Naomba sababu tatu kwanini mtu amiliki laini za simu zaidi ya moja!

Nikiwa na Airtel nikienda nayo mkoani kwangu network yake ni hovyo. Hapo inabidi nitumie Tigo.

Lakini nikitaka huduma za kifedha M pesa ndiyo ina agents.

Sasa wanakuja watu hawana akili sawa wanashangaa kwanini mtu una laini zaidi ya moja.
 
In addition, hata wafanyakazi wa TCRA wana laini zaidi ya moja. Sijui wamekula maharage ya wapi kuja na matamko ya ajabu. Au labda mleta mada amewavutisha lile jani?!?
Wafanyakazi wa Tcra nao ni wanajamii wana mahitaji sawa na wengine. Muhimu ni sababu tu za kumiliki!
 
Mie nina mbili.
1. Airtel hii ina umri wa mtu. Since 2001 sijabadilisha.
2. Halotel kwa ajili ya data. Sizijui hata namba zake. Nilikuwa na tigo nikawapumzisha.
 
Kwani laini nyingi zinazuia uchumi wa viwanda sio?Mtu hata akiamua kuwa na laini mia..kwani tatizo liko wapi..cha msingi asajili kama ilivyo ada...kuna vitu vidogo sana ambavyo watu wanapoteza muda tu....
Line zangu,vocha yangu,bundle langu,simu zangu..sasa hapo tatizo liko wapi?
 
Mi ninazo NNE tigo 2 VODA na halotel. Tigo moja ya chuo nyingine ni ya kawaida,VODA na halotel ni kwa ajili ya internet (speed na ukubwa bando)
 
Ninamilliki biashata mbili katika maeneo tofauti. Sim card moja ipo mkononi mwangu na nyingine mbili katika sehemu zilipo hizo biashara. Ni unafuu wa kukusanya na kutoa pesa.
 
Kwa Mimi ni utofauti was gharama za matumizi. Kila kampuni lina nafuu zake tena kubwa sana hata kwa network ni tofauti msituletee. Kuiga nchi za kidictotor.
 
Kwa sisi wafanya biashara .ni muhimu kuwa na namba zaidi ya moja.
alafu sisi ni watu wazima.
Masuala ya kutupeleka peleka Kama watoto wa shule.ni mambo ya kiboya.
USITUPANGIE CHA KUFANYA.
SIMU ZETU, LAINI ZETU.
WEWE UNAWASHWA NA NINI?
alafu masuala ya kusajili laini YAMETOA AJIRA NYINGI KWA VIJANA.
MNATAKA WAJE WAFANYE KAZI GANI?
Najua mtasema kwa ajili ya usalama.
lakini nyie nyie mliopo kwenye system ndo WAHALIFU WAKUBWA.
mmefanya nini kuwakamata watu waliokuwa wanamtishia Ben kwenye simu mpaka akapotea?
 
Kakojoe ulale, mambo yakupangiana usiwe na mchepuko yanatoka wapi, mwl jkn Nyerere alisema adui mkubwa wa mtanzania nii, ujinga, maradhi na umasikini, du tutafika tu safari
 
Kwa sisi wafanya biashara .ni muhimu kuwa na namba zaidi ya moja.
alafu sisi ni watu wazima.
Masuala ya kutupeleka peleka Kama watoto wa shule.ni mambo ya kiboya.
USITUPANGIE CHA KUFANYA.
SIMU ZETU, LAINI ZETU.
WEWE UNAWASHWA NA NINI?
alafu masuala ya kusajili laini YAMETOA AJIRA NYINGI KWA VIJANA.
MNATAKA WAJE WAFANYE KAZI GANI?
Najua mtasema kwa ajili ya usalama.
lakini nyie nyie mliopo kwenye system ndo WAHALIFU WAKUBWA.
mmefanya nini kuwakamata watu waliokuwa wanamtishia Ben kwenye simu mpaka akapotea?
Kumbe jibu unalijua!
 
Back
Top Bottom