Naomba ufafanuzi kuhusu Mifuko ya jamii na SSRA

njiro

Senior Member
Nov 7, 2010
146
107
Nilikuwa nimeajiriwa sehemu. Baada ya hapo nikaacha kazi, na mafao yangu nikachukua hapo NSSF. Nikakaa mtaani bila kazi kwa mwaka mmoja (nilienda kusoma). Baada ya hapo nikabadilisha jina kisheria(kwa sababu binafsi).

Nikafanikiwa kuapata kazi sehemu nyingine nikiwa natumia jina jipya. Sehemu niliyopata kazi wafanyakazi wake wote wanapeleka mafao yao yanaenda NSSF. Nilipewa form ya kijiunga na mfuko tajwa, ila sikufanikiwa kupata namba hadi muda huu, hapa nimeishafanya kazi kama miaka mi 3 hivi so pale NSSF pesa yangu ipo kwenye suspense akaunti.

Kuna siku wakapita watu wa LAPF ofisini kwetu, nikajiunga na mfuko huo, na namba nikapata. Ila mafao yangu ya miaka mitatu yapo bado NSSF.

Swali ni hili
1. ni jinsi gani ya kuhamisha?
2. Sheria inasemaje?

Naomba ufafanuzi
 
Hilo la kubadirisha jina halina uhusiano na mulugo au mwigulu? Kuepuka usumbufu nenda ssra alpha house makochi ali hassan mwinyi road between moroco-victoria miaka mi3 hauna nssf no.? Kuna wizi hapo fuatilia usikae ofisini tu.
 
Hilo la kubadirisha jina halina uhusiano na mulugo au mwigulu? Kuepuka usumbufu nenda ssra alpha house makochi ali hassan mwinyi road between moroco-victoria miaka mi3 hauna nssf no.? Kuna wizi hapo fuatilia usikae ofisini tu.

yap hapo ndio mwisho na pia payroll master wao amwambie anapeleka wapi hizo hela..
 
kaka sheria inasema unaweza kuhamia mfuko wowote ule na haki zako zote utapata, ingawa zamani ilikua huruhusiwi, kama payroll yako inaonyesha unakatwa nssf basi fuatilia hiyo pesa yako, kwanza wasiliana na mwajiri wako kama anapeleka makato yako, pili nenda nssf wakupe mchakato kwanini hawajakupa Id yako hadi leo, chakufanya wakupe pesa zako zote plus any privilege wakikataa nenda SSRA wafuatilie hilo swala/
 
nilikuwa nimeajiriwa sehemu. Baada ya hapo nikaacha kazi, na mafao yangu nikachukua hapo nssf. Nikakaa mtaani bila kazi kwa mwaka mmoja (nilienda kusoma). Baada ya hapo nikabadilisha jina kisheria(kwa sababu binafsi).

Nikafanikiwa kuapata kazi sehemu nyingine nikiwa natumia jina jipya. Sehemu niliyopata kazi wafanyakazi wake wote wanapeleka mafao yao yanaenda nssf. Nilipewa form ya kijiunga na mfuko tajwa, ila sikufanikiwa kupata namba hadi muda huu, hapa nimeishafanya kazi kama miaka mi 3 hivi so pale nssf pesa yangu ipo kwenye suspense akaunti.

Kuna siku wakapita watu wa lapf ofisini kwetu, nikajiunga na mfuko huo, na namba nikapata. Ila mafao yangu ya miaka mitatu yapo bado nssf.

Swali ni hili
1. Ni jinsi gani ya kuhamisha?
2. Sheria inasemaje?

Naomba ufafanuzi


kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiunga na lapf, nadhani maofisa wa lapf wangetakiwa wakupe ushauri, mana ulikutana direct na wahusika, sasa unakimbilia jf acha uzoba, au ulilazzmishwa. Watanzania bwana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom