Naomba tofauti ya maneno haya yanayotumiwa serikalini

1. Idara (department) mfano idara ya usalama wa taifa
2. Kurugenzi mfano kurugenzi ya mawasiliano ikulu
3. Mamlaka (authority) mfano mamlaka ya bandari
5. Taasisi mfano taasisi ya elimu ya watu wazima
6. Tume mfano tume ya uchaguzi
7. Baraza mfano baraza la michezo
8. Wakala mfano wakala wa vipimo

Vigezo vipi vinatumika kutofautisha na mtumizi yake
Pia wakala wa M pesa, Aitel money, Tigo pesa na Halopesa!!
 
1. Idara (department) mfano idara ya usalama wa taifa
2. Kurugenzi mfano kurugenzi ya mawasiliano ikulu
3. Mamlaka (authority) mfano mamlaka ya bandari
5. Taasisi mfano taasisi ya elimu ya watu wazima
6. Tume mfano tume ya uchaguzi
7. Baraza mfano baraza la michezo
8. Wakala mfano wakala wa vipimo

Vigezo vipi vinatumika kutofautisha na mtumizi yake
Council Mfano National Council for Tech Education
Council Mfano Town Council
 
Hata hyo tume ya vyuo vikuu inaweza ikavunjwa Kama itafika mahali itakuwa haihitajiki Tena the same kwenye tume ya madini nk
Tume sio kitu Cha kudumu inaweza ikafanya kazi hata miaka kumi lakini sio kitu Cha kudumu Kama taasisi
Hicho nduo nilimaanisha

Tume ya uchaguzi , je uchaguzi ukiisha inafanya kazi gani. Naomba unieleweshe
Tume ya uchaguzi bado ipo operational, inaendelea kuratibu mambo kadha wa kadha yanayohusu uchaguzi. Tume hii haijavunjwa wala haijapumzika. Majukumu yanayofanywa na tume hiyo ni pamoja na kuratibu chaguzi ndogo, kufanya marekebisho ya daftari la kudumu la wapiga kura, kugawa maeneo ya uwakilishi (majimbo) n.k n.k


Ukisema kwamba hata tume ya vyuo vikuu inaweza kuvunjwa ikiwa haihitajiki ndio kigezo cha kwamba inafanana na "tume matukio" (tume ya katiba mpya, tume ya makinikia, tume ya mfumo wa vyama vingi, n.k) unakua unakosea sana.

"Tume matukio" zinavunjika mara baada ya suala walilokua wanashughulikia kumalizika. Mara nyingi ni baada ya kukabidhi ripoti kwa aliyeiunda (Rais).

Kuvunjwa kwa tume kama TCU, NEC n.k kunafanana na kuvunjwa kwa Mamlaka, Taasisi, Wakala, idara, halmashauri za miji au majiji.

Kwahiyo uwezekano wa kuvunjwa wa tume kama TCU usiwe ndio kigezo cha kufanana na tume matukio ambazo kimsingi zina_dissolve.

Rais Magufuli alivunja Mamlaka ya Ustawishaji makao makuu Dodoma (CDA), alivunja JIJI la DSM, angeweza kuivunja au kuifuta TBS (Taasisi), NEC (tume), TRA (Mamlaka), REA (wakala), TANESCO (shirika), NECTA (Baraza) n.k
Kusema hiki na kile vinafanana kwa sababu vyote vinaweza kuvunjwa au kuvunjika sio sahihi hata kidogo.
 
Tofauti ipo
Kila chombo kinaendeshwa kisheria
Na kinaanzishwa kisheria na sheria hazifanani, pia majukumu ya Kila chombo kulingana na sheria zilizowekwni tofauti

Wote tunakubaliana kwamba kila chombo cha serikali kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria.
Utofauti wa sheria hizo hauwezi kuwa ndio utetezi wa tofauti kati ya yaliyotajwa katika swali la mtoa mada hapo juu.

Twende kwa mifano.
Baraza la Sanaa (BASATA)
Limeundwa kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 1983 (na marekebisho ya mwaka 2019).
Sheria hiyo imetamka kwamba kutakua na BARAZA la sanaa, ambalo muundo wake utakua hivi, litakua na majukumu haya na yale.

Kwanini liwe ni BARAZA la sanaa na isiwe TUME ya sanaa, BODI ya sanaa, MAMLAKA ya sanaa, TAASISI ya sanaa, WAKALA wa sanaa, IDARA ya sanaa, n.k

Jibu la swali hili haliwezi kuwa ni "kwa sababu sheria imetamka BARAZA" maana sheria ingeweza kutamka MAMLAKA, BODI, TUME, IDARA n.k

Na hapo ndipo swali la mtoa mada linapokuja, je kuna tofauti gani kati ya mamlaka, wakala, taasisi, idara, tume, bodi, baraza n.k

NB: Kila chombo cha kiserikali (tume, bodi, baraza, mamlaka, n.k) ni lazima kiwepo kisheria (kipewe legal being), hakiwezi kuanza kiholela kama GROUP LA WHATSAPP
 
Mamlaka.. authority.. power... nguvu... mamlaka ya mapato... lazma ulipe kodi..
Safi sana. Hutoi gari bandarini(TPA) mpaka umuone mzee TRA. Vinginevyo litaozea kule. The authority to control certain activity regarding specific issue (large scale) given by the Government (Power)
 
Mkuu, katika ufuatiliaji wangu nimekuja kugundua haya mambo yana mkanganyiko mkubwa sana na hakuna clear difference baina ya hayo majina ya hivyo vyombo vya kiserikali.

Ukitaka kuweka utofauti, kuna sehemu nyingine utakutana na kukiukwa kwa ile tofauti (contradiction).

Kwa mawazo yangu ni kwamba, hayo maneno sio kwamba yana maana moja, la hasha. Ila yanatumika ili angalau kuleta utofauti baina ya vyombo mbalimbali vya serikali maana viko vingi sana (isingependeza kila chombo kuitwa taasisi).

Mfano, ukisema kurugenzi ni chombo ambacho kinaongozwa na mkurugenzi, unakuja kugundua kwamba kuna mamlaka, wakala au taasisi zinaongozwa na wakurugenzi pia (contradiction).

Nizungumzie TAASISI kidogo. (Hoja yako namba 5).
Kwa ufahamu wangu, najua kuna taasisi za aina mbili, kuna zinazoitwa "institutes (au institutions)" na zile zinazoitwa "Bureau". Sasa je kuna tofauti gani kati ya hizi "taasisi mbili"
Mifano:
Taasisi Bureau
NBS (Takwimu)
TBS (Viwango)
PCCB (Rushwa)
N.k
Taasisi Institute
TARI (Utafiti kilimo)
NIMR (Utafiti afya)
JKCI (Taasisi ya Moyo J. Kikwete)
MOI (Taasisi ya mifupa)
TIE (Elimu)
N.k

Sasa kama hata kwenye taasisi tu kuna mkanganyiko, itakuaje huko kwingine?

Umelata hoja nzuri, ngoja wajuvi na wajuzi watutoe tongotongo
Nimepata kitu ngoja waje wengne chief
 
Safi sana. Hutoi gari bandarini(TPA) mpaka umuone mzee TRA. Vinginevyo litaozea kule. The authority to control certain activity regarding specific issue (large scale) given by the Government (Power)
Endelea
 
Back
Top Bottom