Naomba ufafanuzi juu ya hili, mbona bado tunalipia nguzo za umeme?

heavyload

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
900
497
Napata changamoto juu ya kauli hii ya Mh waziri wa nishati kuwa wananchi nchi nzima hawapaswi kulipia nguzo ili kusambaziwa umeme. Mbona bado tunaambiwa tulipie nguzo kwa mfano huku chamwino watu wanashindwa kuingiza umeme kwa kigezo cha nguzo kuwa na gharama kubwa?

Au hii kauli ya waziri inawahusu wananchi gani?
Naomba ufafanuzi wakuu kwa mwenye ufahamu juu ya hili
 
Avatar yako inatisha aiseee!!

Kuhusu swali lako ni hivi, hii ni Tanzania! Wanasiasa wana lugha za majukwaani ambazo wakati mwingine hazitekelezeki!!
 
Napata changamoto juu ya kauli hii ya Mh waziri wa nishati kuwa wananchi nchi nzima hawapaswi kulipia nguzo ili kusambaziwa umeme. Mbona bado tunaambiwa tulipie nguzo kwa mfano huku chamwino watu wanashindwa kuingiza umeme kwa kigezo cha nguzo kuwa na gharama kubwa?

Au hii kauli ya waziri inawahusu wananchi gani?
Naomba ufafanuzi wakuu kwa mwenye ufahamu juu ya hili
Na sisi huku mikoa mingine changamoto ni hiyo hiyo nasubiri jibu, OFISI WAZIRI IHUSIKE NA TANESCO YAO
 
Napata changamoto juu ya kauli hii ya Mh waziri wa nishati kuwa wananchi nchi nzima hawapaswi kulipia nguzo ili kusambaziwa umeme. Mbona bado tunaambiwa tulipie nguzo kwa mfano huku chamwino watu wanashindwa kuingiza umeme kwa kigezo cha nguzo kuwa na gharama kubwa?

Au hii kauli ya waziri inawahusu wananchi gani?
Naomba ufafanuzi wakuu kwa mwenye ufahamu juu ya hili
Funzo! Usiwe unachukulia serious kauli za kisiasa tena zinazotolewa na wanasiasa kisiasa kwa mikakati ya kisiasa!
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali Subiri nguzo za bure uonee kama hutakaa giza miaka kumi
 
waziri ni mongo, gharama za kuingiza umeme kama nguzo ziko mbali na nyumba yako ni kubwa mno kwa mwananchi wa kipato cha kawaida. nimefanyiwa survey na tanesco Manyoni-Singida kama inahitajika nguzo moja tu kufikisha umeme kwako ni Tsh. 338,000/= gharama zikiwa nguzo moja 160,000/= na nyingine zinazo baki 178,000/= ni kwaajili ya mita na waya n.k accessories ambazo tanesco watakuja nazo kukuingizia umeme. na gharama ya nguzo intaongezeka zaidi ya 160,000/= kama utahitaji zaidi ya nguzo mbili kufikisha umeme kwako.
 
Back
Top Bottom