Naomba tumsaidie Joyce Kiria wa wanawake live. Anabomoa msingi wa taifa Bora

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Nasoma posti zake kupitia wanawake live fb. Anaposti kila uchwao story za wanawake wanasemekana kuteswa katika ndoa zao na kuamua kuachika kabisa.

Pamoja na kubainisha malengo yake ni kupigania haki za wanawake, kuwainua kiuchumi nakuwatetea Ila anachofanya Sasa kinaonekana wazi NI kujenga uadui Kati ya wanawake na waume zao.

Najua aliyopitia na huenda hayuko sawa kisaikolojia kuhusu ndoa. Akiwa na ushawishi wake anaenda kubomoa taifa. Mi namshauri Leo Tena humu JF.

Sawa sikatai pigania haki za akinadada wasinyanyasike. Lakini kwanini mwisho wa siku uhitimishe na kuachana?!! Huwezi pinga ukatili bila kuhimiza kuvunja ndoa za watu? Kila ndoa inachangamoto zake na inasemekana kiutafiti Hadi 40% ya wanaume hunyanyaswa kwenye ndoa zao na wanawake Ila hawasemi, huona aibu.

Unachokifanya ni utume wa shetani. Taifa ovu hutokana na familia mbovu au ukosefu wa familià.

Dadaangu omba Mungu akujalie upendo. Himiza upendo katika familia ili kupinga ukatili. Toa mifano ya familia Takatifu zinavyoishi kwa upendo na walivyoweza kuepuka manyanyaso na wanavyotafua changamoto zao.

Mungu alimpa Mariam Mama yake Yesu mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Lkn baada ya hapo akampa Mume wa kumsaidia kulea Mimba na mtoto. Kama mimba iliwezekana patikana bila Mume lkn Malezi bora bila familia Mungu hakuruhusu itokee kabisa. Yeyote apingae ndoa NI nabii wa shetani.

Tuko pamoja kupinga ukatili wa wanawake kwa njia Yoyote Ile lakini sio kuhimiza kuvunja ndoa za watu.
 
Nimeshauri tupinge manyanyaso bila kuhimiza usingle mama. Soma posti upya
Tuambie wewe njia za kuzuia manyanyaso.....unasema ahubiri upendo wewe hujui kuwa unatakiwa kumpenda mkeo? Mlipokuwa mnafunga ndoa wimbo mkuu kwenye siku hiyo ulikuwa ni upendo mchungaji, waimbaji, wazazi marafiki na wote waliohushuria harusi yako walikuwa wanaimba neno upendo...kama yote yale hayakukuingia ndio yatakuingia leo ukiambiwa na Joyce Kiria?

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Tuambie wewe njia za kuzuia manyanyaso.....unasema ahubiri upendo wewe hujui kuwa unatakiwa kumpenda mkeo? Mlipokuwa mnafunga ndoa wimbo mkuu kwenye siku hiyo ulikuwa ni upendo mchungaji, waimbaji, wazazi marafiki na wote waliohushuria harusi yako walikuwa wanaimba neno upendo...kama yote yale hayakukuingia ndio yatakuingia leo ukiambiwa na Joyce Kiria?

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Kibiblia hakuna Cha kututenganisha. Kila tukio la kutoelewana na ugonvi Lina sababu zake. Na mwisho wa kuamua kuachana na ndoa abaki kuwa mwanandoa mwenyewe bila kushauriwa na mtu. Nachopinga anapostiwa kisa tu, hazungumzi na aliyempostia kiundani, hamtafuti mlalamikiwa anakuja na swala la kuachana.

Lazma ujue kilakitu kinachangamoto zake. Biblia inasema makwazo yapo tu. Na tutavikwa taji tukiweza kuyashinda. Lazma tuwe chombo Cha Amani. Tuoneshe msamaha kwa wale wanaotukosea na kuwapatanisha wale wenye kugombana.

Dunia nzima ushauri nasaha NI Muhimu Sana. Bora aanzishe kampuni ya ushauri nasaha ili asaidie kupatanisha ugonvi na kujenga familia Bora sio kutetea u single Mother.
 
Kibiblia hakuna Cha kututenganisha. Kila tukio la kutoelewana na ugonvi Lina sababu zake. Na mwisho wa kuamua kuachana na ndoa abaki kuwa mwanandoa mwenyewe bila kushauriwa na mtu...
Mkuu thamani ya ndoa anaijua mwanandoa mwenyewe na uchungu wa ndoa anaujua mwenyewe.... Sidhani kama kuna mwanandoa anaweza kuvunja ndoa kisa Joyce Kiria kasema, ni kwamba hata yeye anakuwa amefika mwisho wa uvumilivu.

