan nieleweshe
Aepuke mazingira yanayompa stress, afanye meditation, atakaa Sawa. Naongelea kitu ambacho nimekipitia na nakipitia till now. Sio hali hatarishi kwa afya japo inaleta wasiwasi mwingi. Yatapita atakaa sawa.
 
Sawa mkuu nimekuelewa shukrani
 
Dawa ya ugonjwa wa wasiwasi ni karafuu tu ndo unatibu tatizo ili kwa haraka saana
 
Back
Top Bottom