Naomba ufafanuzi kuhusu kuchukua mtoto mahakamani

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,245
Habari ndugu zangu,

Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kwa wanasheria wote mliopo humu jukwaani. Kwa kifupi nilipata elimu humu jinsi ya kumpata mtoto wangu toka kwa mama yake baada ya kutimiza miaka saba.

Sasa nilikwenda mahakama ya mwanzo na kufanikiwa kukabidhiwa mwanangu. Sasa limekuja suala jipya kuwa yule mama wa mtoto ananiambia amekata rufaa.

Na mtoto nimekabidhiwa tarehe 12 Desemba 2019. Sasa naomba kufahamu kuwa kuna uwezekano wa kukata rufaa kwa suala kama hili maana huyo mama wa mtoto ananipigia tu simu kuwa nijiandae amekata rufaa wakati mpaka sasa karibu mwezi unaisha.

Au ananitisha tu.
Lakini siogopi chochote.
Msaada wa kisheria wakuu.
Msaada wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nihaki kama hajaridhika na uamzi ,ila jiandae kutafta wakili mzuri ikitokea unahitaji ,au kama unaweza kusimama mwenyewe kizimbani sawa...ila bado sheria inakupa nguvu,anabwata hua wanajisahau kama watoto sikuzote sio wamwanamke

Samahani mkuu hivi gharama za wakili huwa zipoje?
Natamani sana niwe na wakili katika maisha yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu...
Huku kwetu Africa kama sio Tanzania, mtoto agombewi.
Kama mzazi mwenzio hataki umchukuwe mwanao, basi wemuachie tu naitafika time atashindwa kumhudumia peke yake ama mtoto mwenyewe ataanza kumsumbua kwa kumtaka baba/mama yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu hivi gharama za wakili huwa zipoje?
Natamani sana niwe na wakili katika maisha yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mawakili hawana tofauti na waganga wa kienyeji....watakupotezea muda na fedha

Mkuu...
Huku kwetu Africa kama sio Tanzania, mtoto agombewi.
Kama mzazi mwenzio hataki umchukuwe mwanao, basi wemuachie tu naitafika time atashindwa kumhudumia peke yake ama mtoto mwenyewe ataanza kumsumbua kwa kumtaka baba/mama yake

Sent using Jamii Forums mobile app

Fwata ushauri huu is the best.
 
Ndio inawezekana kwakua kukata rufaa ni haki ya kimsingi kabisaa kwa mshindwa yoyote wa kesi, usiogope, jipange vizuri.
 
Pale unagombea mtoto halafu unakuja kugundua si damu yako hebu punguzeni viranga kwani ungemwacha kwa mama yake kisha ukamuhudumia huyo mtoto ungepungukiwa nini?

Anayejua mtoto ni wa nani ni mwanamke tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mlifunga ndoa? Halafu kwanini mnagombania mtoto? Ni aibu hata mtoto anawashangaa..mnaona mnakomoana lakini anayeumia ni huyo mtoto na vuta nikuvute yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa nini mgombee mtoto mkuu, mama yake alimbeba kwa shida na maradhi ya uja uzito ya hapa na pale, akajifungua kwa uchungu, anaumia sana unavyomfanyia. Mwachie mtoto,msiwe na uhasama na ugomvi wa mtoto,akimwa,akifa,itakuwaje?
Think outside the box mkuu
 
Back
Top Bottom