Naomba ufafanunuzi juu ya kisa cha tajiri na yesu(luka 18:18-27)

Kumbuka hata Abraham alipimwa Imani yake kwa kumtoa mtoto wa pekee, lkn alipoishinda Imani yake aliongezewa uzao pia,... Yesu anatufundisha siri ya mafanikio,. Si kwamba angeuza mali akaigawa angekuwa maskini, hapana, angeongezewa zaidi ya kile alichokiuza.. Sasa utaona alionyesha Imani yake pasi na matendo katika amri Ile ya mpende jirani yako kama nafsi yako..

Mathayo 19:29 Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
 
Ukisoma katika luka 18:18-27 kuna kisa cha kijana tajiri na yesu. Kijana anataka kuingia katika ufalme wa mungu na kazishika amri zote tangu utoto wake. Lakini yesu anamwambia ili aupate ufalme wa mungu basi auze mali zake zote na kuwagawia maskini kisha amfuate. Kijana anaondoka kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

maswali yangu,
je, matajiri hawataurithi ufalme wa mungu kwa sababu ya mali zao?

definition ya utajiri hapo ni ipi??
Kwa sababu kila mtu kuna kitu kamzidi mtu mwingine, je na mimi niuze nyumba,gari au hata hii simu niliyonayo ili nikamsaidie asiye na vitu hivyo ili niingie kwenye ufalme wa mungu??

mwishoni yesu aliposema kwa mwanadamu hayawezekani bali kwa mungu yanawezekana alikuwa na maana gani?,
Twende taratibu mleta mada, tunaposema neno iman unaelewa nini?
 
twende specifically katika mfano tajwa hapo juu.

Huyo tajiri alipungukiwa Jambo moja. Aliutamainia Utajiri wake kuwa ndio kila kitu. Kuwa bila huo hawezi kuishi.
Hivyo alifanya Utajiri huo Kama Mungu wake.
Na ndivyo matajiri wengi walivyo. Na hao ndio ujumbe huo unawahusu.

Lakini kasome kisa cha Ibrahimu au Ayubu uone tofauti yao na huyo Tajiri aliyekutana na Yesu.

Ayubu hata alipojaribiwa na kuchukuliwa Mali zote ili amkufuru Mungu lakini alikataa, hii ilimaanisha kwake Utajiri haukuwa namba moja Ila Mungu pekee.

Angalia na kisa cha Ibrahimu pia utaelewa,

Angalia na kisa cha Suleiman pia utaelewa kuwa wao Utajiri haukuwa namba moja isipokuwa Mungu pekee.
Suleiman alipoambiwa na Mungu aombe chochote, yeye akaomba hekima na maarifa kumbuka hekima na maarifa chanzo chake ni kumcha Bwana. Hivyo akachagua kumcha Bwana.
Soma
1 Wafalme 3:5
Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.

1 Wafalme 3:9
Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?

1 Wafalme 3:11
Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;
 
Binadamu tuna ishi kwenye dunia mbili ya kwanza Dunia ya Kimwili ya pili Dunia ya Kiroho.
Katika Dunia hizi Mbili Utajiri unatakiwa hili kuweza ishu na kutumikia Mungu na Jirani zetu.
Hapa kijana alikuwa anaambiwa kuuza mali zake zote zile za Kiroho kama vile majivuno, Uchoyo, Roho mbaya ili aweze mtumikia Mungu wake kikamilifu. Aingii akili kuwa auze Mifugo, Mashamba n.k ili aweze mtumikia Mungu wakati Mungu uwabariki watu wake kwa Utajiri wa mali mbalimbali zikiwemo Mifugo mashamba na mengineyo
Mmmmh! Ndugu sidhani Kama ni kweli maana kuna sehemu Bwana Yesu anazidi kupigilia msumari kuwa "Huwezi kuwatumikia mabwana wawili, MALI NA MUNGU" akasema chagua kimoja kingine ukiache. Najua kuna watu watawatolea mfano akina Suleiman lakini ukiangalia Akina Suleiman utajili wao hawakuutafuta bali Mungu aliwapatia Kama zawaidi, Suleiman alipouliza aombe chochote hakuomba Utajili aliomba shibe ya Roho. Zaidi hata ule Utajili aliopewa baadaye ikawa tanzu kwake kwenye kumtumikia Bwana baadaye akaona ni Ubatili mtupu.

Mwisho: Bwana Yesu anazidi kusema Ole wenu mnaocheka( mnaoenjoy maisha) sasa maana furaha yenu mmeishaimaliza. Haiwezekani utanue Duniani na Mbinguni Utanue uyo Mungu siyo Mjomba wako bwashee.
 
Kila mtu ana udhaifu wake kimwili unaomzonga ashindwe kufikia ukamilifu. Bwana Yesu alipomuangalia huyu ndugu(sababu aliona hadi moyo) akajua moyo wake upo kwenye mali(utajiri) na kwa asilimia zote hizo mali zitakwamisha juhudi za kuirithi mbingu.

Hivyo Bwana Yesu alipiga panapouma ili apone.
 
Huyo tajiri alipungukiwa Jambo ila kitu. Kuwa bila huo hawezi kuishi.
Hivyo alifanya Utajiri huo Kama Mungu wake.
Na ndivyo matajiri wengi walivyo. Na hao ndio ujumbe huo unawahusu.

Lakini kasome kisa cha Ibrahimu au Ayubu uone tofauti yao na huyo Tajiri aliyekutana na Yesu.

