Habari za ahsubuhi wana Jf! Naomba madokta wa humu ndani kama wana uzoefu kuhusu uvimbe wa mafuta kwa kitaalam Lipoma au (Fatty tumors/lump) nini causes zake,tiba,na prevention ya lipoma! Thanks!
---Majibu kutoka kwa wadau---
---Majibu kutoka kwa wadau---
LIPOMA NI NINI?
Lipoma ni uvimbe unaotokea kutokana na kukua zaidi kwa seli mafuta ( fatty cells) na uvimbe huu huonekana ndani ya ngozi. Lipoma sio saratani na haiwezi kuwa saratani. Sehemu zinazo hathiriwa sana ni shingoni, kwenye mapaja, mikononi, kwenye makwapa, ila inaweza tokea sehemu yoyote ya mwili.
LIPOMA HUSABABISWA NA NINI?
Lipoma bado haijafahamika husababishwa na nini hasa, ila kwa tafiti zilizofanywa huonesha kuwa asilimia kubwa huwa ni urithi( heredity) kutoka kizazi hadi kizazi, pia kuumia kunakoweza kukusababishia uvimbe usiopungua.
UTAJUAJE KUWA UNA LIPOMA?
Lipoma kwa kawaida huonekana kwa macho pia ukikishika kinasogea( movable) na ni laini kama mpira, pia hakina maumivu yoyote na huwa ni kidogo lakini hukua kadri miaka inavyoenda.
Kitaalam inaweza ikachukuliwa sample ya sehemu ya uvimbe ( biopsy) na kwenda kufanyia uchunguzi kugundua kama kutakuwa na saratani ndani yake.
JINSI YA KUTIBU LIPOMA.
Lipoma kwa kawaida huwa haitibiwi ila itatolewa kama kutakuwa na maumivu au kuathiliwa na vimelea vya magonjwa.
Lipoma hutolewa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo( minor surgery) kwa kuzingatia usafi wa hali ya juu (sterility) ili kupunguza maambukizi ya magonjwa mengine.