Kama vile ambavyo hawezi kukujengea nyumba yako vivyo hivyo hawezi kukuvunjia....yeye ni mtoa maoni tu kama mimi ninavyotoa hapa

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Nasoma posti zake kupitia wanawake live fb. Anaposti kila uchwao story za wanawake wanasemekana kuteswa ktk ndoa zao na kuamua kuachika kabisa. Pamoja na kubainisha malengo yake NI kupigania haki za wanawake, kuwainua kiuchumi nakuwatetea Ila anachofanya Sasa kinaonekana wazi NI kujenga uadui Kati ya wanawake na waume zao...
We jomba nimekuelewa Sana..na kwa kweli Sasa amepotea njia..nadhani ameachika na ndoa yake lakini asidhani kila ndoa itakuwa Kama yake, lakini umempa mifano asilimia 40 ya wanaume wananyanyasika na ndoa zao..lakini wapo kimya wanatafuta njia mbadala was kutafuta ufumbuzi lakini bila kutaka kuvunja ndoa..superb..nimeipenda hii.

Kwa hiyo huyo mama asivutuge Mama zetu dada zetu na watoto wetu..akome kuwashawishi wanawake waone Kama vile ndoa Ni jehanamu..nooooo...ipo kwenye vitabu vya Mungu vyote na Ni amri ya Mungu..asilete ushetani katika familia zetu
 
Sijawahi kuona joyce kiria akishawishi watu waache ndoa zao .. huwa analeta matukio yalitokea yanayotokea kwenye ndoa ambayo mengine yamesababisha maafaa kama vifo na ulemavu na asilimia kubwa ya matukio hayo yamesababishwa na wanandoa hasa wanawake kuvumilia kwa muda mrefu manyanyaso na vipigo .
 
Mbona Muzungu anakupigania wewe Mwanaume wa Kiafrika? Kwa nini Mwanaume mzima unakwenda kushitaki kwa Mwanaume mwenzio? Hakuna tofauti, huyo Mama anapigania haki za Mwanamke kama vile Muzungu anvyoopigania haki za nigga na ,,black life matters“, ...
 
Tatizo Mamlaka zinazo toa na kuratibu huduma za familia hapa nchini zimelala. Kutoa Ushauri masuala ya Familia Ni Professional, tena nyeti, sio kila mTu anaweza akaamka tu kesho akaanza kufundishaa masuala ya Jamii. Ni Upotoshsji Mkubwa ,Ilitakiwa Vipindi vinavyohusu masuala ya Familia yawe yanaririwa na Waendeshaji wake wawe na Taaluma hiyo!
@KAMISHNAwa Ustawi wa Jamii!🥺
 
Msingi wenyewe ndo huu acha aubomoe tu
122129069_347445626320333_6139800271667525604_n.jpg
 
Huyo dada bora na wewe umemuona

Watu wa dizaini hiyo wamelelewa na ma single mother tena wale maselaa kweli kweli

Yawezekana tabia hyo kairithi kwa mamaake na ndio maana dingi yake akachapa lapa mapemaaaa

Mungu anataka familia ziungane wewe unatumia ushawishi wako kisa ulikua hausigeli unataaka familia zisambaratike
 
Mkuu, kuna jambo la msingi ktk hoja yako.

Masuala ya migogoro, ni muhimu kusikiliza na upande wa mlalamikiwa na kwa lengo la kutafuta suluhu/muafaka kwa manufaa ya wote.

Huyo mdada hatengi wasaa wa kusikiliza upande wa pili. Kitendo cha kuruka hewani akiwa na 'biased conclusion' ni hatari kwa jamii.

RAI, kwa yeyote aliye karibu nae, amfikishie huu ujumbe.
 
Mnaohangaika na wanawake wanaharakati mna shida

Kama wanawake wanaona suluhu ni kuachana wacha wazivunje ndoa ila asili inaonyesha ndoa sio tatizo kwa mwanaume
Mwanaume anaweza kupata mwenzi hata akiwa na 70 yrs ila uwanda wa kujiachia wa mwanamke ni finyu sana

Unaendekeza kuachana wakati nafasi/muda wa kuwa sokoni ni mdogo hicho ni kichaa
 
Back
Top Bottom