Naomba ufafanuzi kuhusu makundi ya damu kwa watoto

Mwana Mnyonge

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
518
451
Habar wandugu

Napenda kuuliza Hivi group la damu la mtoto linatokana na baba na mama magroup Yao ya damu au?

Kwa mfano kama baba na mama ni b positive mtoto group lake linakuwa ni lipi?

Ningependa kupata maelezo kwa magroup yote ya damu na mtoto anakuwa na group gani.

Asanteni
 
Kitaalamu kuna kitu kinaitwa Homozygous na Heterozygous, kama baba na mama wote ni Group B+ maana yake wanaweza kuwa homozygous au Heterozygous, isohaemaglutinogen zao zitatoa possibility nyingi sana za group la mtoto!

Mfano kama wote baba na mama ni homozygous yaani group B+ obvious mtoto naye atakuwa group B+ na kama mmojawapo kati yao ni heterozygous pia mtoto atakuwa na group B+ Endapo wote ni heterozygous, basi uwezekano Wa mtoto kuwa na magroup B+ au O ni mkubwa. Kumbuka kuwa B huwa ni dominant na O ni resessive!

Hayo ni maelezo kulingana na BIOLOGY yangu ya F4!
Karibu mwingine mwenye uelewa zaidi au tofauti na nilivyoelezea!
 
Asilimia kubwa ya group la damu la mtoto hutegemea sana group la damu la mama au baba...kwahiyo sasa group la damu la mtoto huwa linakuwa la baba au la mama
Kama baba ni group B+ na mama ni A+ basi tunategemea mtoto awe na group A+ au B+ hakula group lingine zaidi ya hayo no AB+ au O+ mtoto lazima aende kwa mzazi mmoja vinginevyo kuna asilimia mzazi mmoja mtoto sio wake😁
 
Kama baba ni group B+ na mama ni A+ basi tunategemea mtoto awe na group A+ au B+ hakula group lingine zaidi ya hayo no AB+ au O+
Mkuu, kwa huo mfano wako;

Hiyo itakuwa kweli kama kila mmoja kati ya baba na mama ni homozygous (BB + AA) ambapo kundi la mtoto linaweza kuwa AB tu.

Kama baba ni heterozygous na mama ni homozygous (BO + AA) mtoto anaweza kuwa na group AB au A. Kama baba ni homozygous na mama heterozygous (BB + AO) mtoto anaweza kuwa na group AB au B.

Otherwise, kama wazazi wote ni heterozygous (BO + AO); kuna uwezekano wa wa kupata mtoto mwenye group lolote, yaani; A, B, AB na O.

Rudia kupitia notes zako.
 
Uko sawa Mkuu pia endapo mzazi mmoja ni AB na mwingine ni O hapo mtoto anaweza kuwa na group A or B but in rarely cases ndo inatokea.
 
Back
Top Bottom