Naomba ufafanuzi katika hili la Torques vs Horse Power

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
53,102
53,357
Hili jambo huwa linanichanganya sana. Tuchukulie una Scenario 2 za Model Moja lets say BMW M50d na BMW x40i.

Scenario 1: Una gari ya Petrol ina 400HP na 300 lb/ft Torque.

Scenario 2: Una gari ya Diesel ina 300HP na 400 lb/ft Torque.

Utachagua ipi? Na kwanini?

Zingatia: Matumizi ya kila siku, Safari ndefu, Service and Maintanace.

Nataka nifahamu umuhimu wa Torque over Horsepower and viceversa
 
Inategemea kwenye gari unahitaji nini, mbio au kuvuta mizigo. Kwa matumizi ya kawaida horsepower iwe kubwa kuliko torque.
Ila kama gari yako inavuta trailers etc torque kubwa muhimu.

Kwa mifano yako hapo juu namba 1 itakuwa na mbio na namba 2 itakuwa na uwezo wa kupiga kazi(kuvuta trailer,kubeba mizigo,milima etc).
 
Mkuu Bavaria mimi labda niseme hivi. Kwa uelewa wangu:-

1. Horsepower inaelezea ni kwa haraka kiasi gani gari inaweza kuperform kazi fulani. Au tukiizungumzia kwa upande wa engine tunaweza kusema ni kwa haraka kiasi gani crankshaft ya engine inaweza kuzunguka(kuwa twisted).

2. Torque inaeleza uwezo wa gari kufanya kazi fulani.

Labda nitoe hii mifano miwili labda ninaweza kueleweka zaidi.

1. Malori huwa yanakuwa na Torque kubwa na horsepower ndogo. Sababu ni kwamba yanafanya kazi nyingi lakini siyo necesary hiyo kazi ifanyike haraka.

2. Sport cars huwa zinakuwa na Horsepower kubwa ila torque ndogo. Maana yake engine inahitajika izunguke haraka ndani ya muda mfupi lakini siyo kama yanafanya kazi nyingi kama ilivo kwenye malori.

Gari yenye Horsepower kubwa na torque ndogo inaaccelerate haraka kuliko gari yenye Horsepower ndogo na torque kubwa. Na kinyume chake kwenye power.

Sijui kama nimeeleweka.
 
Inategemea kwenye gari unahitaji nini, mbio au kuvuta mizigo. Kwa matumizi ya kawaida horsepower iwe kubwa kuliko torque.
Ila kama gari yako inavuta trailers etc torque kubwa muhimu.

Kwa mifano yako hapo juu namba 1 itakuwa na mbio na namba 2 itakuwa na uwezo wa kupiga kazi(kuvuta trailer,kubeba mizigo,milima etc).

Sahihi kabisa.
 
Mkuu, kwa maelezo rahisi, gari lenye horsepower kubwa, linauwezo wa kuwa na top speed kubwa kuliko gari lenye horsepower ndogo. Gari lenye torque kubwa lina uwezo wa kuchanganya haraka kufikia top speed kubwa kuliko gari lenye torque ndogo.

Sasa hapo kwenye combination ya horspower na torque inategemea saana na mahitaji ya mtumiaji. Kwa mfano wako, kwa matumizi ya kila siku, nitachukua Scenario 1: Una gari ya Petrol ina 400HP na 300 lb/ft Torque.

Hili lina uwezo wa kufikia speed kubwa sababu ya hp kubwa, na lina torque ya kutosha kulisukuma upesi kuweza kufika speed kubwa mapema kwa matumizi ya kila siku. Ndio maana gari nyingi ndogo ni za petrol. Inakuwa efficient zaidi kama priority yako ni speed hasa over a short distance.

Kwa Scenario 2: Una gari ya Diesel ina 300HP na 400 lb/ft Torque.
Nitalichukua kama nina kawaida ya kubeba mizigo au kuvuta tela, au kwenda njia yenye milima milima au offroad. Huko nguvu inahitajika zaidi kuliko speed. Ndio maana gari nyingi kubwa au zinazofanya hizo kazi nimetaja hapo zinakuwa za diesel. Mfumo wa uchomaji wa diesel unasaidia gari kupata torque kubwa kuliko petrol, hivyo linakuwa na nguvu ya kulisukuma maeneo tajwa.

So, vyote vinahitajika saana, ila matumizi yanasababisha combination ipi ya HP vs Torque kutumika. Unaweza kuta bus lina HP kidogo kuliko saloon cars nyingi tu mtaani. Ila lina torque kubwa zaidi. Sababu priority ya bus sio speed kubwa, hasa hasa over a short distance.
 
Inategemea kwenye gari unahitaji nini, mbio au kuvuta mizigo. Kwa matumizi ya kawaida horsepower iwe kubwa kuliko torque.

Ila kama gari yako inavuta trailers etc torque kubwa muhimu. Kwa mifano yako hapo juu namba 1 itakuwa na mbio na namba 2 itakuwa na uwezo wa kupiga kazi(kuvuta trailer,kubeba mizigo,milima etc).
Okay. Naongelea gari ya kawaida ya maisha ya kila siku hasa hizi SUVs.

SUVs za Europe kuna za Diesel nyingi kuliko Petrol. Najiuliza kwanini wajaze madiesel kuliko petrol?
 
