Naomba tujadili utawala wa Magufuli tukiweka kando itikadi zetu za kisiasa

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
3,330
Mimi sio mwanachama wa chama chochote ila naipenda CHADEMA. Uchaguzi uliopita niliimpigia kura Tundu Lissu na uchaguzi wa 2015 nilimpigia kura Lowassa.

Binafsi naamini kwenye utendaji na uchapa kazi Magufuli anawazidi wakina Lowassa na Lissu. Anayoyafanya Magufuli nina uhakika Lowassa na Lissu hawawezi kuyafanya.

Kwa huu uchapakazi wa Magufuli (na kama factors zingine ambazo nitaziongelea hivi punde angejiepusha nazo) haki ya Mungu Tanzania ingekuwa kama Malasyia au South Korea au kama nchi zingine zilizoendelea kwa kasi ya ajabu.

Watu mnaweza kujiuliza "kwa nini nimekuwa nikichagua upinzani kwenye kila uchaguzi?" Jibu langu ni fupi tu. Siipendi ccm toka moyoni. Umaskini wote tulionao watanzania umesababishwa na CCM.

Mimi nimezaliwa kijijini na miaka yangu ya utotoni nimeishi kijijini kabla sijapata ufahamu nakuamua kukimbilia mjini hatimae kufanikiwa kuondoka Tanzania.

Vijijini kuna ufukara wa kutisha. Kuna familia ni kama zimetengwa na jamii kwa sababu ya ufukara. Kuna jamii za Kitanzania, amini usiamini bado zinaishi kama wanyama.

Hazina ustaarabu na uelewa kuwa binadamu wote ni sawa. Kila binadamu ana mwili wa nyama hivyo maumivu ya kumtendea mwenzako uovu ni sawa na yale wewe ungeumia kama ungetendewa.

Nimeshuhudia mara nyingi sungusungu wakiua mtu kwa fimbo kisa kaiba ngo'mbe. Huu ni mfano mmoja wapo kuwa kuna jamii bado hazijastaarabika na zinaishi kama wanyama.

Mfano mwingine kuna familia vijijini ni fukara kabisa, sijui nielezaje ili nieleweke. Kuna familia fukara ambazo watoto ni kama vile watoto wamejizaa. Utotoni mwangu nimechunga ng'ombe.

Huko machungani kuna familia unaweza ukamkuta mtoto wa kike mwenye miaka 7 anakaa na bibi yake asiyejiweza, wanakaa kwenye nyumba ya nyasi iliyoraruka isiyo na matumaini yoyote ya uhai wa mtu.

Familia inashindia mlenda na ugali wa mtama. Haina chochote hata kuku. Haya matatizo yote nikiyafikiria naona yamesababishwa na CCM.

Wakuu wa wilaya walikuwa wanakuja vijijini wakiwa na matumbo makubwa na vipara wakiendeshwa kwenye magari ya kifahali wakati jamii inaishi kwenye ufukara uliotopea. Hii ndio sababu kwa nini siipendi CCM.

Turudi kwa Magufuli. Magufuli ni mchapa kazi, tena sana. Kama ni Rais huyu ndio rais watanzania tulikuwa tunamhitaji. Kwa huu utendaji wake, angejiepusha na kasoro ya kukandamiza demokrasia angeifikisha nchi mbali sana.

Kinachomharibia Rais wetu ni chuki dhidi ya wapinzani. Laiti angefanya huu uchapakazi bila kukandamiza wapinzani, na kutoa uhuru kwa vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserikali, haki ya Mungu Tanzania ingekuwa level nyingine.

Magufuli kwa huu utendaji wake hakuna mpinzani angemshinda kwenye sanduku la kura kama asingekandamiza demokrasia. Binafsi hata mimi japo mara zote nimekuwa nikiwapigia kura wapinzani lakini nilikuwa natamani ashinde. Simpigii kura lakini natamani ashinde. CCM ndio siipendi ila Magufuli nampenda.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Magufuli laiti angeachana na mambo ya kukimbizana na wapinzani, akaweka mahusiano mazuri na jumuia za kimataifa hakika Tanzania ingekuwa level nyingine.

Demokrasia ingemsaidia sana kwenye uchapakazi wake. Jumuiya za kimataifa zingemuunga mkono hivyo jitihada zake zingekuwa na back up kutoka sehemu nyingi tofauti na sasa anapambana peke yake.

Naomba kuwasilisha.
 
Hapa ndio huwa nashindwa kuwaelewa wapinzani.

Unasema Magufuli ni mchapa kazi na kasoro yake ni moja tu kuwakandamiza wapinzani.

Wakati huo hizo kazi unazosema amechapa, mgombea wako alizipinga zote akisema ni maendeleo ya vitu huku nyie washabiki wake mkishangilia.

Kwa mujibu wa chadema unayoishabikia, yote aliyofanya Magu wanasema ni bure kabisa hayana maana yoyote kwa mtanzania na amefanya ili kukifurahisha mwenyewe tu.
Ndio maana kwenye uchaguzi mkapigwa chini sababu hamueleweki mnataka nini.
 
Binafsi naamini kwenye utendaji na uchapa kazi Magufuli anawazidi wakina Lowassa na Lissu. Anayoyafanya Magufuli nina uhakika Lowassa na Lissu hawawezi kuyafanya.
Niongeze na mimi kwenye orodha ya hao uliowataja! Hata mimi pia siwezi kuyafanya hayo anayofanya kwa kiwango hicho anachofanya yeye, labda ashuke na malaika kutoka mbinguni akiwa kwenye umbile la binadamu, awe pamoja nami kama msaada wangu wa nyongeza
 
SIJAWAHI KUWAELEWA WAPINZANI WA KISIASA WA TAIFA HILI. WENGI WANAJIKANYAGA TU.NOTHING MORE
 
Magufuli ni muumini wa maendeleo ya vitu, watanzania wanataka maendeleo ya watu ambayo unayajenga within wao... Elimu bora, Afya bora, Uhuru wa fikra !!
 
Mimi sio mwanachama wa chama chochote ila naipenda CHADEMA. Uchaguzi uliopita niliimpigia kura Tundu Lissu na uchaguzi wa 2015 nilimpigia kura Lowassa.

Binafsi naamini kwenye utendaji na uchapa kazi Magufuli anawazidi wakina Lowassa na Lissu. Anayoyafanya Magufuli nina uhakika Lowassa na Lissu hawawezi kuyafanya.

Kwa huu uchapakazi wa Magufuli (na kama factors zingine ambazo nitaziongelea hivi punde angejiepusha nazo) haki ya Mungu Tanzania ingekuwa kama Malasyia au South Korea au kama nchi zingine zilizoendelea kwa kasi ya ajabu.

Watu mnaweza kujiuliza "kwa nini nimekuwa nikichagua upinzani kwenye kila uchaguzi?" Jibu langu ni fupi tu. Siipendi ccm toka moyoni. Umaskini wote tulionao watanzania umesababishwa na CCM.

Mimi nimezaliwa kijijini na miaka yangu ya utotoni nimeishi kijijini kabla sijapata ufahamu nakuamua kukimbilia mjini hatimae kufanikiwa kuondoka Tanzania.

Vijijini kuna ufukara wa kutisha. Kuna familia ni kama zimetengwa na jamii kwa sababu ya ufukara. Kuna jamii za Kitanzania, amini usiamini bado zinaishi kama wanyama.

Hazina ustaarabu na uelewa kuwa binadamu wote ni sawa. Kila binadamu ana mwili wa nyama hivyo maumivu ya kumtendea mwenzako uovu ni sawa na yale wewe ungeumia kama ungetendewa.

Nimeshuhudia mara nyingi sungusungu wakiua mtu kwa fimbo kisa kaiba ngo'mbe. Huu ni mfano mmoja wapo kuwa kuna jamii bado hazijastaarabika na zinaishi kama wanyama.

Mfano mwingine kuna familia vijijini ni fukara kabisa, sijui nielezaje ili nieleweke. Kuna familia fukara ambazo watoto ni kama vile watoto wamejizaa. Utotoni mwangu nimechunga ng'ombe.

Huko machungani kuna familia unaweza ukamkuta mtoto wa kike mwenye miaka 7 anakaa na bibi yake asiyejiweza, wanakaa kwenye nyumba ya nyasi iliyoraruka isiyo na matumaini yoyote ya uhai wa mtu.

Familia inashindia mlenda na ugali wa mtama. Haina chochote hata kuku. Haya matatizo yote nikiyafikiria naona yamesababishwa na CCM.

Wakuu wa wilaya walikuwa wanakuja vijijini wakiwa na matumbo makubwa na vipara wakiendeshwa kwenye magari ya kifahali wakati jamii inaishi kwenye ufukara uliotopea. Hii ndio sababu kwa nini siipendi CCM.

Turudi kwa Magufuli. Magufuli ni mchapa kazi, tena sana. Kama ni Rais huyu ndio rais watanzania tulikuwa tunamhitaji. Kwa huu utendaji wake, angejiepusha na kasoro ya kukandamiza demokrasia angeifikisha nchi mbali sana.

Kinachomharibia Rais wetu ni chuki dhidi ya wapinzani. Laiti angefanya huu uchapakazi bila kukandamiza wapinzani, na kutoa uhuru kwa vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserikali, haki ya Mungu Tanzania ingekuwa level nyingine.

Magufuli kwa huu utendaji wake hakuna mpinzani angemshinda kwenye sanduku la kura kama asingekandamiza demokrasia. Binafsi hata mimi japo mara zote nimekuwa nikiwapigia kura wapinzani lakini nilikuwa natamani ashinde. Simpigii kura lakini natamani ashinde. CCM ndio siipendi ila Magufuli nampenda.

Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba Magufuli laiti angeachana na mambo ya kukimbizana na wapinzani, akaweka mahusiano mazuri na jumuia za kimataifa hakika Tanzania ingekuwa level nyingine.

Demokrasia ingemsaidia sana kwenye uchapakazi wake. Jumuiya za kimataifa zingemuunga mkono hivyo jitihada zake zingekuwa na back up kutoka sehemu nyingi tofauti na sasa anapambana peke yake.

Naomba kuwasilisha.
Mauaji ya Raia wasio na hatia

Kuteka watu na kuwapoteza

Kula nyama za watu

Kuua na kutupa baharini Maiti za raia wasio na hatia nk...

Kweli Haya mambo si Lissu wala Lowassa wanaweza kuyafanya maana ni wacha Mungu
 
Ulivyotaka tu kuifananisha Tanzania na South Korea hapo hapo ndio nimekuupuza na sijaendelea zaidi kusoma huu ugoro wako.

Hao Nigeria tu hawasubutu kutaka kujifananisha na South Korea.

Yani watu watengeze Samsung na bado wawe na watu maboya kama wagogo?
 
Mkuu umeongea kweli tupu
 
Back
Top Bottom