Elections 2010 Naomba oradha ya wabunge wa chadema walioshinda mpaka hivi sasa

Bob_Dash

Member
Nov 1, 2010
90
13
Nimekuwa nikipitia blog mbalimbali kutafuta takwimu ya wabunge wa CHADEMA waioshinda katika majimbo yao, lakini bado sijafanikiwa kupata habari za uhakika, zaidi ya Zitto Kabwe ambaye ameshinda takribani katika vituo vyote vya kura huko Kigoma-vijijini. Sasa naomba tuweke majina yao na majimbo yao.
 
Jamani huku Arusha wanachakachua maana chadema wamepata viti vya udiwani 12, ccm 6 na chadema 1.wanatakakusema eti batlida wa ccm ameshinda kwa silimia 62 sis tumekataa mpaka sasa watu wamejaa manispaa
 
Wawakilishi wa CHADEMA katika zoezi la kuhesabu kura walikuwa wapi???? Halafu mbona viongozi wa CHADEMA wako kimya ??? WHAT'S GOING ON OVER THERE????
 
Lowasa kweli mtaalamu wa kifisadi, amekwenda kufisadi uchaguzi wa Arusha mjini!!!! Kama ni vurugu hizi ndizo dalili za kuleta vurugu!!!
 
Hivu huyu EL ni mtanzania kweli?achunguzwe manake inatia shaka sana kila jambo analoshiriki.Watanzania tuwe makini tungemsikiliza mwalimu mapema sana huyo mtu hatari wanataka kutuvurugia amani
 
Mi kweki Arusha mjini CHADEMA imeshinda lakini kinachoonekana ni uchakachuaji.
wanchi wenye uchungu na nchi yao, na wapenda haki, wamejumlisha matokeo kwenye vituo vyote Lema anaongoza kwa kura nyingi sana. yani amemvuruga Buriani vibaya sana, lakini cha ajabu hawataki kutangaza. na kwa hali hii watachochea vurugu.
 
Kinachotokea Arusha ni sawa kabisa na kinachotokea Nyamagana. tangu jana jioni Masha ilishajulikana ameshindwa tena vibaya sana lakini eti kujumlisha matokeo na kutangaza imekuwa issue.


Mkurugenzi wa Mwanza badala ya kutangaza matokeo amemwita Katibu wa CCM wa wilaya, na hai sasa wako ndani wanajadili. Nje ya jengo walilopo wananchi wapenda haki wamezingira jengo hilo la halmashauri.

Hizi si dalili nzuri, maana wakijaribu kuchakachua matokeo, vurugu zitakazotokea hakuna wa kuweza kuzuia.
 
Fredie Mpendazoe, Segerea Ukonga originally posted by Wambandwa

Mh hii ni ya kweli!!!
 
Hii ya kweli kabisa mr.tukutuku,
mi mwenyewe nimesikia nikalazimika kusitisha shughuli zangu kwenda kujionea. Watu walikuwa wengi sana hali iliyoashiria vurugu kama haki yetu ikipokwa.
 
mwingine aliyeigaragaza ccm bila huruma ni mzee philmon ndesamburo, wa chadema,moshi mjini.

amemshinda mpinzani wake wa karibu wa ccm mr.salakana kwa kishindo kikubwa mno.

nevrthelss chadema wameshinda kata 18 jimbo la moshi mjini huku ccm wakiambulia kata 3 tu.
so, council ya moshi municipality itaongozwa na chadema, baaa ya kukaa mikononi mwa mafisadi kwa muda mrefu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom