Naomba Serikali iingilie kati suala la Wananchi kuambulia vichapo kutoka kwa Wanajeshi

Jul 15, 2018
96
125
Salaamu watanzania,

Leo naandika haya kwa uchungu mkubwa baada ya jana kuona ukandamizwaji wa haki za kibinadamu kwa macho yangu, ukiukwaji wa sheria ukifanyika hadharani Jeshi la Wananchi Tanzania katika kambi ya Jeshi iliyopo Mbagala.

Siku ya jana Majira ya saa 3 usiku kulikuwa na foleni kubwa barabara ya Kilwa road, kama wewe ni mwenyeji utakubaliana na mimi kuwa katikati ya kituo cha Kizuini na Zakhem kuna kambi ya Jeshi

Kwa kuwa kulikuwa na foleni baadhi ya magari yalikuwa yanatumia barabara ya service road ambayo ipo upande wa Jeshi. Pamoja kuwa eneo hilo la Jeshi limepakana na barabara lakini wanajeshi wamekuwa wakisimamisha magari na kuwashusha raia huku wakiwapiga mateke ngumi, viboko na kuwapa adhabu mbalimbali hali amabayo imekuwa ikiwadharirisha na wengine kuumia vibaya.

Tunaomba Serikali iingilie kati suala hili.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
24,993
2,000
Kama umesoma vizuri thread usingesema hivi,tunakopita ni service road ambayo imepakanna na eneo la jesho,namaanisha ndani ya bicon ya Tanroad.
Service road Toka lini ikatumika kama barabara ya kutembeza magari.Traffic akikudaka utakoma .Hizo leseni zenu za kuhonga kuletewa majumbani Bila kupitia driving school matokeo yake ndio hayo service road iogope kama ukoma sio kazi yake kutumika kama barabara ya kawaida iwe karibu na jeshi au popote
 
Ni kweli lakini hali hiyo iliwakumba hata watembea kwa miguu,Je kukamata magari yanayokiuka sheria ni kazi ya Ya mwanajeshi au Trafic?
 
avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
3,998
2,000
Mjifunze kutii sheria, kazi ya service road ni kupitisha magari? kwani hata kukiwa na foleni itadumu siku mbili? kwa nini usiwe na uvumilivu kila kitu unapenda kuwahi wahi? nashauri hao wanajeshi waongeze kadoze kidogo maana kuna baadhi ya madereva wa hiace na boda boda hawana uvumilivu hata kidogo na wamekuwa chanzo cha kusababisha ajali kwa watembea kwa miguu, unakuta gari lililo mbele yake limesimama na limeshaona hatari lakini yeye anamwona kama kichaa na kutaka kum overtake mwisho wa siku ajali
 
2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,550
2,000
KWA NINI MPITE ENEO LA JESHI BILA RUHUSA, UNAFIKIRI HAO NI MGAMBO, HUO NI MOTO BABA,KAA MBALI
Tlishawahi kuingilia msafara aa jeshi unatoka Monduli kwenda Dodoma.. Aisee walitulazimisha tuwafate hadi mafuta yalipoisha katikati ya Misitu ya Babati na Bereko.. Hao jamaa wasikie tu wanaadhabu za kutesa mwili na akili.
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,226
2,000
Askari polisi,na wanajeshi wa vyeo vya chini,ni watu wanaoishi kwa msongo mkubwa wa mawazo,stress kibao,wao wenyewe wananyanyaswa vibaya na wakubwa wao,kwahiyo njia pekee ya kumaliza hasira zao,ni kuwasulubu RAIA.
Ukiona MTU ana abuse wengine,iwe mtoto,mke Mme,ujue yeye mwenyewe ni muhanga wa manyanyaso.zamani nirikuwa siwezi kuwapita wajeda,bila kuwapa lift,Siku hizi thubutu yake,
Akiingia anga zangu hata vichwa namlukia,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jul 15, 2018
96
125
Mjifunze kutii sheria, kazi ya service road ni kupitisha magari? kwani hata kukiwa na foleni itadumu siku mbili? kwa nini usiwe na uvumilivu kila kitu unapenda kuwahi wahi? nashauri hao wanajeshi waongeze kadoze kidogo maana kuna baadhi ya madereva wa hiace na boda boda hawana uvumilivu hata kidogo na wamekuwa chanzo cha kusababisha ajali kwa watembea kwa miguu, unakuta gari lililo mbele yake limesimama na limeshaona hatari lakini yeye anamwona kama kichaa na kutaka kum overtake mwisho wa siku ajali
Hawana mamlaka hayo,kama ingekuwa Trafic sina shida wala nisenge lalamika.
 
Aiba

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,007
2,000
Mjifunze kutii sheria, kazi ya service road ni kupitisha magari? kwani hata kukiwa na foleni itadumu siku mbili? kwa nini usiwe na uvumilivu kila kitu unapenda kuwahi wahi? nashauri hao wanajeshi waongeze kadoze kidogo maana kuna baadhi ya madereva wa hiace na boda boda hawana uvumilivu hata kidogo na wamekuwa chanzo cha kusababisha ajali kwa watembea kwa miguu, unakuta gari lililo mbele yake limesimama na limeshaona hatari lakini yeye anamwona kama kichaa na kutaka kum overtake mwisho wa siku ajali
Mtu akikosea c kumpiga tujifunze kufata sheria kuna faini za barabarani au kumfikisha mahakamani unampiga mtu akikufia unabaki ww na familia yako wakukutetea hayupo alafu unatete ni ujinga sana kuwa mwanajeshi haimaanishi uko juu ya sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
avogadro

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
3,998
2,000
Mtu akikosea c kumpiga tujifunze kufata sheria kuna faini za barabarani au kumfikisha mahakamani unampiga mtu akikufia unabaki ww na familia yako wakukutetea hayupo alafu unatete ni ujinga sana kuwa mwanajeshi haimaanishi uko juu ya sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu ambao bila mkongoto ulioenda shule hawasikii !!!! hao kulipa faini watalipa lakini kesho watarudia!!! nakuhakikishia kwa sasa watasimuliana wakifika eneo hilo wataliheshimu na hawatalisogelea...
 
Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,272
2,000
Service road Bado Ni njia ya gari lakini kwa matumizi maalum. Mfano unatokea mlimani City unataka kwenda Sinza kuoitia kwa kakobe lazima uchepuke kupitia service road. Hivyo sio kosa kupita service road, Ila iwe kwa matumizi kusudiwa.

Pili Kama dereva kakosea kupita njia ambayo sio au matumizi sio adhabu yako inajulikana fine au mahakamani.

Je hai wanajeshi wamepata wapi mamlaka ya kupiga hai madereva?

Pili kosa lifanywe na dereva iweje abiria wapigwe? Na mamlaka hiyo ya kupiga raia wamepata wapi?

Ukisikia kukiuka Hali za binadamu Ni huku kupiga raia pasipo kuchujukiwa hatua ilihali serikali IPO?

Wanaofanya vitendo hivyo wapo wanajulikana?

Kama Ni eneo muhimu weka ilani.

Mfano: Nyuma ya ikulu happy Dar Kuna bango kubwa kabisa Hakuna njia. Kwa Nini kueluka usumbufu na yeyote atakaepita anayohaki ya kuchukuliwa hatua.

Mwisho madereva hutumia barabara kulingana na vibao vinaonyesha alama gani. Hivyo Kama Hakuna alama yeyote ya katazo. Mahakani atakushinda tu

Ombi: usimfanyie mwenzio kile usichopenda kufanyiwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom