Naomba ufafanuzi kuhusu kuharibu gauge ukijaza full tank-pomoni

mzeelapa

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
1,115
389
Heshima zenu wakuu

Mara nyingi naona watu wakijaza magari yao full tank kwa kuinua tairi la nyuma upande wa tank ili lijae zaidi ya pale pump ilipokata mpaka yanaonekana karibu kumwagika na wakati mwingine wanatikisa gari ili mafuta yaingie zaidi. Je ni kweli mtindo huu huharibu gauge ya mafuta au pump (Kwa zile zilizomo ndani ya tank) au boya lililomo ndani ya tank?
 
Kimtazamo tu inaoneka unafanya kitu sicho,na ukifanya kitu sicho uwezekano wa kuharibu gauge au kitu kingine upo.

Miaka ya nyuma niliwai kufanya jambo kama hili la kujaza mafuta kwenye tank kiasi kinachotakiwa,gari iligoma kuwaka kabisa.
Ilikuwa ni mark 2,nikamwita fundi akachekiiiii akanambia punguza mafuta,nikapunguza,chuma ikawaka.
 
1617272956829.png

Mafuta jaza ujazaje haina madhara tikisa yaingiye utakavyo hata yajae na kufurika kwenye mdomo/ mlango, ile mashine /Gauge haitadhurika
muundo wa Tank kuna sehemu kwa juu umeinuka kuweka sehemu ya hewa
hivyo pump itavuta na kusukuma, yanayobaki huwa kuna mrija/pipe ya kurudisha km hayatatumika, hiyo picha ni gauge kwa baadhi ya gari za Toyota, boya likifika juu litakwambia ni F na hata ukiongeza lita 10 au kufurika zaidi ni ni F
1617273260512.png
 
View attachment 1740376

View attachment 1740382
Niliwahi kushusha Tank Mbalizi pale sababu nilipita njia mbovu likatoboka kwa bahati mbaya, likasafishwa, zibwa na kurudishiwa ila ever since that day gauge reading haiko sawa! Sasa sijajua ni namna walivyorudishia hii pampu ilikaa tofauti ama la!
 
Itakuwa ilikaa tofauti kwani Fuelpump imeunganishwa kwenye gauge na boya ndani ya Tank, ukitaka kuifungua unaitoa kwa juu ya tank unatakiwa kuchunga sana kwani ukiigusa ile fimbo /rod ya boya itajasoma ndivyo sivyo, ukiishusha sana au kuikunja unaweza shangaa mafuta yameisha gari inazima. kwa hiyokm uliigusa un-adjust angalau kwa juu ili hata lita 10 taa iwake huko kujaa sio kubaya maana gari ndogo ni lita 35 mpaka 50 ni full
kumbuka hapo kwenye gauge pia kuna switch ya tahadhari kuwa mafuta yanakaribia kufika mwisho (empty)
 
Niliwahi kushusha Tank Mbalizi pale sababu nilipita njia mbovu likatoboka kwa bahati mbaya, likasafishwa, zibwa na kurudishiwa ila ever since that day gauge reading haiko sawa! Sasa sijajua ni namna walivyorudishia hii pampu ilikaa tofauti ama la!
Walipotoa pump wameharibu sensor. Huna jinsi ni kubadili pump maana iko intergrated na hiyo fuel gauge sensor.
 
Kujaza mafuta hadi utikise gari ni ujinga ,tu , na kuhusu kuharibu gauge ni uongo pia , katika rough road tanki linatikisika sana na gauge hazifi.
Huu ujinga naufanya.

Napenda ninapolipa iwe kwenye 5 au 10.

Mfano 125K au 130K.

Tank likijaa na pump inasoma 122K. Ntahakikisha mpaka isome 125K. Mambo ya kuhangaika na chenji sitaki.
 
View attachment 1740376
Mafuta jaza ujazaje haina madhara tikisa yaingiye utakavyo hata yajae na kufurika kwenye mdomo/ mlango, ile mashine /Gauge haitadhurika
muundo wa Tank kuna sehemu kwa juu umeinuka kuweka sehemu ya hewa
hivyo pump itavuta na kusukuma, yanayobaki huwa kuna mrija/pipe ya kurudisha km hayatatumika, hiyo picha ni gauge kwa baadhi ya gari za Toyota, boya likifika juu litakwambia ni F na hata ukiongeza lita 10 au kufurika zaidi ni ni F
View attachment 1740382
Jibu la kitaalam na limenishibisha. Ubarikiwe sana.
 
Hukuwa na kidumu cha kuweka akiba?
Ukiweka kidumu cha petrol ndani ya gari kunakuwa na harufu na inawezekana ukalewa au hujui petrol ni kilevi?
Siku moja nilimuazima gari jamaa yangu, aliponirudishia nikakuta taa ya fuel inawaka baada ya kutembea kidogo gari ikazima. Ikabidi ninunue kidumu mtaani nikaende kununua petrol ya kuniwezesha kufika kituoni. Baada ya siku kadhaa jamaa yangu mwingine alifungua buti na kuona kile kidumu, alichofanya ni kukitupilia mbali huku akisema gari kama hilo halitakiwi kutembea na kidumu wakati gari lina geji kwanza kuendesha gari mpaka linawaka taa pia ni aibu. Tangu kipindi hicho geji ikionesha imebaki robo tank kwangu inakuwa ni empty, nakimbilia kituoni.
 
Back
Top Bottom