Naomba ufafanuzi kuhusu mamlaka ya baraza la kata

HPAUL

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
410
567
Wanabodi moja ya majukumu makubwa ya baraza la kata ni kutatua migogoro ya ardhi. Upande ambao haujaridhika na maamuzi ya baraza la kata hukata rufaa baraza la ardhi na nyumba la wilaya.

Maswali yangu ni kama yafuatayo;
1. Je baraza la kata husikiliza migogoro ya ardhi na nyumba peke yake au pamoja na migogoro mingine ?

2. Endapo baraza la kata pia husikiliza migogoro mingine, je upande usiokubaliana na maamuzi ya kata utapeleka rufaa yake katika chombo gani?
 
Mabaraza ya Kata kwa ufupi yamekosa weledi kwa sababu ya kukosa wataalam wa kisheria kwa ajili ya maamuzi
1.Sidhani ila kwa sababu ya njaa zao hunaingilia mambo ambayo hayausu ili tu wapige dili za virushwa
2.Upande usiokubaliana na maamuzi utaomba shitaka lipelekwe Mahakamani

Yaan haya Mabaraza yangefutwa kabisa maana ni kama vichochoro vya kupiga dili yaan hata maamuzi yao yamejaa rushwa kabisa na sometimes wanafanya kazi ambazo zipo nje ya mamlaka yao.
 
Kweli kabisa, nimeshuhudia baraza la kata likifanya kesi za mirathi tena zenye miaka zaidi ya 16 huku Mwanza.
 
ukiacha kusikiliza migogoro ya ardhi (thamani yake isizidi milioni 3) hayo mabaraza yana mamlaka ya kusikiliza baadhi ya mashauri ambayo yameanishwa kwenye sheria ya mabaraza ya kata ya mwaka 1985 kama ilivyorekebishwa muda hadi muda.

Lengo la hayo mabaraza kuhakikisha kwenye kata husika kuna amani na usalama.
 
Linaweza pia kuskiliza migogoro ya wapangaji na matatizo yote ya kodi zisizo zidi milion 5.
 
Wanabodi moja ya majukumu makubwa ya baraza la kata ni kutatua migogoro ya ardhi. Upande ambao haujaridhika na maamuzi ya baraza la kata hukata rufaa baraza la ardhi na nyumba la wilaya.

Maswali yangu ni kama yafuatayo;
1. Je baraza la kata husikiliza migogoro ya ardhi na nyumba peke yake au pamoja na migogoro mingine ?

2. Endapo baraza la kata pia husikiliza migogoro mingine, je upande usiokubaliana na maamuzi ya kata utapeleka rufaa yake katika chombo gani?
Mabaraza ya kata yalianzishwa kwa Sheria Na. 7/1985 na Sheria hii ilianza kutumika mwaka 1988. So yalianza kufanya kazi mwaka 1988. Hii ilitokana na uchache wa mahakama kipindi hicho. Na yalikuwa yakishughulika na makosa ambayo yapo chini ya jedwali (SCHEDULE) lililotengenezwa chini ya kifungu cha 9.

Mwaka 2002 kupitia sheria Na. 2/2002 yaliongezewa mamlaka ya kuanza kusikiliza migogoro ya Ardhii hii ni kutoka na matakwa ya Sheria Na. 5/1999 na sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995.

Kwa hiyo majibu sahihi ya UZI WAKO unaweza kurejea Kifungu cha 8, 9, 20 na jedwali lake la sheria ya mabaraza ya kata Na. 7/1985.

NB:
1. Kuna baadhi wanapotosha na kuita BARAZA LA KATA LA ARDHI ni makosa yanaitwa BARAZA LA KATA.

2. Mabaraza ya kata, hayana mamlaka ya kusikiliza migogo ya Ardhi maeneo ya munispaa, miji, na majiji. Hii ni kwa mujibu wa hukumu ya mahakama kuu kanda ya mtwara iliyotolea na Jaji Ngwala 2009.

(Case citations: Rehema Hamis and others v
Faudhia H. Awadhi Misc. Land Appeal No. 129 of 2009)
View attachment Ward Tribunals Act No. 7-1985.pdf
 
Wanabodi moja ya majukumu makubwa ya baraza la kata ni kutatua migogoro ya ardhi. Upande ambao haujaridhika na maamuzi ya baraza la kata hukata rufaa baraza la ardhi na nyumba la wilaya.

Maswali yangu ni kama yafuatayo;
1. Je baraza la kata husikiliza migogoro ya ardhi na nyumba peke yake au pamoja na migogoro mingine ?

2. Endapo baraza la kata pia husikiliza migogoro mingine, je upande usiokubaliana na maamuzi ya kata utapeleka rufaa yake katika chombo gani?
wanahusika na ardhi na nyumba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom