Naomba tujadili kidogo juu ya huduma za afya Hospitali Binafsi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Inapofika mahali ukachunguza unaporekebishiwa uhai huna budi kuchunguza ukiwa umefunga mdomo,milango na madirisha.

Hospital ya Aga Khan ni moja ya hospitali zinazopokea wagonjwa wengi kwa sasa ni hospital ya private. Nadhani inaweza isiwe na vifaa vizuri Kama mloganzila ila inaweza ikawa na usimamizi na huduma nzuri kuliko Mloganzila.

Hospital nyingi za serikali hazina huduma na watoa huduma wamekatishwa tamaa. Hawana Uhuru wa kuhoji wala Uhuru wakutoa huduma kwa kuzingatia taaluma zao Bali wanatoa huduma kulingana na mfumo wa siasa unavyotaka.

Niwaombe serikali katika kipindi hiki kigumu tunachopitia msitumie nguvu kupambana na hospitali za private zungumzeni nao. Hadi Sasa Waziri wa afya na timu yake hawapaswi kuendelea kuwepo na kuruhusu dola kuingilia kazi za utoaji wa afya. Mtawafanya wagonjwa waliopo ICU kwa kushindwa kupumua wapoteze maisha kwa sababu badala madaktari wawe busy kutoa huduma mnakwenda kuwaweka busy kwenye mahojiano.

TUACHE siasa kwenye afya tutapoteza wapendwa wetu. Kama ni gharama tujiulize wanaotibiwa nje akiwemo mmoja wa Mawaziri wetu, akiwemo spika na wengine walilipa kiasi gani kutoka kwenye Kodi za wananchi?

Watu wanakwenda hospitali binafsi kwa sababu serikalini Hali ya huduma si nzuri. Tusilazimishe hospitali binafsi zitoe huduma ya chini bali tujadiliane nao kuhusu gharama na namna nzuri ya kupunguza gharama hizo.

Polisi kwenye afya atakwenda kuzalisha mgomo baridi na ndugu zao kama siyo ndugu zetu watapoteza maisha pasipo na ulazima.
 
150045524_4095638310454408_7175310047829840858_n.jpg
 
Wasimchezee Agakhani yule ni beberu mkubwa hii vita tutashindwa kama alivyoshindwa Meko kwenye Sukari na Korosho
 
Back
Top Bottom