mashi ga ngoko
Member
- Jul 15, 2018
- 96
- 50
Salaamu watanzania,
Leo naandika haya kwa uchungu mkubwa baada ya jana kuona ukandamizwaji wa haki za kibinadamu kwa macho yangu, ukiukwaji wa sheria ukifanyika hadharani Jeshi la Wananchi Tanzania katika kambi ya Jeshi iliyopo Mbagala.
Siku ya jana Majira ya saa 3 usiku kulikuwa na foleni kubwa barabara ya Kilwa road, kama wewe ni mwenyeji utakubaliana na mimi kuwa katikati ya kituo cha Kizuini na Zakhem kuna kambi ya Jeshi
Kwa kuwa kulikuwa na foleni baadhi ya magari yalikuwa yanatumia barabara ya service road ambayo ipo upande wa Jeshi. Pamoja kuwa eneo hilo la Jeshi limepakana na barabara lakini wanajeshi wamekuwa wakisimamisha magari na kuwashusha raia huku wakiwapiga mateke ngumi, viboko na kuwapa adhabu mbalimbali hali amabayo imekuwa ikiwadharirisha na wengine kuumia vibaya.
Tunaomba Serikali iingilie kati suala hili.