So touching, hadi nimekupenda Beatrice😘😘😘Naomba Chadema mnielewe vyema na mjitafakari Sana kuhusu mjadala ulioanzishwa na Zitto na baadaye Mwandishi wa habari na ndugu yetu Erick Kabendera kuingilia Kati. Kwanza tunapaswa kujua Erick Kabendera ni nani kwenye mfumo wa siasa na amechangia vipi awamu ya tano kuingia madarakani kabla awamu hiyo kumkamata na kumweka ndani.
Erick Kabendera, Januari Makamba, Kinana, Nape na wengine kumbukumbu zinaonyesha wao ndio walioshiriki kuhakikisha kwamba Lowasa anashindwa uchaguzi 2015. Hawa watu ndio walioshirikiana na baadhi ya vijana wa IT kuiba uchaguzi uliomweka madarakani JpM. Nape wiki Ili aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter akijinadi kwamba bila yeye Lowasa angekuwa Ikulu. Alitaka kumwonyesha Polepole kwamba yeye Nape kwenye CCM ni Nani.
Baada ya awamu ya Tano kuingia madarakani JPM Nadhani makubaliano au mategemeo ya akina Kinana yalibadilishwa na ndipo mfumo ulipoanza kupambana nao bila kujali ushiriki wao kwenye Vita ya kuwaungiza madarakani. Walisambaratishwa mmoja baada ya mwingine Hadi ilipozaliwa mfumo mpya. Na hata baada ya kusambaratishwa na kwakuzongatia Bado watu Hawa walikuwa na wafuasi nyuma Yao JPM Nadhani ndipo alipoamua kutowatumia Tena kwenye uchaguzi kama viungo wachezeshaji, in short waliwekwa bench na rigging ya election ikafanyika kwa style tuliojionea.
Kwa kuwa Erick alitambua dhambi iliyokuwa nafsini mwake kuhusu tawala za afrika ilimlazimu kuingia kwenye mazungumzo may be ikiwemo kuomba msamaha kwa sababu anajua wapi alikengeuka. Nimeona kwenye post yake anakiri walifanya vikao zaidi ya 50 na JPM Hadi yeye anatolewa gerezani. Tujiulize Erick ni nani hadi afanyiwe vikao 50 ? Alikosa Nini? Vikao vilihusu Nini? Hakuna aliyejua Erick aliwahi kufanyiwa vikao vya usuluhishi akiwa gerezani hadi Leo alipoandika mwenyewe tweeter. Na kwa muktadha huo lazima tutambue Erick SI mtu mdogo ni mtu mwenye nafasi au alikuwa na nafasi flani kwenye mfumo.
Kwanini nawataadharisha CHADEMA kuhusu Erick, nikwasbabu Mbowe Hana kosa alilotenda lakini Erick alikuwa na makosa yake yakupingana au kushindwa kukubaliana na wenzie alioshirikiana nao kwenye uchaguzi 2015.
Lakini pia nawataadharisha CHADEMA dhidi ya Erick kwa sababu kwa sasa Erick na watawala akina Januari Makamba ni kitu kimoja. Kuwa mwanaharakati sometimes Kuna saidia lakini lazima tuwaangalie vyema hawa wanaotumwa kujadili hoja ya maridhiano wanatumwa na Nani? Kukubaliana nao sometimes nikukubali kununua haki Yako.
Erick na Zitto wamewahi kupingana na utawala uliopo kwa chochote? Means kwa Sasa hawa pia ni watawala ila hawana nafasi zinazoonekana Kwa macho. Madhara ya Mbowe kwenda kwenye mazungumzo kwa kuwasikiliza akina Erick nikufungua milango ya kuzimwa kwa agenda ya katiba mpya iliyopelekea Mbowe awe ndani Leo. Lakini majadiliano yenye masharti upelekea uliyekubaliana naye kukudhibiti kwa masharti yale Yale .
Nikubaliene n wanaounga MKONO kwamba waliomweka Mbowe ndani ndio wenye makosa na ndio wenye maamuzi afungwe au afutiwe Kesi. Endapo tukiruhusu majadiliano tukubaliane na masharti ya majadiliano, lakini kwa kuwa tunaamini kama Taifa kuwa Mbowe Hana kosa basi tubaiki na msimamo wetu kwamba tuache mahakama iamue kumfunga lakini tubaki na moyo thabiti wakuendeleza mapambano dhidi ya demokrasia.
Hatuwezi tukafanya mazungumzo kuhusu mwenyekiti tukawa na nguvu yakuwanyamazisha akina mdee, lazima tutalazimika kufanya mazungumzo nao. Tuache wakosaji wafanye wazungumzo, MBOWE SIYO MKOSAJI.
Umeolewa?