Naomba picha ya Stendi kuu ya mabasi Moshi nione kama ina tofauti na ile ya Bukoba tujiridhishe na CHADEMA!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,888
141,822
Sina mambo mengi naomba bwashee yoyote mwenye picha ya stendi kuu ya mabasi pale Moshi aitupie hapa.

Manispaa ya Moshi kwa muda mrefu imeongozwa na Chadema nataka kujiridhisha na ubunifu wao.
Hapa Iringa Chadema walijitahidi wakatujengea Stendi ya kisasa pale Igumbilo ila sijajua kule Mbeya kwa Sugu hali ikoje.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Jo sometimes nalinganisha akili zako na za ndugai
 
Sina mambo mengi naomba bwashee yoyote mwenye picha ya stendi kuu ya mabasi pale Moshi aitupie hapa.

Manispaa ya Moshi kwa muda mrefu imeongozwa na Chadema nataka kujiridhisha na ubunifu wao.
Hapa Iringa Chadema walijitahidi wakatujengea Stendi ya kisasa pale Igumbilo ila sijajua kule Mbeya kwa Sugu hali ikoje.

Mungu ni mwema wakati wote!
Bukoba uwekezaji wao upo Airport..
Ina uafadhali kuliko ya Mwanza...

Kwenye stand ni tope tu limejaa pale halifananishiki na popote
 
Aisee nimepita mikoa mingi stendi ya moshi iko safi tatizo sio chadema tatizo ni mipango miji hii stendi iko katikati ya mji kitu ambacho hakikupangiliwa kwa utashi ila naskia kuna eneo liko Toyota sijajua itamishwa lini
 
Soon tu,mpya hii hapa

41744453_328470861046390_7024032770494038016_o.jpg
 
10 Jun 2020
Serikali mkoani Kilimanjaro imeongeza timu ya wataalam kufanya utafiti wa kina kubaini kiini cha chemchemi chini ya jengo la kituo kipya cha mabasi cha kimataifa Ngangamfumuni mjini Moshi, Tanzania.

Habari za ziada :

July 9th, 2020
Moshi, Kilimanjaro
Tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo ametoa ushauri kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Mjini kukaa na wataalam ili wafanye utafiti wa kina wa jinsi ya kukabiliana na maji yaliyopo chini ya ardhi katika eneo lililojengwa kituo cha Mabasi.
Ujenzi Wa Stendi Ya Mabus Moshi Mjini Mkondo Wa Maji

Picha : Ujenzi wa Stendi mpya ya Kimataifa ya mabasi , Moshi Tanzania

Ujenzi Wa Stendi Ya Mabasi Moshi Mjini unakabiliwa na changamoto Mkondo Wa Maji unaoibua chemchem katika ghorofa ya chini ya ardhi katika ujenzi wa stendi hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Moshi wakati akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.

Mhe. Jafo amesema kuwa kwa sasa maji yanapita katika eneo hilo lakini yakiwa yamepungua, huku wataalamu wakiendelea kutafuta ufumbuzi kwa maji kujaa yakitokea chini ya Ardhi.

Ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Moshi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo hasa katika ujenzi wa miradi ya kimkakati japokuwa mradi huo umekuwa na changamoto ya jengo kujaa maji kwa chini.

Aidha Mradi wa Stendi ya Mabasi Mkoani huo utagharimu shilingi bilioni 28 fedha ambazo zilitolewa na Serikali kwa Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa Miradi ya kimkakati.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Bw. Michael Mwandesi ameeleza kuwa mradi wa stendi ya mabasi umepata changamoto kubwa ya jengo kujaa maji chini jambo ambalo lilisababisha Halmashauri kusimamisha ujenzi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa chanzo cha maji hayo.

Amesema mpaka sasa wataalam wameshafanya utafiti wa kina na imegundulika kuwa jengo hilo halijaathrika na maji hayo, kutokana na uimara mkubwa wa jengo hilo.

Source : Jafo aagiza wataalamu kufanya utafiti wa maji yaliyochini ya ardhi mradi wa Stendi ya Mabasi

21 June 2020
Moshi, Kilimanjaro
Tanzania

Wataalamu wa Jiolojia wafanya utafiti wa Chemchem mkoani Kilimanjaro

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kurugenzi ya Huduma kwa Umma pamoja na Idara ya Jiologia kutoka Ndaki ya Sayansi Asili na Sayansi Tumizi, imeleta wataalamu wa maji ya ardhini ili kuisaidia Manispaa na Moshi kupima na kuangalia maji yanayotoka ardhini na kujaa kwenye makazi ya watu na katika mradi mpya wa Stendi maeneo ya Majengo. Msafara huo wa wataalamu unaongozwa na Dkt. Mona Mwakalinga- Mkurugenzi Huduma kwa Umma, Dkt. Simon Melekioly, Dr. Remigius Gama na Bwn. Majura Songo kutoka Idara ya Jiolojia.
Source : University of Dar es Salaam
 
Hivi kuna halmashauri yoyote ya mji au wilaya iliyokuwa inaongozwa na chadema ambako wamefanya jambo lolote la maana kweli? Mbona sijaona wala kusikia!
Kama ofisi ya makao makuu imewashinda, itakuwa kujenga stendi?
 
Tatizo wale Bukoba wameishia kuwa 'chawa' ,na hakuna cha maana chochote kwenye mji/ mkoa wao..... ..... .... kazi kwelikweli.
Bukoba uwekezaji wao upo Airport..
Ina uafadhali kuliko ya Mwanza...

Kwenye stand ni tope tu limejaa pale halifananishiki na popotko
 
Back
Top Bottom