Jskinondo
Member
- Jan 9, 2020
- 36
- 34
Kama kichwa kinavyo ongea, kutokana na janga la Corona virus pandemic, watu wana shauriwa kunawamikono kwa maji tiririka na sabuni.
Lakini siku hizi wengine wanaona kunawa maji kila wakati ni usumbufu kwahiyo hutumia sanitizer kama mbadala wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
Njia zote hizi bado zina maswali ambayo wananchi wengi hawajapata ufafanuzi mzuri.
Hii imepelekea wengine kuamini ukinawa mikono kwa maji tiririka na sababu au kupaka hand sanitizer ni suruhisho la kuviua virus vya Corona.
Binafsi hii sintofahamu bado inanichanganya kama inavo wachanganya baadhi ya watu.
Mfano 1: kwa upande wa matumizi ya sanitizer; bado sina uhakika kama nikipaka sanitizer mikononi inaweza kuviua virusi vya corona.
Najiuliza hili swali na ningependa nipate ufafanjzi sababu sanitizer bei yake ipo juu na inatakiwa itumike mara kwa mara unapo interact na mtu au watu endapo nitapata uhakika kuwa inaweza kuua corona virus na bacteria nitajitahidi kutumia.
Mfano: 2 kwa upande wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni: bado sijafaham ni sabuni zipi zina faa kutumika na zipi hazifai kutumika kunawa mikono.
Hili limepelekea sabuni zote kutumika mtaani.
Najiuliza swali hii sababu tulio wengi uchumi wetu ni mdogo wengine pesa ya kula tu ni ya kuunga unga.
Mambo yote haya yanafanyika sababu ya kukosa elimu juu ya matumizi sahihi ya hizi vitu.
Kama ilivyo kwenye wiki ya nyungu kabla ya wataalam wa tiba asilia hawajatoa mchanganyiko sahihi wa kujifukiza, wapo walio kwisha changanya miti zaidi ya sita na waliwafukiza hadi watoto chini ya miaka 3.
Ni vema hili nalo likatolewa ufafanuzi kusudi watu wasifanye mambo kwa kubahatisha.
Naamini hapa Jf tuna madaktari bingwa ambao wanaweza kutoa elimi kwa niaba ya wengine.
#Stay home# stay safe.