Naomba nipumzike kila nikipenda naishia kuumizwa.

njachama

Member
Feb 5, 2019
55
125
Habari wana jf hususani jukwaa hili.
Kwamara ya kwanza nimejitokeza kwenu lakini nitawasimulia machache kati ya mengi niliyonayo moyoni.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 40 sasa, mzaliwa wa kanda ya ziwa.

Ndugu zangu nielekee kwenye simulizi zangu kama utangulizi unavyosomeka hapo juu, nimejisikia kuwaandikia ili nanyi mpate kujisomea lakini kujifunza au kukumbushana kwa wale waliofikwa maumivu kama yangu.

Kwa muda wote niliojaaliwa kuishi mpaka kufikia leo nimewahi kuwa na marafiki wapenzi kadhaa katika safari yangu ya maisha.

Lakini nasikitika kila ilipofikia hatua fulani ambayo ilitamanisha kuifikia kila aliye na mahusiano ya kimapenzi nilijikuta naumizwa .

Ndugu zangu maumivu ya mapenzi yanauma kuliko jeraha, Kwakweli wapenzi wangu hao niliokua nao katika vipindi tofauti nilijitahidi kuwafanyia yale mazuri ambayo kila mwenye mpenzi angeweza kumfanyia anayempenda.

Kila niliyempenda nilimuonyesha mapenzi ya kweli yaliyojaa uaminifu ,ukweli na uwazi katika sehemu zote lakini nasikitika yote ilikua kazi bure, kila penzi lilipofika mwisho maimivu yalibaki upande wangu.

Wakati mwingine nilijiuliza wapi nilikosea mbona malipo niliyoyapata hayakulingana na mapenzi niliyowaonyesha.

Nianze na wa kwanza , huyu mwanamke niliamini nimefika hata nilidiriki kuwaza moyoni tutazikana .Siku moja nili mueleza napaswa nisafiri na nitarudi baada ya wiki aliniandalia kila kitu tayari kwa safari, alinisindikiza mpaka stendi na tuliagana vizuri huku tukiombeana heri safarini.

Nilisafiri na kufika salama , nilipofika nilimkuta mwenyeji ana hali mbaya nami kufika kwangu ndiyo ulikua msaada wa pekee.

Sikuweza kulala nilisafiri na mgonjwa wangu na kufika nyumbani usiku, nilipofika niligonga hodi bila mafanikio hatimaye mama mwenye nyumba alinifungulia geti na nilisogea mlangoni kwangu na kugonga bila mafanikio ,kwa bahati tuligawana funguo nikafungua na kuingia ndani hakikua na mtu.

Nilikosa wa kuniuliza, lakini nilipiga moyo konde nilichokumbuka ni kutoa godoro la ziada na kumuwekea mgeni wangu alale,
nami niliingia kitandani na kujilaza bila ya kupata usingizi mpaka kunakucha.

Ilipofika asubuhi wakati natafakari nianzie wapi nilisikia mlango ukigongwa nikaitika namuona mpenzi wangu anaingia akataamaki uso wake na wangu, akaingia na kutoka alipoenda nje nilimsubiri bila mafanikio hakurudi tena aliniacha kinywa wazi kwa mshangao.

Nilisubiri bila mafanikio pamoja na jitihada nilizofanya ili arejee zilishindikana,
Nilijipa muda kutafakari yaliyotokea lakini siku zilipita miezi ikasonga ndipo nilipoamua kuanza mahusiano mengine.

Huyu naye nilifanya kila nilichoweza kwa sehemu yangu ili kufanya mapenzi yetu yawe na furaha na amani.
Nilliishi naye bila kugundua tofauti yoyote kipindi nilichokua naye.

Baada ya miezi kadhaa nilianza kugundua tofauti ingawa nililazimika kuvumilia ili nione yatazidi au kupungua. Lakini kama wasemavyo waswahili jasiri haachi asili,
Polepole mambo yake yalidhihirika.

Wakati niko naye kumbe alikua na mahusiano mengine ambayo alikua akiendelea nayo. Lakini si hilo tu bali alikua na tabia kila ninapotoa msaada upande wa familia yangu uliohusu pesa alikua hapendi.

Kilichonishangaza zaidi aliponambia matatizo ya nyumbani kwao nilitoa pesa na zilitumwa na alikua na amani yote. Nilijiuliza kwanini iwe tofauti inapokua upande wangu?

Basi niliendelea na shuguli zangu za kutafuta uchumi huku nikisafiri siku kadhaa na kurudi. Ndipo siku moja tulipoamka asubuhi akaniambia anataka kusafiri kwenda kwao kusalimia nilimuandalia safari yake na nilimsafirisha.

Tangu aliposafiri nikimpigia simu usiku haipatikani, asubuhi sana haipatikani nikiomba kuwasalimia watu wa familia yake ananizungusha , nilifanya hivyo mara kadhaa bila mafanikio .

Siku moja nilifanya safari ya kushtukiza kwenda kwao nilifika na kumkuta mama yake tulisalimiana ndipo aliniuliza mwenzio hajambo? Nilimjibu mbona ana siku kadhaa amesafiri kuja kusalimia ,
Ndipo mama alishangaa kusikia hivyo .

Niliumia sana kiasi niliwaza na yale ya mwanzo , nikasema moyoni kwanini mimi? Kwa uchungu niliokua nao niligeuza sikua na raha tena ya kubaki pale.

Mama naye alichanganyikiwa kwa kupata taarifa hiyo, nikiwa kwenye gari narudi nilimpigia simu nikimjulia hali , huku nikimuuliza vipi hali ya mama na wanafamilia wengine alinijibu kwa kujiamini bila kujua kinachoendelea.

Nilipofika nyumbani kwangu nilitafakari
maumivu yanayoniandama. Lakini nilishindwa kuvumilia maumivu niliyonayo na niliamua kumpigia na kumueleza ukweli , alitaharuki na hakuamini kilichotokea.

Yeye alijiamini sana huku akidhani nitaamini kila alichonieleza , hatimaye huyu naye aliniachia maumivu ya kunijeruhi moyo.

Lakini nilimweleza maamuzi yangu kwamba nimefika mwisho naye...nilipokata nilifuta kumbukumbu zake kwenye simu na kukaa huku nikitafakari,
Hakika mahusiano haya yaliniumiza mfurulizo.
Natamani nimalizie kuwasimulia maumivu niliyoyapata kwa mpenzi wa tatu na wa nne lakini ninahofu ya kuwachosha wana jukwaa kwa kusoma kisa kirefu.

Hivyo nawaomba msome hapo kisha nitawamalizia visa vilivyosalia kwa wapenzi waliosalia tukutane tena kesho kwa muendelezo wa simulizi hii ya kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
3,991
2,000

Never ever take a woman serious in your life....kama unataka amani in future.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,659
2,000
Chief umenizidi miaka mingi sana.

Huu mwaka wako wa 40 unalilia penzi haya mambo mi nilifanya kidato cha tatu.

Anyway shit happens.

Nahisi umeanza mapenzi ukubwani.

Overtime utagundua kua hizi nyingine ni comedy tu za maisha.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom