Naomba ufafanuzi kuhusu hili suala la mwili kufika nyuzi joto 39

Dark mode

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
732
859
Jana usiku baada ya kutoka katika pilika pilika za hapa na pale na mfanyakazi mwenzangu ambae ni jirani yangu, muda wa kama saa sita usiku nikaenda kumgongea geto kwake kwa nja ya kuazima chaji.

jirani alipofungua mlango pamoja na ile mvua na geni alikuwa amewasha ndani kwake lakini alikuwa anatoka jasho sana, nikaamuuliza jirani kulikoni akasema anajisikia homa sana ila asubuhi (leo) atakwenda hospitali.

Asubuhi akaenda zahanati binafsi hizi za uswahilini, joto la mwili baada ya kupimwa likawa nyuzi 39. Dkt akamwambia ungeenda sehemu nyingine wangekwambia una Corona..

Basi akamchoma sindano ya kushusha homa wakamuuzia dawa ya Malaria (Orodar),nimemuacha nyumbani (geto kwake) amejilaza japo bado joto la mwili linaonekana kuwa juu hata ukimuangalia anavotoka na jasho.

Je, hii inaweza inaweza ikawa corona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari Kabisa Poleni Sana Mkuu
Kama daktar mwenye taaluma yake kasema sio Corona. No more to add

I'm on that good kush and alcohol
 
Huyo dokta analeta utani, angeuliza dalili nyingine. Mtu kua na joto kali inamaanishi mwili wake unapigana na ugonjwa flani, yaweza kua virus au bacteria.

Sasa inatakiwa kama daktari apime ajue tatizo linalosababisha ni nini sio kumpa tu kidawa na kumwambia asepe. Yaweza kua korona ndiyo ila yaweza kua tatizo jingine pia huwezi jua hadi afanyiwe vipimo. I really hope daktari alipima akagundua tatizo la si hivyo mgonjwa wenu yupo hatarini. Mnaleta utani na afya naona
 
Joto juu ni fever ipo kabla Covid -19 haijaibuka duniani

Kikubwa wamcheki vipimo vingine ikiwemo na ugonjwa pendwa ili kujiridhisha tu
 
Huyo dokta analeta utani, angeuliza dalili nyingine. Mtu kua na joto kali inamaanishi mwili wake unapigana na ugonjwa flani, yaweza kua virus au bacteria.

Sasa inatakiwa kama daktari apime ajue tatizo linalosababisha ni nini sio kumpa tu kidawa na kumwambia asepe. Yaweza kua korona ndiyo ila yaweza kua tatizo jingine pia huwezi jua hadi afanyiwe vipimo. I really hope daktari alipima akagundua tatizo la si hivyo mgonjwa wenu yupo hatarini. Mnaleta utani na afya naona
Huyo alikuwa ni Daktari wa soko huria.
 
Back
Top Bottom