GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,468
- 108,621
Nimeambiwa kuwa kuna Mbinu mbalimbali ila najua hapa Jamvini JamiiForums wapo Watu ambao enzi zao nao ' Walibobea ' ama katika Kuita Ndugu zake wakati wa Kula au Kuitwa Yeye na Mwanafamilia ili akale Chakula. Binafsi huwa nakaa sana Vijiweni hivyo Mwanafamilia wangu huwa akija Kunitaarifu kuwa Chakula kipo tayari huwa anaropoka tu kwanguvu kiasi kwamba huwa najikuta naona Aibu na nawakaribisha Wenzangu Kijiweni ambapo nao huwa hawajui kuwa Kukaribishwa ni Uungwana tu na ukienda kweli Kula ni Ulafi hivyo nao huamka na kwenda Kula nami hivyo najikuta sijashiba au sishibi kabisa.
Leo nataka mbinu ambazo nitakuwa nampa huyu Mwanafamilia wangu ili akiwa anakuja Kunitaarifu pale Kijiweni kuwa Chakula tayari na nikale basi asiwe anasema kwa Nguvu hadi Watu wanasikia na Kung'ang'ania kwenda Kula nami. Ni Ishara gani labda anatakiwa awe ananifanyia ambazo nitakuwa nazijua Mimi na Yeye tu?
Nawasilisha.