Naomba nisaidiwe namna ya kutengeneza cake ya kawaida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba nisaidiwe namna ya kutengeneza cake ya kawaida

Discussion in 'JF Chef' started by Mbwambo, Oct 11, 2012.

 1. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Wana jamii nimepata mengi sana kwenye JAMII FORUMS na nina imani hata hili wapishi au Chef wa Jamii forums atanipatia
  NATAKA NIWE NATENGENEZA BIRTHDAY CAKES KWA FAMILIA YANGU MWENYEWE
  ASANTE
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hii hapo sasa ila ni kizungu sasa itabidi ukomae tu mkuu...

   
 3. k

  kisukari JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  kwa ninavyopika mimi keki.
  ingredient:
  mayai sita {tatizo la mayai mengine yanakuwa na maji mengi} kiurahisi chukua kikopo cha siagi robo kilo.hiyo siagi iweke kwenye bakuli lako.
  na sukari ipimie kwenye hicho hicho kikopo cha siagi ila isijae mpaka juu.ichanganye pamoja na siagi.kama una mashine yako ya kusaga saga,mpaka ilainike.hicho hicho kikopo chako cha siagi,tia mayai yako.ila yasijae mpaka juu.mwaga kwenye huo mchanganyiko wa siagi na sukari.
  saga wee,mpaka unakuwa uji mzito.hicho hicho kipimo chako cha siagi,tia unga wako wa ngano mpaka juu
  mwagia kwenye ule mchanganyiko wako,tia baking powder kijiko kimoja cha chai.
  unatia flavour yoyote unayopenda kama vanila au rose,au ya machungwa au ya mananasi.kila mtu na test yake.nusu ya kijiko chs chai.
  unachukua mwiko wako,unachanganya{hapo hautumii mashine}unachanganya kwa muda kama wa dakika 2.{umemaliza}
  unapaka sufuria lako mafuta kidogo.unakata karatasi lako ambalo liko plain,shape ya sawa na chombo unacho bake keki yako.unaiweka ndani.
  unatia mchanganyiko wako.{mimi hupendelea rangi 2,ya chicklate na ya kawaida}kama unataka keki iwe kati kati ina rangi.unachukua mchanganyiko wako kidogo,unautia kwenye bakuli,unachanganya na cocoa.ukimaliza.mchanganyiko wako mweupe unautia chini mwanzo
  halafu katikati unaweka mchanganyiko wako wa rangi ya cocoa na juu unamalizia mchanganyiko wako mweupe.unaweka kwenye oven.wakati vkeko ipo ndani ya oven utasikia harufu nzuri ya kunukia.na ukitaka kujua keki imeiva katikati
  unachukua kijiti kikavu unakiingiza katikati.kijiti kikitoka kikavu,maana keki imeiva.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  acha nikumbuke....... Keki ya fasta fasta.....

  - Unga, siagi, sukari (kumbuka kipimo cha siagi na unga ni half fat to flour)
  - mayai 4 au it depends na ukubwa wa keki
  baking powder
  vannila (vitone vichache), kama huna vanila kwangua ganda la kijani la limao (hapa una grate, hii ni kuondoa shombo na kutia harufu taaamu)

  - changanya siagi na sukari koroga mpaka iwe nyeupe flani (ni vyema kama una mashine itakua fasta, kama huna bakuli kubwa la kioo na mwiko bapa vinahusika - hii niliitumiaga sekondari kwenye kipindi cha cookery)
  tia mayai mix
  tia vanila/maganda uliyograte ya limao mix
  unga uchanganye na baking powder then mix
  kama una zabibu au vikorombwezo (sometimes maziwa kwa mbaaali sana inategemea na mbwembwe zako), mix

  paka baking tins zako siagi, hii huzuia keki kuganda kumbuka hapo oven iwe ushawasha
  weka mchanganyiko wako
  bake mpaka iiwe.....

  Kuhakikisha keki yako imeiva vyema chukua palate knife dumbukiza, ikitoka clear jiandae kuidecorate

  sijui nimeeleweka , i hope sijaacha kitu
   
 5. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Asante sana kwa kunipa hitaji langu barikiwa
   
 6. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  asante sana nimekuelewa barikiwa
   
 7. m

  micky mouse Senior Member

  #7
  Mar 22, 2013
  Joined: Feb 15, 2013
  Messages: 157
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  wow kesho natoa kitu majirani wakae chonjo na harufu
   
 8. N

  Nabii Mleke Member

  #8
  Mar 23, 2013
  Joined: Mar 22, 2013
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Mi Mgen Nimetokea Fb
   
 9. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2013
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Mkuu badili tabia yaani ni umekimbia kiasi kwamba kuna baadhi ya details zinamiss so without hard feelings allow me to have them shared with other JF members.
  Back to the topic, tutaanza na mahitaji then procedures and lastly heat specificatios.
  Mahitaji;

  1. EGGS .............................. 5
  2. SUGAR ............................ vijiko 4 hadi 5 vya chakula
  3. Siagi......................... .......¼ Kg ( hata ya 100g may work)
  4. Vanilla....................... ......... Vijiko 2 vya chai
  5.Unga wa Ngano.................. vijiko vya chakula10
  6. Baking Powder................... vijiko vya chai 2
  7. Zabibu kavu......................... ½ kikombe cha robo lita (si lazima)
  NB; hayo mahitaji ni kwa jili ya keki ndogo kabisa hivyo basi vipimo vipo subjected to change depending na size ya cake utakayo.
  Najua kwa wabongo tulio wengi tunakuwa na sukari zile nene za kawaida za kuunga kwenye chai ila na ni kikwazo kikubwa katika keki kuiva Barabara ila tuungane katika kipengele cha namna ya kutengeneza.
  JINSI YA KUANDAA ;

  1. Weka sukari kwenye kinu na itwange hadi iwe powder kabisa ( kwa wale wenye common brown sugar kama za ilovo)
  2. Weka unga wa sukari kwenye bakuli lako la kukorogea ukichanganya na Blue band
  3. Changanya huo mchanganyiko wa sukari na Blue Band kwa nguvu hadi B/Band iwe nyeupe kabisa na sugar particles ziyeyuke kabisa.
  4. Weka mayai kwenye mchanganyiko wa B/Band na Sukari na koroga kwa nguvu hadi mchanganyiko uwe wa aina 1 (kama una blender itakuwa safi pia)
  5. Weka Unga wa ngano vijiko kama 5 kwanza then huku ukiangalia uzito wa mchanganyiko wako endelea kuweka unga katika huo mchanganyiko hadi vijiko 7 au nane then angalia uzito wa mchanganyiko. Mchangayiko usiwe mwepesi sana au mzito sana (kwani ikiwa nzito sana haitaiva vizuri katikati ). Koroga kwa nguvu hadi mchanganyiko ushikane vizuri na kusiwe ma mabonge yoyote yale.
  6. Weka B/powder yako na endelea kuchanganya (ni vizuri katika hii hatua ya mwisho hata kama una blenda ukakoroga kwa mkono katika bakuli ili mchanganyiko uwe vizuri/ichanganyike vizuri.
  Wakati huo huo kama unatumia mkaa basi moto wako uwe tayari na umewaka vizuri au kama unatumia oven basi uwe umewasha oven kama dakika 5 kabla ya kuanza kuoka keki yako.
  HEAT SPECIFICATION
  Washa oven yako joto liwe nyuzi 150, ila kwa mkaa hakikisha kuwa moto sio mkali sana au joto halipo chini sana ila la wastani. Kama moto ukiwa mkali haitaiva ila itababuka tu juu juu na kama ukiwa ni mdogo basi keki haitaumuka wala kuiva vizuri.
  Baada ya dakika 15 au 20 basi angalia kama keki yako imeiva , Jinsi ya kujuwa kama keki ipo tayari ni kuingiza kijiti kwenye keki na kikitoka na mchanganyiko unao nata ujuwe bado, ila kikitoka kikavu basi keki yako ipo tayari, pia hata rangi ya nje utaiona imebadilika…
  Enjoy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:smile:
  SAM_3111.JPG
   
 10. C.Thady

  C.Thady JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2015
  Joined: Jan 4, 2015
  Messages: 580
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asanteh kwa hilo somo kesho napika
   
 11. born to win

  born to win JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2015
  Joined: Jun 21, 2015
  Messages: 567
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Mkaa unawekwa juu na chini?
   
 12. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2015
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  Ndio. Mkaa unaweka juu na chini
   
 13. M

  Mama fetty New Member

  #13
  Mar 26, 2016
  Joined: Feb 10, 2016
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  NAOMBA vipimo vya cake kubwa
   
Loading...