Naomba tufahamishe njia mnazotumia kutuma mizigo kutoka China kuja hapa Tanzania

Dreams Mastermind

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
403
500
Kuna mambo mawili hapa,
1.Mzigo unaununua mwenyewe kwa njia unazo zijua,ila unataka kuusafirisha kwenda Tanzania.
Hapa ni unawatumia wauzaji address ya wasafirishaji ambao watatumiwa mzigo wako na kukusafirishia.Kuna kusafirisha kwa meli (siku 30+).Hapa kuna kampuni nyingi zinafanya kama Sikent Ocean,GNM cargo,Mapembelo cargo, etc.Hawa wana kucharge kutokana na size ya mzigo (CBM)
Pia unaweza safirisha kwa ndege (wengi siku 7) Wata kuchaji kwa uzito wa mzigo wako.Na kuna mizigo mingine ambayo bei zake haziko determine kutokana na uzito.Mfano simu/laptop etc.Kuna kampuni nyingi tu zinasafirisha kwa njia hii.
2.Unataka kujua mtu/kampuni inayoweza kukununulia na kukusafirishia kwenda Tanzania.
Hapa wasiliana na watu au kampuni either zinazo safirisha mizigo wakununulie au watu/kampuni wanaosaidia kununua mizigo China.Watakufanyia hivo na watakutumia kulingana na njia uliyo amua kuitumia kama ni ndege au meli.
Maelezo yote yametokana na kuwa ni mdau wa hii kazi.Mwenye nyingeza atakusaidia
Hope umepata idea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom