Naomba ufafanuzi kuhusu mamlaka ya spika kuamuru polisi nje ya bunge kukamata watu.

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,417
1,829
Nakuombeni nyie mliobobea katika mambo ya sheria na katiba ya nchi yetu mfafanue hili jambo. Navyofahamu, spika anaweza kutoa amri kwa askari wa bunge wamkamate mbunge na kumtoa nje. Lakini je, spika anapotoa amri kwamba mbunge fulani akamatwe popote alipo nje ya bunge, hiyo amri anaielekeza kupitia kwa mkuu wa polisi nchini (IGP) au anaitoa yeye mwenyewe kama spika? Je, kama anaruhusiwa kisheria na kikatiba kutoa amri kama hiyo, polisi wakigoma kutekeleza amri yake atachukua hatua gani za nidhamu dhidi yao? Swali la pili: Je, kwenye bajeti ya bunge lipo fungu la gharama za kwenda kumkamata mbunge ambaye spika ameamuru akamatwe? Tatu: je, kisheria, mbunge akimdhalilisha mbunge mwenzake anahesabiwa amelidhalilisha bunge zima au amemdhalilisha tu mbunge mwenzake? Kwa vile spika ni mbunge, je ni sahihi kusema mbunge aliyemdhalilisha spika amelidhalilisha bunge au amemdhalilisha mbunge mwenzie?
 
Back
Top Bottom