Naomba nikiri Tu kuwa Huyu Mgombea tuliyemsimamisha Huko Buyungu ni mzee

Ukweli usiopingika Huyu Mgombea tuliyemsimamisha kugombea Huko Buyungu ni kikongwe na anahitaji kupumzika baada ya kulitumikia Taifa kwa Muda mrefu kama Mbunge na Waziri.
Naomba tusirejee tena kosa kama hilo la kuwapitisha wazee. Wacha wapumzike wale Pension fund Zao.
Hivi huko hakuna kijana wa kuweza kusimama mpaka apitishwe huyo?
Anyway ni Mbunge atakayetokana na CCM yetu tuungane tuwe wamoja.
Narudia tusirudie kosa la Kumpitisha Mzee sehemu nyingine yoyote ile. CCM tuna vijana wengi tena wasomi wakubwa sio kung'ang'ania wazee.
Tuwaache wazee wetu wapumzike.
Ahsanteni sana Nawatakia utekelezaji mwema.
CCM OYEEEE!!!!
Hapana jamaa, tusiwabague watu kisa umri mkubwa haha wazee hawana ufisadi kwa sana na ni watetezi wazuri wa wananchi mfano mzuri ni mbunge wa mpwapwa waliwahi mtosa lakini baadae wananchi waliona wamechemsha wakamrudisha tena..
 
Mleta mada kifupi nikwambie hilo ndio tatizo alifanya Lowasa kudharau wazee akawa anakimbizana Na vijana akasahau kuwa kuna Amri ya Mungu inayosema waheshimu wazee upate heri iwe ya kisiasa Na maisha marefu duniani inasema waheshimu baba Na mama yako awe wa kuzaa au wa rkisiasa upate maisha marefu ya kisiasa ,kibiashara nk yenye heri duniani.Hicho kigombea chadema hakina heri ya wazazi wake kiishapiga mama yake makofi Na kikafukuzwa Na baba yake nyumbani hakitashinda.Kipagani wazee ndio washika mikoba iwe ya ushindi wa kisiasa nk ukiwadharau wazee imekula kwako hawakupi mikoba ya uchawi ya ushindi Lowasa alinyimwa Na hako katoto kabungu hata kama kiapagani hakashindi kwa dharau kalikonazo kwa wazee.Pia katiba inasema binadamu wote ni sawa hivyo hata babu Na Bibi ana haki ya kupiga kura Na kupigiwa kura.
Sina maana ya kumbagua mimi ninachoona ni kuwa tuwaache wazee wetu wapumzike kwani Wamelitumikia Taifa letu kwa Muda mrefu sana. Tuwape nafasi na wengine ili wale keki ya Taifa. Sidhani kama alikosekana mtu ambaye ni anafaa kugombea. Ila kubebana bena ndio Tatizo letu Watanzania.

Taifa tuongoze kwa Zamu
 
yaani mimi niseme tu huyu mgombea wetu hauziki ,kila unapopita kumuuza tunaambiwa ni mzee, baadhi ya maeneo wanatuambia tunamuuza bata, hauziki kabisa
Lakini Atakuwa Mbunge... Ninachoona mimi tungemwacha tu Apumzike jamani CCM yangu
 
Sina maana ya kumbagua mimi ninachoona ni kuwa tuwaache wazee wetu wapumzike kwani Wamelitumikia Taifa letu kwa Muda mrefu sana. Tuwape nafasi na wengine ili wale keki ya Taifa. Sidhani kama alikosekana mtu ambaye ni anafaa kugombea. Ila kubebana bena ndio Tatizo letu Watanzania.

Taifa tuongoze kwa Zamu
Hilo nalo neno sasa wanataka nao waendelee kusikika kina Babu. Muuache amalizie hii miaka akipita lakini.
 
Back
Top Bottom