Ayubu hata alipojaribiwa na kuchukuliwa Mali zote ili amkufuru Mungu lakini alikataa, hii ilimaanisha kwake Utajiri haukuwa namba moja Ila Mungu pekee.

Angalia na kisa cha Ibrahimu pia utaelewa,

Angalia na kisa cha Suleiman pia utaelewa kuwa wao Utajiri haukuwa namba moja isipokuwa Mungu pekee.
Suleiman alipoambiwa na Mungu aombe chochote, yeye hanzo chake ni kumcha Bwana. Hivyo
Kama ni hivyo ni kwa nini wakristo leo wasiuze mali zao zote wamfuate yesu kama agizo la yesu lilivyomtaka yule tajiri ili kuonesha hawatumainii mali zao?
 
Binadamu tuna ishi kwenye dunia mbili ya kwanza Dunia ya Kimwili ya pili Dunia ya Kiroho.
Katika Dunia hizi Mbili Utajiri unatakiwa hili kuweza ishu na kutumikia Mungu na Jirani zetu.
Hapa kijana alikuwa anaambiwa kuuza mali zake zote zile za Kiroho kama vile majivuno, Uchoyo, Roho mbaya ili aweze mtumikia Mungu wake kikamilifu. Aingii akili kuwa auze Mifugo, Mashamba n.k ili aweze mtumikia Mungu wakati Mungu uwabariki watu wake kwa Utajiri wa mali mbalimbali zikiwemo Mifugo mashamba na mengineyo
😂😂😂😝😝😝😝huwezi kuwashinda hawa watu #wachungaji
 
Kuna maandiko mengi kwenye Bible, napenda hili
kumb 8:18"nawe utamkumbuka BWANA Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri ili kulitimiza agano lake alilowaahidi babu zenu "

Kama Mungu ndiye anayempa mtu nguvu za kupata utajiri, hawezi kuchukia utajiri. Anasisitiza kumkumbuka maana wengi husahau wakipata Mali nyingi
 
Watu wote Tajiri na masikini tutaingia peponi mungu ni mkuu wa rehema siku ya mwisho ataonesha ukuu wake kuwasamehe hata wale wouvu kabisa ...furahia maisha Wazee
 
Ukisoma katika luka 18:18-27 kuna kisa cha kijana tajiri na yesu. Kijana anataka kuingia katika ufalme wa mungu na kazishika amri zote tangu utoto wake. Lakini yesu anamwambia ili aupate ufalme wa mungu basi auze mali zake zote na kuwagawia maskini kisha amfuate. Kijana anaondoka kwa masikitiko kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

maswali yangu,
je, matajiri hawataurithi ufalme wa mungu kwa sababu ya mali zao?

definition ya utajiri hapo ni ipi??
Kwa sababu kila mtu kuna kitu kamzidi mtu mwingine, je na mimi niuze nyumba,gari au hata hii simu niliyonayo ili nikamsaidie asiye na vitu hivyo ili niingie kwenye ufalme wa mungu??

mwishoni yesu aliposema kwa mwanadamu hayawezekani bali kwa mungu yanawezekana alikuwa na maana gani?,

kwani ule mstari unaosema kama jicho lako linakukosesha au mkono au mguu ukate

na wewe utaenda kuchukua msumeno ukate mguu wako kweli??

sio kila kitu kinachonadikwa inabidi ukifanye hivo hivo. Hizo ni lugha za picha na mifano kusisitiza jambo fulani

hapo ujumbe ni kuwa fanya matendo mema kutoka moyoni hata kama itakugharimu utajiri wako

-------

kuhusu matajiri

chukua top 3 ya matajiri duniani
angalia kama wana time na Mungu

ukipata jibu sawazisha kwa pole pole
dunia hi ya Mola sio ya kwenda nayo kwa mapepe
mwisho wetu sote tunarudi kwa udongo!

-----

kuhusu lisilowezekana kwa wanadamu

chukua mfano wa Sauli kuwa Paulo ndio maana yake
 
Kuna maandiko mengi kwenye Bible, napenda hili
kumb 8:18"nawe utamkumbuka BWANA Mungu wako maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri ili kulitimiza agano lake alilowaahidi babu zenu "

Kama Mungu ndiye anayempa mtu nguvu za kupata utajiri, hawezi kuchukia utajiri. Anasisitiza kumkumbuka maana wengi husahau wakipata Mali nyingi
wapi wamesema kijana alimsahau mungu?? Zaidi ya yote kijana amekiri kuzifuata amri za mungu tangu utoto wake.
 
Ni kwa nini wakristo wa leo wasiuze mali zao zote wawape maskini kama yesu alivyomtaka yule tajiri??
Yesu kama kiongozi na Mungu mkuu alivyotoa ile amri alitumia nafsi ya 2 umoja. Sasa kwenye Bible ikitumika nafsi ya pili umoja hiyo amri sio general. Itawahusu wenye tatizo tu. Kwa wote ambao nafsi zao zinapenda pesa kuliko kumpenda Mungu ingawa midomo yao inamtaja Mungu mara kwa mara tena wengine na kupewa uongozi kanisani.
Hao wauze mali zao wabakishe za kuwatosha tu ndipo wamfuate Yesu.
Natamani ningekueleza deeply kisa kile . Kuandika Mimi ni mzito.
Rejea mstari wa 23. (Alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi).
Huo mstari ndio unaonyesha kuwa mali ndizo zilikuwa kipaumbele chake kuliko hata huo uzima wa milele aliokuwa akiuulizia.
Past. Ayubu
 
Back
Top Bottom