Naomba tupeane mbinu za Kuimuita Mwanafamilia wako aliyeko Kijiweni kuwa Chakula tayari pasipo aje Kula na wale wengine wasijue

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,363
108,402
Nimeambiwa kuwa kuna Mbinu mbalimbali ila najua hapa Jamvini JamiiForums wapo Watu ambao enzi zao nao ' Walibobea ' ama katika Kuita Ndugu zake wakati wa Kula au Kuitwa Yeye na Mwanafamilia ili akale Chakula. Binafsi huwa nakaa sana Vijiweni hivyo Mwanafamilia wangu huwa akija Kunitaarifu kuwa Chakula kipo tayari huwa anaropoka tu kwanguvu kiasi kwamba huwa najikuta naona Aibu na nawakaribisha Wenzangu Kijiweni ambapo nao huwa hawajui kuwa Kukaribishwa ni Uungwana tu na ukienda kweli Kula ni Ulafi hivyo nao huamka na kwenda Kula nami hivyo najikuta sijashiba au sishibi kabisa.

Leo nataka mbinu ambazo nitakuwa nampa huyu Mwanafamilia wangu ili akiwa anakuja Kunitaarifu pale Kijiweni kuwa Chakula tayari na nikale basi asiwe anasema kwa Nguvu hadi Watu wanasikia na Kung'ang'ania kwenda Kula nami. Ni Ishara gani labda anatakiwa awe ananifanyia ambazo nitakuwa nazijua Mimi na Yeye tu?

Nawasilisha.
 
Mwanaume anayetafuta pesa ni mwiko kuwa mchoyo kwa vitu kama vinywaji na chakula kutokana na pesa anazotafuta ni za kula na kufanya mambo mengine ya msingi.

Hizo technique waachie dada zako wajifunze zaidi namna ya kunyimana lipstick madera etc.
 
Kuna Watu hapa Jamivini JamiiForums huwa mnanifanya nivunjike mno mbavu zangu kwa Kucheka. Nimecheka sana na mno Mkuu.
Kweli mkuu.. Kama ugali unasema tu Oii bakari unaitwa tukale... kama wali unamwambia Oii Bakarii mama anakuita... Kama wali Kuku unamwambia Bakari Shauri yakoo mbiooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom