Naomba ufafanuzi: Je, kwa hali hii aliyonayo huyu binti je inawezekana kwamba alitoa mimba?

Prodigy Oligarchy

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
571
643
Salaam,

Tuzidi kuchukua tahadhari dhidi ya Covid-19 , maana ipo na ni hatari.

Naomba niingie moja kwa moja katika mada husika;

Ni hivi, kuna ndugu yupo mkoa fulani ndani ya Tanzania. Ndugu huyu anamtoto mmoja tu, ambaye ni wa kike.

Umri wa msichana wake, ni chini ya miaka 22, lakini haishuki chini ya 20. Huyu binti elimu yake, karibia yote ya secondary alisoma shule ya bweni tena nje ya mkoa wao.

Kilichonifanya kuandika uzi huu wa kuomba msaada wa ushauri ni baada ya ndugu huyo hivi karibu kuwasiliana nami, kuniuliza ikiwa ninafahamu madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.

Sikuwa na jibu la moja kwa moja juu ya swali lake, ndipo nilipomuuliza 'kulikoni' ?
akaanza kunielezea, kwamba kwa takriban mwaka na nusu binti yake , kila anapoingia kwenye period, basi huwa anakua ni mgonjwa wa taaban, hajiwezi kwa lolote kwa chochote, na anakua na maumivu makali mno ya tumbo, yaloyopitiliza na anakua anatapa-tapa kama vile anataka kufa kabisa.

Wamejaribu kumpeleka hospital kadhaa, lakini hakuna cha zaidi sana walichopata zaidi tu ya kumpa dawa za kutuliza (amenitajia dawa, nimesahau).

Akaongeza kwamba, kuna kipindi walimfanyia vipimo, wakabaini ana viuvimbe kidogo, lakini hawawezi kumfanyia upasuaji, akasema huenda akija kushika ujauzito na kujifungua basi na vyenyewe vitaisha.

Nilimuuliza huwa inachukua muda gani, akasema ni muda ambao anakua ndani ya siku zake, ila akimaliza au akiwa mwishoni mwishoni kukaribia kumaliza, huwa anakua sawa.

Sijui tu ni kwanini, lakini mawazo yangu yalienda mbali sana, mbali mno, nikawaza/nikahisi huenda pengine binti alishawahi kutoa ujauzito , na kinachomsumbua ni matokeo ya alichofanya kwa siri.?!

Nilikumbuka likizo fulani, ndugu alifanya tu mawasiliano namie, akaniambia 'fulani likizo hii hatokuja, kwa sabahu hatorudi nyumbani, anabakia shuleni' ilinishangaza kidogo na hata ndugu yangu huyo ambaye ndiye mzazi wake ilimshangaza pia lakini akajua huwenda anatulia ili apate muda wa kujisomea zaidi.

Na cha ajabu ni kwamba, ni kitu ambacho hakikuwahi kujirudia. Ninaambiwa, Aliporudi, afya yake haikuwa yule wa sikuzote, kuna muonekano fulani wa tofauti kidogo yupo nao, mwanzoni walihisi ni kwa sababu ya shule, ila haikuwahi kubadilika, hakuwahi kurudi kwenye muonekano wake wa kawaida kama alivyokua awali (anase,a mzazi wake)

Naomba wataalamu wa kada hii ya afya, haswa ambao wamebobea kwemye mambo haya ya afya ya uzazi especially kwa wanawake, mnisaidie ikiwa mawazo yangu yapo sahihi, na kama ndio ni hatua gani za kumsaidia zichukuliwe?

Nitashukuru kwa michango yenu itakayotoa mwanga mzuri wakuweza kumsaidia.

Ahsante.

P. Oligarchy.
 
OK kwa mawazo yako, hauko sahihi

Dysmenorrhea (maumivu makali wakati wa hedhi )... Inaweza kuwa ni primary au secondary.

Hii primary haisababishwi na shida yoyote ya ugonjwa., mwanamke atalalamika sana maumivu ya tumbo la chini, kutapika, kichefu, wakati mwingine kuharisha hata nakuchoka sana

ATAKAPOZAA BASI MAUMIVU YATAKWISHA

hii Secondary ,inasababishwa na Ugonjwa au shida Fulani ya afya inayo endelea ktk maungo yake ya Uzazi, mfano, mama mwenye vimbe kwa uterus ,au PID n.k .....mwanamke atapata maumivu makali sana lkn yanaweza yasiambatane na kutapika au kichefuchefu, kuharisha n.k

Hapa Mama atalazimika kutibiwa gonjwa ambalo Ndio linalompa maumivu makali ya Hedhi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
client,
Ahsante kwa ,aoni, tiba sasa ni nini.?!
Na kuna kipimo chochote ambacho kinaweza kufanyika kubaini kama binti aliwahi kutoa ujauzito.?! Nimeongea na mwenzake (binti mwenzie) ambaye ni rafiki wa karibu sana.

Nimeongea nae kitaratibu sana, ni kama ana kiri hivi, kwamba mwenzie aliwahi kufanya hicho kitu lakini na wakati huo huo anahofia.

Hii inazidi kunipa mashaka zaidi.
 
Wasiwasi wako ni huo uvimbe uloambiwa?

Binti akifanya abortion ndani ya miezi isiyozidi miwili huwezi kumgundua, unless aseme mwenyewe, labda kama alitoa kwa vyuma huenda ikamletea shida.

Fuatisha wataalamu waliotangulia hapo juu walichosema.

Mwisho kabisa, huyo rafiki yake muite aende nae hospitali, usitake kujua mtoto anasumbuliwa na nini hasa, usije ukaumia zaidi moyoni.

Akienda hospitalin aonane na Dr peke yake aeleze shida zake, na amwambie Dr kuwa hapendi hii shida ijulikane, hapo mtoto atapona mapema.

Hii kusema mzazi afatilie tu kila hatua, hapo mkuu utampoteza mtoto, anaweza akachukua maamuzi magumu ili asitie aibu familia au alinde usalama wake.

Mtoto wa kike akishakuwa unapaswa utumie hekima sana kuishi nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kawaida mkuu mimi kuna binti namfahamu akiwa katika kipindi hicho cha MP huwa ni mtu wa kulazwa hospital kabisa ni full sindano za kutuliza maumivu.
 
Wasiwasi wako ni huo uvimbe uloambiwa?

Binti akifanya abortion ndani ya miezi isiyozidi miwili huwezi kumgundua, unless aseme mwenyewe, labda kama alitoa kwa vyuma huenda ikamletea shida.

Fuatisha wataalamu waliotangulia hapo juu walichosema.

Mwisho kabisa, huyo rafiki yake muite aende nae hospitali, usitake kujua mtoto anasumbuliwa na nini hasa, usije ukaumia zaidi moyoni.

Akienda hospitalin aonane na Dr peke yake aeleze shida zake, na amwambie Dr kuwa hapendi hii shida ijulikane, hapo mtoto atapona mapema.

Hii kusema mzazi afatilie tu kila hatua, hapo mkuu utampoteza mtoto, anaweza akachukua maamuzi magumu ili asitie aibu familia au alinde usalama wake.

Mtoto wa kike akishakuwa unapaswa utumie hekima sana kuishi nae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naam,

Ahsante kwa ushauri wako kaka. Maneno mazito hakika.

Lakini je, inawezekana kwamba alifanya kitendo hicho?
 
Back
Top Bottom