Naomba ufafanuzi juu ya kauli ya DC Sabaya "DESI ilivyofumuliwa na Rais Magufuli"

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,290
17,734
Wakuu habari?

Kwanza nimpongeze sana DC Sabaya jinsi alivyo weka juhudi kuwasaidia watu waliolalamika kulaghaiwa na kampuni ya Q-Net wilayani kwake.

Katika mazungumzo yake na waalimu akawauliza "bado tu hamjajifunza jinsi taasisi ya DESI ilivyofumuliwa na Rais Magufuli?"

Chanzo: Youtube channel ya Jamiiforums.



Kwa kumbukumbu zangu DESI ilisimamishwa kufanya kazi zake na viongozi wake kushitakiwa wakati wa Waziri mkuu Mh.Mizengo Pinda na raisi akiwa Mh. Jakaya Kikwete.

Mh.Pinda ndiyo alisimamia zoezi hilo.

Kwa vile mimi binadamu huenda nimesahau naomba kukumbushwa sakata la DESI lilishughulikiwa wakati wa raisi gani?
Kama nipo sahihi ilikuwa kipindi cha Mh.Kikwete basi naomba niweke rekodi sawa kama nilivyo eleza.

Wakati mwingine kama viongozi wetu au wanasiasa wanataka kutoa sifa au kukumbushia taarifa kama hizi basi wajizuie kutaja majina ya viongozi au muda husika endapo hawana uhakika wa nani alihusika.

Yakifanyika makosa kama haya mnawapa nafasi wakosoaji wenu kuthibitisha mnasema uongo sana au mnasifia sana kupita uhalisia kiasi cha kumfanya anaye sifiwa aonekane mpenda sifa kupitiliza kumbe hajawatuma.

Ilitosha kusema 'hamjajifunza jinsi DESI ilivyo fumuliwa na serikali' bila kumtaja mheshimiwa raisi.

Mwisho DC Sabaya nakupongeza sana kwa juhudi ulizofanya hadi kuwatafuta watu wa BRELA hapo hapo kwenye kikao wakupe uthibisho wa usajili wa Q-Net.

Pia naomba niwaulize jeshi la polisi na vyombo vingine vya kusimamia sheria kwanini mnasubiri mambo kama haya yaje kushughulikiwa na viongozi wakubwa wa kisiasa?

Hamkupata malalamiko ya wananchi juu ya Q-Net na hii biashara yao yenye kutia mashaka?
 
Kuna muda walamba viatu wanazidi mipaka ya kusifu na kuabudu alafu mzee Tuhuma zinakuja kumuangukia kuwa anapokea sifa za watu wengine walofanya makubwa Inakuwa point kwa Wapinzani...

Sinaga interest na Mkuu ila kuna muda namuonaga ni mtu haelewekagi yaan hana Rafiki wa kudumu au wa kupenda tabia flani ya kudumu sa yoyote anaeza kumwaga mboga. Yaani hatabiriki.

Naona Juzi hapa mzee pascal alimtabiri atamrejesha naibu ila ikabuma
 
Ila jambo la kusikitisha wengi wa waathirika wa mchezo huu hatari ni walimu. Hivi inakuwaje hawa walimu wanashindwa kuelewa kwamba hakuna fedha inayopatikana kimiujiza kwa kuweka kidogo na kupata kingi. Nothing comes out of nothing.
 
Kumbukumbu zangu zina sema DESI ilifumuliwa na JK Mrisho ...

Maana JK alivyo ingia na yy alianza vizuri lkn alikuja kupotea baada ya RICHMOND
 
Ila jambo la kusikitisha wengi wa waathirika wa mchezo huu hatari ni walimu. Hivi inakuwaje hawa walimu wanashindwa kuelewa kwamba hakuna fedha inayopatikana kimiujiza kwa kuweka kidogo na kupata kingi. Nothing comes out of nothing.
Shida ndugu yangu, yaani ikishakuwa na shida au njaaa iliyopitiliza basi jua ni rahisi sana kuingizwa mkenge
 
....Walamba viatu wanalamba viatu had kufikia hatua ile ambayo kwa Kisambaa chetu tunasema ni 'Sickening', inatia kichefuchefu!

Unamrundikia mwanaume mwenzako sifa hata zisizo zake ilimradi tu akusikie kuwa umemtaja? Kweli Sickening!

Na hapa nilidhani nguvu zake nyingi za kukoroma alipaswa pia kuzitumia kuwakoromea walimu wetu. Mwalimu. Mwalimu... Utakubalije kununua SAA ya shilingi Milioni NNE ukitaraja MTU akutengenezee Faida? Milioni NNE kwa kununua SAA??
 
Tanzanians my people ,hii kampuni ina matangazo kila kona halafu brela inakataa kuwa haiwajui kweli, na nyie walimu hii network marketing ni kama betting jitambueni au mnafikiri kwa kutumia makalio
 
Nawasifu sasa wamama wa kichaga wanaijua pesa dah, walipo ona hawaoni faida wakamua kupanda hadi kwa mkuu wa mkoa.

Ila huko kwingine tz nzima watu wamepigwa kipigo cha mbwa koko ila wapo kimia tuu, hasa DSM, kuna D9, Alliance, BF SUMA, watu wamepigwa sana hadi huruma
 
Tanzanians my people ,hii kampuni ina matangazo kila kona halafu brela inakataa kuwa haiwajui kweli, na nyie walimu hii network marketing ni kama betting jitambueni au mnafikiri kwa kutumia makalio
Usifananishe Qnet na Betting

Betting zimesajiliwa na zinalipa Kodi
 
Wakati mwingine utadhani watz hawana kumbukumbu.
Kuna mtu alitaja mwendo kasi na daraja la Nyerere na uwanja wa ndege Dar na wazo la kuhamia Dodoma
 
Back
Top Bottom