Naomba ufafanuzi kuhusu marekebisho ya form ya mkopo

ngotho

Senior Member
Jun 18, 2021
142
110
Wakuu habarini za wakati huu.

Husika na mada tajwa hapo juu, hapo nyuma form yangu ya mkopo ilikuwa na shida, kuna sehemu ilikosewa wakati wa kuaply mkopo.( Yaani alijichanganya akaandika LOCAL POSTGRADUATE badala ya LOCAL UNDERGRADUATE ).

Sasa form ikawekewa alama nyekundu pale ilipokosewa, sasa wakati wa kufanya marekebisho nilifanya marekebisho na kusubmit, lakini iliendelea kubaki na ile alama nyekundu as if haijafanyiwa marekebisho yoyote., Nikafanya tena marekebisho kwa mara ya pili na ya tatu ( niliedit, print na kusubmit) lakini form iliendelea kubaki vilevile (NOTE; form ilikuwa inakubali kufanya edition/marekebisho). watu wakaniambia et nikishafanya marebisho niache tu hivohivo, sasa nikatulia.

Jana nilipoingia kwenye account yangu, nakuta form imekuwa verified and found to be compelte LAKINI ILE ALAMA NYEKUNDU BADO IPO/ INAONESHA AS IF SIJAFANYA MAREKEBISHO.

Sasa leo jana tarehe 4 wametoa muda wa kufanya marekebisho, Je, form yangu pia naifanyia marekebisho? Naombeni mniambie cha kufanya.

Form Yang mpaka sasa inaonesha hivi sehemu zote mbili;
Screenshot_20211006-002017.png
Screenshot_20211006-001954.png
 
Kaka kama upo dar, chukua nauli kawafuate makao makuu yao ukawaeleze shida ako watakusaidia, usiamini la kuambiwa, nenda ukawaulize wahusika kabisa
GOOD LUCK
 
Kwa case yako nenda ofisini tazara kawaelezee kama uko Dar.

Samahani naomba niulize swali kwa ajuaye. Je kwa wale wenye marekebisho inabidi u print tena ukishafanya marekebisho then ukawatumie kwa EMS tena kule posta? ili wapate hard copy?
 
Kwa case yako nenda ofisini tazara kawaelezee kama uko Dar.
Samahani naomba niulize swali kwa ajuaye. Je kwa wale wenye marekebisho inabidi u print tena ukishafanya marekebisho then ukawatumie kwa EMS tena kule posta??? ili wapate hard copy?
Nadhani marekebisho ni online tu
 
Mkuu hatimaye nimeshaenda tazara, wamesema et kama imeshakuwa verified the haina tatizo lolote..

Ingekuwa na kosa lisingefanyiwa verification, kwa maana form ipo complete.
Mimi nimerekebisha toka juzi Ila sijajibiwa kitu
 
Form yako iko sahihi. Imeshakuwa verified tayari... subiri allocation mkuu( ingekuwa ina makosa wangeandika)
Chukua Pepsi baridi shushia taratibu ukiomba Mungu kila kitu kikae sawa, kwa sababu form kuwa sahihi sio guarantee ya kupata mkopo. Vigezo ni Vingi!
 
Kwa case yako nenda ofisini tazara kawaelezee kama uko Dar.

Samahani naomba niulize swali kwa ajuaye. Je kwa wale wenye marekebisho inabidi u print tena ukishafanya marekebisho then ukawatumie kwa EMS tena kule posta? ili wapate hard copy?
Ivi we baada ya marekebisho kale ka notification ka kukosea kametoka??
 
Form yako iko sahihi. Imeshakuwa verified tayari... subiri allocation mkuu( ingekuwa ina makosa wangeandika)
Chukua Pepsi baridi shushia taratibu ukiomba Mungu kila kitu kikae sawa, kwa sababu form kuwa sahihi sio guarantee ya kupata mkopo. Vigezo ni Vingi!
😃😃, Et pepsi,
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom