Naomba tujuzane namna ya uandaaji wa kinywaji cha "al-kasusu"

Sambwisi

Senior Member
Nov 12, 2010
175
67
Nikiwa Tanga mwaka jana nilisikia kuhusu kinywaji kiitwacho Al-Kasusu. Nilinunua na kunywa kinywaji hicho na kukuta ni kweli kinachangamsha. Nilijaribu kuulizia kinavyotengezwa nikaambiwa na wale wanouza kuwa wananunua unga wake (Al-kasusu) ambao wanapika na maziwa na kuunga kwa asali; wakanieleza sehemu unapouzwa huo unga kwa pale Tanga mjini ni jirani na soko la Nganiani.

Nilienda pale unapouzwa na kukuta umefungwa katika pakiti za robo kilo. Nilimhoji muuzaji akanieleza matumizi yake na kwamba ni mchanganyiko wa viungo (spices) tu lakini naye hajui ni mchanganyiko wa vitu gani na kwa viwango gani.

Kwa jinsi unga wake unavyonukia na kinywaji chake kinavyoburudisha ningelipenda mwenye kufahamu kuhusu mchanganyiko wake(ingredients) na viwango vyake (ratios) atujuze zaidi.

Karibuni.
 
Nachojua unachukua unga wake unaweka kwenye maziwa,unaweka Habbat Soda(hii muhimu) unachemsha kama upikavyo chai. Unaweza kuweka asali.

Kama huna huo unga we chukua viungo vya chai kama vitano changanya, weka habbat soda chemsha. Kuna rafiki yangu imemponesha bawasiri na vidonda vya tumbo.
 
Back
Top Bottom