Rufaro
JF-Expert Member
- May 7, 2022
- 222
- 340
Nashukuru kwa makaribisho mazuri.!
Naomba moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Naamini asilimia kubwa pengine tupo katika biashara either iwe kubwa au wastani au ndogo. Sasa najua wengi wetu tumekuwa tunasikia baadhi ya wafanyabiashara wanakuambia kuwa mfano alianza na pea moja ya viatu na sasa ana kiwanda cha viatu, mwingine anakuambia nilianza na kubrash viatu (shoeshine) na sasa anamiliki makampuni ya kuuza juisi au mabasi. Hili jambo limekuwa linanipa ukakasi sana.
Basi naomba leo tujadiliane kwa pamoja kuhusu hili na pia tuanze na mfano hai na naamini kupitia maandishi haya wengine pia wataweza kuokota chochote kitu kitakachowasaidia nao pia katika safari yao kibiashara. Ni ndoto za kila mfanyabiashara haswa ndogondogo kwamba anachofanya kitakuwa kikubwa na sio kuishia chini.
Mfano hai wangu ni huu, je nitawezaje kuifanya biashara ya real estate yenye nyumba moja tu ya kupangisha ya familia yenye kuingiza Tsh. 450,000/- kwa miezi mitatu, kuifanya kuwa biashara kubwa ambayo ntakuwa namiliki nyumba za kukodisha(renting) za kukaa na apartments pia na majengo mengi ya kukodisha kama frem za kufanyia biashara? Karibuni tushirikiane kwa pamoja, najua kwenye jumuiya hii ya JamiiForums kuna wafanya biashara wakubwa na wazoefu, na washauri wazuri na hata wanaofanya hii real estate.
Thread hii itakuwa muendelezo....
Asanteni