Naomba ufafanuzi kuhusu hili tatizo la maumivu ya kifua upande wa kulia

airwing

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
306
397
Natumaini ndg zangu Ni wazima, poleni na majukumu ya kikazi na familia.

Nina tatizo liloanza siku ya 3 leo nasumbuliwa na maumivu ya kifua upande wa kulia nasikia maumivu zaidi nikifuta hewa kwa nguvu au kukohoa hivi, hivi shida uminaweza kuwa ni nini?

Kazi yangu ni Udereva wa magari makubwa na muda mwingi huwa naendesha Gari je unaweza kuwa ni sababu?
 
pole mkuu.Hata mimi nilipitia hii changamoto kama wiki 2 zilizopita na kwa kipindi cha wiki 1nilipata haya maumivu,na hali hiyo ilikuwa inanitokea kuanzia mida ya jioni na mpaka usiku,mchana kutwa nakuwa vizuri.Maumivu yalianza upande wa kushoto wa kifua baada ya siku kadhaa yakahamia upande wa kulia.

Niliplan kwenda hosp ila kwanza nikaanza utaratibu wa kunywa maji mengi usiku hasa ninapoanza kuhisi maumivu.
Pili nilitengeneza mchanganyiko wa vitunguu,limao na tangawizi nikawa natumia kila wakati.

tatu,nilijifukiza asbh na jioni

nne,Nikawa napata glass ya maziwa fresh asbh.

Sijaju kama hizo tiba mbadala jilizotumia ndizo zilinisaidia au ni imani yangu tu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Piga tangawizi na limao ili uboost kinga ya mwili at least mara tatu kwa siku.

Nunua ped zinc kunywa kidonge 1 daily

Jifukize mchaichai,au muarubaini, au mkaratusi,au majani ya maembe na mapera, au viksi, au karafuuu na unga wa habat soda, n.k ( kile utakachopata).

Usinywe vitu vya baridi.
 
Sawa wadau kwa ushauri Ila nataka nifahamu shida Ni Nini Kuna. Madkatari humu!! Yaani huo upande maumivu yake yamepoa Kama siku mbili Ila Leo naona yamefufuka upya baada ya kulalia huo upande... Yaani naamka asbh panauma Sana hata ukinyoosha panauma Sana kwa ndani!!!
 
Natumaini ndg zangu Ni wazima, poleni na majukumu ya kikazi na familia.

Nina tatizo liloanza siku ya 3 leo nasumbuliwa na maumivu ya kifua upande wa kulia nasikia maumivu zaidi nikifuta hewa kwa nguvu au kukohoa hivi, hivi shida uminaweza kuwa ni nini?

Kazi yangu ni Udereva wa magari makubwa na muda mwingi huwa naendesha Gari je unaweza kuwa ni sababu?
Piga nyungu mkuu, tangawizi+limao+vitungu chemsha unaweza kuvi blend pia
 
Wakuu mnaosumbuliwa na hili Tatizo hebu jaribuni Kulala Kwenye Godoro tofauti na unalotumia tena Kwa njia rahisi zaidi unaweza hata kulala Kwenye carpet Kwa siku mbili au tatu ukiona Tatizo bado lipo then Hospital Kwa check up zaidi Kama walivyoshauri watalaamu.
 
Natumaini ndg zangu Ni wazima, poleni na majukumu ya kikazi na familia.

Nina tatizo liloanza siku ya 3 leo nasumbuliwa na maumivu ya kifua upande wa kulia nasikia maumivu zaidi nikifuta hewa kwa nguvu au kukohoa hivi, hivi shida uminaweza kuwa ni nini?

Kazi yangu ni Udereva wa magari makubwa na muda mwingi huwa naendesha Gari je unaweza kuwa ni sababu?
Habari ndugu.
Kwa jinsi ulivyoeleza, mambo matatu yaweza kuwa ni shida.

1: Inaweza kuhusisha maambukizi kwenye mapafu. Chochote chaweza kuwa ni chanzo kati ya bakteria, virusi au fungus.

2: Maambukizi kwenye ngozi inayozunguka mapafu (pleurisy).
Hii huweza kusababishwa na bacteria, fungus, virus, baridi au wakati mwingine hautaweza kujua hali imeanzia wapi.

2: Inawezakuwa ni shida ya mbavu, kutokana na aina ya kazi unayofanya. Au kuna kitu ulifanya/nyanyua lakini hukupata maumivu palpale.

3: Inawezakuwa shida ya misuli kama namba 2 hapo juu.

Bado kunahitajika kuulizwa maswali zaidi na kufanyiwa physical examination na daktari ataona kama kuna haja ya vipimo au la baada ya hapo akuandikie dawa kulingana na maoni ya mwisho.
Hivyo, ni mhimu kumwona daktari.
 
pole mkuu.Hata mimi nilipitia hii changamoto kama wiki 2 zilizopita na kwa kipindi cha wiki 1nilipata haya maumivu,na hali hiyo ilikuwa inanitokea kuanzia mida ya jioni na mpaka usiku,mchana kutwa nakuwa vizuri.Maumivu yalianza upande wa kushoto wa kifua baada ya siku kadhaa yakahamia upande wa kulia.

Niliplan kwenda hosp ila kwanza nikaanza utaratibu wa kunywa maji mengi usiku hasa ninapoanza kuhisi maumivu.
Pili nilitengeneza mchanganyiko wa vitunguu,limao na tangawizi nikawa natumia kila wakati.

tatu,nilijifukiza asbh na jioni

nne,Nikawa napata glass ya maziwa fresh asbh.

Sijaju kama hizo tiba mbadala jilizotumia ndizo zilinisaidia au ni imani yangu tu.

Hili tatizo limenipata 3weeks ago!

Pia Kuna jirani angu nikawa namsimulia, nae kumbe akawa anaumwa the same prob

Mm nilitumia maji na mchanganyo wa kitunguu saumu, limao, ginger na majani ya nyonyo! Unatwanga then unachemsha kwa pamoja! Siku mbili tu nipo fit nafanya kazi ngumu!
 
Back
Top Bottom