Naomba sababu tatu kwanini mtu amiliki laini za simu zaidi ya moja!

Nimejiuliza swali hili baada ya jamaa mmoja hapa jirani kusema anamiliki laini 4 za simu kwa ajili ya kucheza bahati nasibu kila anunuapo vifurushi. Nimecheka sana.........labda serikali inataka kupunguza huu upuuzi. Wewe je una sababu gani za kumiliki laini zaidi ya moja?
Nawewe tupe sababu tatu kwanini mitandao ya simu ipo zaidi ya mmoja!!
 
Labda kama line zaidi ya moja inazuia ujenzi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati nitamuunga mkono mhe. Waziri.
 
Moja ya voda Ni ya ofisi kwa kazi za ofisi,moja iko nyumbani kwa ajili ya mawasiliano,ya tatu ni kea ajili ya modem ya internet ,nne Ni ya kampuni ya Airtel pindi nikienda manyara na sehemu Voda haikamati vizuri line ya meisho Ni TTCL kea ajili ya backup ya internet.So line tano
 
Au tunaandaliwa kufosiwa kutumia T. C. C. L peke yake ? na wakifanya hivyo hiyo kampuni ya uma ndiyo bye bye !!
 
Nimejiuliza swali hili baada ya jamaa mmoja hapa jirani kusema anamiliki laini 4 za simu kwa ajili ya kucheza bahati nasibu kila anunuapo vifurushi. Nimecheka sana.........labda serikali inataka kupunguza huu upuuzi. Wewe je una sababu gani za kumiliki laini zaidi ya moja?
1. Ni uamuzi wangu, kwani nanunua line kwa fedha yangu, na naziendesha kwa fedha zangu. After all Tanzania kuna free market unless mniambie sasa tumerudi kwenye uchumi wa kudhibitiwa na dola.

2. Mitandao ina tozo tofauti kwa huduma tofauti, hivyo ni njia mojawapo ya kupunguza ughali wa Maisha. Mfano, halotel wana nafuu kwenye vifurushi vya data, airtel wana vifurushi nafuu vya kupiga, Tigo ina unafuu kwenye vifurushi vya kupiga mitandao yote na voda ina huduma nzuri ya M-PESA (hii ni mifano tu. Je, Kwa kuwa na line nyingi si tunaenda sambamba na nia ya Mkuu wa Nchi kujali Wanyonge kama Mimi.

3. Hakuna mtandao hata mmoja ambao upo kila kona ya nchi. Hivyo kwa kuwa mimi sio mti, nina move kutoka eneo moja kwenda jingine kila wakati, kuwa na line nyingi kunaniwezesha kuwasiliana mahali popote na wakati wowote na mtu yoyote.

Je sababu hizo hazitoshi kuniruhusu kumiliki idadi ya line ninazotaka?
 
Hakika kama mimi ndio TCRA ningefanya laini ya pili kama chanzo cha mapato ya serikali badala ya kuomba kibali kwao ikawa kwa kila laini ya ziada unailipia kwa mwaka elfu hamsini (50000)TRA na usipoilipia inafungwa ni mfumo tu ungetengenezwa kati ya tcra na tra kutambua namba husika inayopaswa kulipiwa
 
Nimejiuliza swali hili baada ya jamaa mmoja hapa jirani kusema anamiliki laini 4 za simu kwa ajili ya kucheza bahati nasibu kila anunuapo vifurushi. Nimecheka sana.........labda serikali inataka kupunguza huu upuuzi. Wewe je una sababu gani za kumiliki laini zaidi ya moja?
Zipo sababu nyingi, wapo watu ambao ni wafanyibiashara na wanawasiliana na watu wengi sana kila iitwapo leo, hivyo akitafutwa kwenye laini moja ikizingua atapatikana kwenye laini nyingine. Pia zipo kampuni za simu zenye huduma ya kutuma pesa nje ya nchi kama ada za shule n.k , wakati kampuni nyingine hazina huduma hiyo. Hata gharama za kupiga simu nje ama gharama za vifurushi zinatofautiana , hizo ni baadhi ya sababu , pia watu wanamiliki handset Zaidi ya moja na kila handset ina beba laini moja.
Leo tukihoji kwa nini mtu anamiliki laini Zaidi yamoja , kesho tutahoji kwa nini mtu amiliki gari Zaidi ya moja nk
 
Nimejiuliza swali hili baada ya jamaa mmoja hapa jirani kusema anamiliki laini 4 za simu kwa ajili ya kucheza bahati nasibu kila anunuapo vifurushi. Nimecheka sana.........labda serikali inataka kupunguza huu upuuzi. Wewe je una sababu gani za kumiliki laini zaidi ya moja?
Nina tigo, voda na halotel. Kila laini ina faida zake kwangu kama ifuatavyo:-

1. Halotel, naitumia kwa data pekee, kama nimewahi kuitumia kupiga, hata sikumbuki lini ilitumika.

2. Vodacom, ni nzuri kwa mobile transaction, kila eneo utawakuta. Aidha ukiwa na voda, huku kanda nilipo ndo mtandao pendwa. Kifurushi cha 2,000/- kwa wiki, kinaniconect na wadau wengi kwa urahisi.

3. Tigo ni laini kongwe tangu chuo. Napenda furushi lao la sms, hivyo ninapokuwa na kazi ya kutumia ujumbe, tigo ni rahisi zaidi kwa 1500 kwa mwezi.

Siku wakiweka usawa, yaani data, dk za kuongea mitandao yote, sms na coverage ikawa sawa kwa kampuni zote, sitaona sababu ya kumiliki laini zote nilizonazo
 
Ttcl hii ya vifurushi vya internet
Tigo huu kwa ajili ya ndugu, jamaa na marafiki
Airtel huu ya kuwasiliana na wateja wangu.
 
Back
Top Bottom