Naomba tushauri hawa graduates wa postgraduate diploma wamekata tamaa

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,191
7,319
Habari wadau?

Kuna rafiki zangu wawili naomba msaada wa ushauri.

Walimaliza chuo 2010 mmoja PSPA UDSM, na mwingine alisoma BCOM UDOM.

Hawakubahatika kupata ajira kwa muda mrefu ambapo mwaka juzi waliamua kwenda kufanya postgraduate diploma ya education pale UDSM kwa ajili ya kupangiwa ajira za moja kwa moja za serikali wakimaliza.

Waliamua kusoma postgraduate ya education sababu waliamini ajira za walimu zipo kila mwaka na graduates wengi wa course tofauti tofauti na wengi sana wamepata kazi ya ualimu kwa mfumo huu miaka ya nyuma.

Wakatumia zaidi ya milion 7 kujisomesha hii ni ada na other cost.

Bahati mbaya baada ya kumaliza serikali mpya nayo imebadili utaratibu wa kuajiri walimu na wametangaza kabisa postgraduate diploma hawatakiwi na walimu ni wa science tu.

Jamaa zangu ni kama wamedata, mmoja amekata tamaa sana na sana.

Naomba tuwashauri hawa vijana wetu
 
Huyo kama aliweza kumudu gharama ya milion 7 basi kupata mtaji wa kufanyia biashara au kilimo kwake haitakua shida!

Ajipange upya ajiari tu kilimo kitamlipa zaidi
Unapataje 7m+ ukiwa huna ajira alafu unaishi kulalamika? Huyo wa Bcom elimu yake haikumsaidia kabisa kwani angeweza kujiajiri, huyo wa political science angeenda kugombea ubunge bush kwao au udiwani mjini
 
Hao wana ilikua n kuwashauri kabla hawajaenda kusoma hzo fani za elimu hawajachelewa haina haja ya kudata ety kisa umekosa laki tano cjuh za silikali kwa mwezi......... Waangalie around kuna oppotyunitiz kibao wanaweza kutumia wakiwa na malengo na bado maisha yakasonga
 
Unapataje 7m+ ukiwa huna ajira alafu unaishi kulalamika? Huyo wa Bcom elimu yake haikumsaidia kabisa kwani angeweza kujiajiri, huyo wa political science angeenda kugombea ubunge bush kwao au udiwani mjini
Yaani watu wanashangaza sana na elimu zao!
any way mpe ushauri akalime tu
 
Hizo ni raana mshambiwa mwalimu achekwi wala wala kudharauliwa kipindi mpo masomo nyie mkifanya kozi tofauti na uwalimu huwa mnawadharau sana walimu mnawacheka mnawadhihaki kuwa wataenda vijijini, wataenda kulipwa Mishahara ya kununulia ice cream super market nk yani kiujumla nikiona mtu ambaye hakusoma kozi ya uwalimu anaenda kwenye uwalimu na analalamika ajira Sijui nini nakereka acha wewe mwanzoni ulikuwa wapi wenzako wanaanzaga hesabu za kujumlisha kisha wanaenda za kutoa nyie mlianza za kutoa mkaja jumlisha haaaaa haaaa go to hell
 
Bro naomba msaada wako nina ml 6 nipo dom nifanye biz ipi niweze kufanikiwa
Fanya biashara ya Dodoma Granite, faida ni 100%, jikite sasa kwani biashara hii bado inaukiritimba sana.., hakuna namna ya kukinganisha bei.., hivyo bei unapanga wewe kama Tanesco
 
Back
Top Bottom