Naomba ufafanuzi kuhusu haya madini ya Niobium yaliyogunduliwa Songwe

Matumizi yake duniani:

niobium-in-steel.jpg
 
mkuu hayo madini yalikuwepo tangu mkoloni lakini baada ya uhuru wachimbaji ambao walikuwa wageni waliondoka na mwalimu kwa busara zake alijenga gereza ili watu wasisogelee. ni sawa na ilivyokuwa bulombola jkt na buhemba. haya yalijengwa juu ya dhahabu ila kwa kupenda kula bila kunawa maeneo hayo yalibinafsishwa na tumeachiwa mashimo
Mkuu usiasahau na KIA pale mwalimu aliagiza pajengwe uwanja wa ndege kuna tanzanite mbuguni cha mtoto.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Yanapatikana sehemu zaidi ya 4 nchi kama Brazil,Russia,Canada.Zaire na Nigeria yapo hayo. Yanatumika ktk sehemu tofauti kama kwenye MRI Scanner, space rocket na pia ktk utengenezaji wa gas pipe
Sasa mbona kazi yake kama gas barafu iliyogunduliwa ngorongoro! Mkuu usije ukawa unachanganya madawa!
 
waTanzania tunapenda sana manun'guniko.. sijasikia mtu hata mmoja ambaye ameona huo mkataba lakini watu wanalalamika mkataba ni mbovu..

Mtu mwenye akili ashajiandaa kuwahi tenda za kusupply mradi ukishaanza. Ila hawa wengine kutwa kulalama mkingojea serikali iwafanyie kila kitu..

Kila la kheri ndugu zangu.
 
Baada ya ku Google inatumika kwy gas pipeline, kuongezea ugumu kwenye metal Na form ya chemical.lkn sio kwy CT scan Na MRI
 
Me naona ni bora yangeendelea kubaki hapohapo chini,mpaka Taifa lipate uhuru mwingine wa kifikra.Na kumbuka nchi hii ni nchi pekee Duniani wananchi wake wanaishi juu ya dhahabu lakini wanashindia mlo mmoja.Yaani nchi yote hii ni madini tupu kama ile Yerusalemu ya kwenye ufunuo kama wewe ni msomaji wa Biblia.
Kwa nini mnafikiria sana mlo mmoja? Kwani kula kil saa ndio maendeleo au?
 
Sikonge....,
Kwa hiyo kwa wa post yako ya matumizi ya Niobium, tunaona kuwa 40% inatumika sana ktk kuimarisha chuma cha ujenzi wa majengo marefu na madaraja makubwa... Kwa hiyo ukichanganya na reserve kubwa ya chuma tuliyonayo nchi hii..., tuna nafasi kubwa sana ya kupiga maendeleo kwa kasi kama tutapata VIONGOZI wa kutunza jambo hili vizuri...
 
Crocodile, Heijah...,
Hii ndio mijadala inayotakiwa haswaa..., huku JF
Naomba wana JF wenye uelewa wa mambo haya wajitokeze wayazungumze mambo ya uwekezaji wa madini yetu ili na sisi wengine tuyajue...
Elimu elimu elimu...., huenda tukipata elimu kuhusu mambo haya sisi wenyewe tutaweza kuwekeza ktk uchimbaji na uuzaji wa madini yetu wenyewe....

Inabidi tusikubali kutumia "uzoefu" na "uelewa" wetu wa uwekezaji kwenye madini kwani haujawa na tija. Tuache kuzungumzia kiasi cha asilimia ya FAIDA ambacho tutagawiwa. "Tuuze madini yetu" kwa tenda. Tenda ya helium inakuwa hivi: mwekezaji atakayeahidi kulipa kiasi kikubwa zaidi per unit na kutoa mchanganuo mzuri zaidi wa uvunaji wa hayo madini ndiye anashinda zabuni. Kila anapochukua mali yetu tunapata chetu. Huu mtindo wa sasa wa kuchukua mali yetu na sisi tukaambulia peanuts eti kwa vile faida ni kidogo hautufai.

We must think out of the box. As Obama said, if we keep doing what we have always done, we will keep getting what we always got.
 
Baada ya ku Google inatumika kwy gas pipeline, kuongezea ugumu kwenye metal Na form ya chemical.lkn sio kwy CT scan Na MRI
Ct scan na MRI ni hellium ambayo imegundulika bonde la ziwa rukwa.ila hii nobium ni njia ya kuelekea tunduma maeneo ya panda hill.
 
Uzi huu huwezi kuona wale washangiliaji wa mambo yale yale toka kwa watu wale wale kwa sababu wanafikiria kama walee...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom