Naomba nisaidiwe hivi mbunge wa viti maalum akifariki nafasi yake hujazwa?.

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
883
337
Hivi mbunge wa viti maalum akifariki nafasi yake hujazwa?na kama hujazwa je mbunge atakayeteuliwa ni lazima atoke ukanda wake ule au anatoka kokote?na kama hujazwa je nafasi ya regia mtema imejazwa na nani?na katoka wapi?
 
kunakuwa na list toka mwanzo, kwahiyo huwa si suala la kuchagua au kufuata ukanda, wanarejea orodha na kumjua anayefuatia.
 
kunakuwa na list toka mwanzo, kwahiyo huwa si suala la kuchagua au kufuata ukanda, wanarejea orodha na kumjua anayefuatia.

Je utaratibu wa aina hiyo si unaweza kumshawishi yule aliyeko kwenye nafsi ya pili kum-polonium mbunge aliyeko mbele yake kusudi yeye ajaze nafasi hiyo?
 
Hivi mbunge wa viti maalum akifariki nafasi yake hujazwa?na kama hujazwa je mbunge atakayeteuliwa ni lazima atoke ukanda wake ule au anatoka kokote?na kama hujazwa je nafasi ya regia mtema imejazwa na nani?na katoka wapi?
hujazwa. Nafasi ya regia mtema imejazwa na mama mmoja anaitwa cecilia paresso, toka Karatu(km sikosei) na aliapishwa siku moja na mbunge wa Arumeru mash. mh Nassari. Swala ninalojiuliza, mbona aliyefariki aliwakilisha Morogoro, alafu mrithi wake katoka kwingine? Hamna zengwe hapa?
 
Huu siyo utaratibu wa tume bali ni wa CHADEMA chama makini ambacho utaratibu wake upo kwenye katiba ya CHADEMA juu ya kuwapata wabunge viti maalumu hapa hakuna zengwe.

Kumbuka kifo cha Amina Chifupa alikuwa anawakilisha vijana lakini Rais kama mwenyekiti wa CCM alimteua mama Ishengoma kuchukua nafasi ya Amina.Hii anaonyesha kuwa CHADEMA siku zote haki inatendeka na hakuna zengwe.
 
Ni utaratibu wa tume mkuu, kwa kawaida kunakuwa na orodha ya majina inayopelekwa tume, orodha ile ndiyo inayofuatwa kwa kuzingatia vigezo ambavyo chama kilifuata na kupata orodha hiyo. CCM walikuwa wanatumia neno "WABUNGE WA KWENYE KAPU" ukienda kwenye Website yao utaikuta orodha hiyo, kwahiyo anayefuata "BAADA YA KUFA MWINGINE" anajijua. Hapo rais hana madaraka.

Kumbuka: Alivyofariki Mh. Amina Chifupa Mama Christine Ishengoma alijaza nafasi hiyo
Alivyofariki Mh. Salome Mbatia Mama Getrude Mongela alijaza nafasi hiyo
 
Back
Top Bottom