Mkuu, kwa maelezo rahisi, gari lenye horsepower kubwa, linauwezo wa kuwa na top speed kubwa kuliko gari lenye horsepower ndogo. Gari lenye torque kubwa lina uwezo wa kuchanganya haraka kufikia top speed kubwa kuliko gari lenye torque ndogo.

Sasa hapo kwenye combination ya horspower na torque inategemea saana na mahitaji ya mtumiaji. Kwa mfano wako, kwa matumizi ya kila siku, nitachukua Scenario 1: Una gari ya Petrol ina 400HP na 300 lb/ft Torque...
Kwa mfano mtu anataka kununua gari lenye varieties mbili tofauti kwenye hizo scenario tofauti. Utamshauri achukue ipi ya diesel au petrol?

Ukiangalia pia maintanance and everyday running costs.
 
Inategemea kwenye gari unahitaji nini, mbio au kuvuta mizigo. Kwa matumizi ya kawaida horsepower iwe kubwa kuliko torque. Ila kama gari yako inavuta trailers etc torque kubwa muhimu.
Kwa mifano yako hapo juu namba 1 itakuwa na mbio na namba 2 itakuwa na uwezo wa kupiga kazi(kuvuta trailer,kubeba mizigo,milima etc).
Ukiangalia maintanance and everyday running costs ya hizo gari mbili. Unamshauri mtu achukue ipi?
 
Ukiangalia maintanance and everyday running costs ya hizo gari mbili. Unamshauri mtu achukue ipi?
Diesel ni high maintenance kuliko petrol engine. Diesel is more susceptible to mafuta machafu ya bongo kuliko petrol engine. Mzee ukiweka diesel chafu injectors zikifa utaambiwa moja £1500 macho yatakutoka. Ya petrol inavumilia kidogo. Kwa bongo achukue petrol engine.
NB: Nazungumzia matumizi hapa Tz
 
Diesel ni high maintenance kuliko petrol engine. Diesel is more susceptible to mafuta machafu ya bongo kuliko petrol engine. Mzee ukiweka diesel chafu injectors zikifa utaambiwa moja £1500 macho yatakutoka. Ya petrol inavumilia kidogo. Kwa bongo achukie petrol engine.
NB: Nazungumzia matumizi hapa Tz

Dah umenikumbusha kuna kipindi nilikuwa mkoa. Kuna jamaa alikuja na Landcruser V8 lake kulicheck likawa limezingua injector moja. Nilichoka niliposikia injector ya ile gari ni milioni tena used.
 
Dah umenikumbusha kuna kipindi nilikuwa mkoa. Kuna jamaa alikuja na Landcruser V8 lake kulicheck likawa limezingua injector moja. Nilichoka niliposikia injector ya ile gari ni milioni tena used.
Hizi gari mpya hasa za diesel usiue kitu inaitwa injector. Ndio maana unashauriwa kuweka mafuta vituo vinavyoeleweka na unachukua risiti likibuma unawarudia.

Tatizo ukisafiri unajikuta huna choice,mtihani uko hapo.
 
Diesel ni high maintenance kuliko petrol engine. Diesel is more susceptible to mafuta machafu ya bongo kuliko petrol engine. Mzee ukiweka diesel chafu injectors zikifa utaambiwa moja £1500 macho yatakutoka. Ya petrol inavumilia kidogo. Kwa bongo achukie petrol engine.
NB: Nazungumzia matumizi hapa Tz
Yaani diesel cars kwa kweli zinahitaji ustaarabu saana. Watu huwa wanazitamani vile bei ya mafuta ni ndogo, lakini zina changamoto saana kwenye maintenance cost.
 
Hizi gari mpya hasa za diesel usiue kitu inaitwa injector. Ndio maana unashauriwa kuweka mafuta vituo vinavyoeleweka na unachukua risiti likibuma unawarudia.
Tatizo ukisafiri unajikuta huna choice,mtihani uko hapo.
Na diesel inachakachulika kirahisi kuliko petrol. So risky inakuwa kubwa zaidi kwa gari la diesel.
 
Okay. Naongelea gari ya kawaida ya maisha ya kila siku hasa hizi SUVs.

SUVs za Europe kuna za Diesel nyingi kuliko Petrol. Najiuliza kwanini wajaze madiesel kuliko petrol?

Hahahaaa unenikumbusha mbali sana
3AFF7F5A-7FDC-443A-83D7-1A1EE9F01C2F.jpeg

Miaka ya 2010-2011 nilikua na Avensis kama hii toka UK kila siku nilikua nabishana na wahudumu sheli. Sedan Inatumia Diesel😄😄
 
Okay. Naongelea gari ya kawaida ya maisha ya kila siku hasa hizi SUVs.

SUVs za Europe kuna za Diesel nyingi kuliko Petrol. Najiuliza kwanini wajaze madiesel kuliko petrol?
Diesel inakupa higher miles per gallon. Diesel ya Ulaya ni safi, Diesel engine inapiga mzigo,SUV Europe unakuta mtu anaburuza motor home, au mkandarasi anaburuza trailer ina tools.

Kingine wazungu wachumi sana wanaangalia ipi inatumia mafuta vizuri ambapo diesel inakuwa juu. Ungekuwa unaitumia Europe ningemushauri diesel engine hata parts huko ni cheaper,ila hapa Tz sikushauri uchukue diesel.
 
Back
Top Bottom