Naomba ufafanuzi kuhusu hili la Muajiri kutopeleka michango mfuko wa pensheni

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
203
250
Nilikuwa muajiriwa kwenye kampuni ya vodacom, chini ya recruiting agency Erolink toka 2016 mpaka march 2017. Toka kipindi hicho Erolink hakuwahi kuweka pesa kwenye mfuko wa pension licha ya kufungua na kutoa namba mapema, mfuko ni NSSF.

Nimefuatilia kwa muajiri amekuwa akinipiga chenga kwa kusema michango alikosea akapeleka PPF, huko nako nimeenda na wamesema muajiri apeleke CONTROL NUMBER NA LEDGER.

Nilimuambia muajiri hivo vitu vinahitajika na ni mwezi wa tano sasa na nikimpigia ameniweka black list. NSSF nimeenda sana wanasema fuatilia kwa muajiri wako.

Naomba kujua njia au wapi naweza kwenda kupata ufumbuzi kwenye hii tatizo na maelekezo mengine.
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,445
2,000
Nssf ndio wanatakiwa kuhakikisha mwajili amepeleka michango yako, pia kuna adhabu wanatoa iwapo mwajili hajapeleka michango yako.
Zamani ilikuwa unapeleka malalamiko ssra lakini baada ya kuvunjwa sijui nani anashugulikia.
Nakushauri uende wizara ya kazi uonane na kamishina anayehusika na mifuko ya pensheni lakini ni vizuri unapolalamika uwe unalalamika kimaandishi kwani ni rahisi kukuruka huwa na tabia ya kupokea rushwa
 
DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,380
2,000
Wewe ni member wa mfuko mmojawapo katika hiyo? Una ID yao? Kama ndio unaweza kuishtaki bodi of trustees wa mfuko wako kwasababu wao ndio walikuwa na jukumu LA kisheria LA kufuatilia michango yako.

Kama ni LA, mpeleke muajiri CMA haraka kabla hujawa time barred.
 
Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
12,009
2,000
Sasa mkuu bora hizo nauli unazotumia kufatilia hiyo michango unywe bia.

Maana hata ikipelekwa itakubidi usubiri hadi ufike miaka 60 ndio uende kuyachukua ilihali life expectancy ya mtanzania ni 40 years.
 
emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
203
250
Sasa mkuu bora hizo nauli unazotumia kufatilia hiyo michango unywe bia.

Maana hata ikipelekwa itakubidi usubiri hadi ufike miaka 60 ndio uende kuyachukua ilihali life expectancy ya mtanzania ni 40 years.
angalau ikae huko nssf siyo waile wao
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,971
2,000
Sasa mkuu bora hizo nauli unazotumia kufatilia hiyo michango unywe bia.

Maana hata ikipelekwa itakubidi usubiri hadi ufike miaka 60 ndio uende kuyachukua ilihali life expectancy ya mtanzania ni 40 years.

Haiko hivyo chief...mimi nilikuwa nafanya kazi kampuni fulani huku mkoani...sasa nilikuwa na contract ya miaka 2...after end of contract...nikaona nifatilie michango yangu..mara ya kwanza nilikuwa LAPF baadae wakaiita PSSSF...baadae tena ikapita sheria kuwa Private sector wote tuwe NSSF...so nikajiunga na NSSF...kwahiyo nikawa nimechangia sehemu mbili ambayo ni PSSF na NSSF...kimbembe kikaanza nilipoanza kudai mafao yangu...nikienda NSSF kuchukua statement inaonyesha michango haijalipwa na kampuni...na nikimpigia mwasibu wa ile kampuni anasema imeenda,siku nikajaa sumu..mguu mpaka kwa meneja wa NSSF nikamwambia scenario yote...nikashangaa ananiambia mtu anayepost hiyo michango hayupo ila michango yangu mwajiri alishaileta ..hapo ndo nilibaini NSSF kuna mambo ya rushwa..meneja akaniambia next week itakuwa posted nikaondoka...PSSF hakukuwa na shida hawa jamaa wako vizuri...wiki iliyofata nikaibuka NSSF..nikakuta michango ime reflect..nikajaza fomu za ku claim nikaenda na PSSF nikachukua statement nika attach na ile ya NSSF ili itoke pamoja ..after completion ya kila kitu wakaniambia after 30 days..itakuwa deposited kwenye account yangu...mamaweee siku thelathin zikapita hadi ikawa mwezi wa pili cheche...nikampigia simu meneja wa NSSF nashangaa ananiambia kuwa kuna taratibu wanafanya ili wanilipe..sasa nimechoka nataka niende PCCB nikachukue za moto nije niwashikishe mana ndicho wanachokitaka. Ila utaratibu wanalipa ndani ya siku thelathini sio hadi miaka 60...
 
wacha nitafute muda, siku nizame kwa meneja kabisa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom